CHADEMA jifanyieni tathmini

Hao hao Polisi hua mnawaita POLISICCM na Lissu huwa anawaita haya mapolisi leo mbona mnakua na mahaba nao kiasi hicho?
 
..I agree.

..Swali langu ni, polisi walichukua hatua gani?

..Siamini kwamba taarifa kama ile inahitaji kuwa rasmi ili IGP aifuatilie.
Nitashangaa sana kama Polisi watasikia habari zinazohusu usalama wakakaa kimya kwasababu si rasmi wakisubiri ajitokeze mtu kuripoti.

Najiuliza hivi, ni nani aliyefikisha malalamiko ya mtu kutishia maisha kwa 'face book' na inakuwaje hakuna aliyeripoti, Polisi bado wakamtia mtu mbaroni!!!
 
4. Kuna Wabunge akiweno Nape wamepeleka taarifa rasmi kuhusu kufuatiliwa, nini kimetokea!

Labda wanafuatilia na wakishajua kulikoni wataufahamisha umma au watawafahamisha watoaji taarifa.

Hayo mambo huchukua muda kuyafanyia uchunguzi.
 
Hao hao Polisi hua mnawaita POLISICCM na Lissu huwa anawaita haya mapolisi leo mbona mnakua na mahaba nao kiasi hicho?
Hakuna mahaba kuna maswali juu yao. Soma vizuri uelewe

Pili, wao ndiyo mamlaka inayochunguza tukio hili. Kwa namna inaonekana kuna kujichanganya

Mfano, Polisi wanamtaka dereva wa TL ajisalimishe Dodoma au Dar
Ukisikiliza taarifa ile ni kama vile dereva 'ni mtuhumiwa' kwa jinsi ilivyoelezwa

Dereva wa TL ni mtu muhimu sana katika uchunguzi huu kwani matukio yote ya nyuma na hili la sasa amekuwa ni sehemu yake. Umuhimu wake ni katika kusaidia uchunguzi kwa taarifa
Kuna mambo mawili
1. Anaweza kuwa shahidi ikiwa watuhumiwa watapatikana
2. Anaweza kuwa mtuhumiwa ikiwa ushahidi utapatikana

Katika hali hizo, suala ni kumpata kama mtu muhimu katika uchunguzi na si 'mtuhumiwa'

Kwa maelezo ya kumtafuta dereva yule, unaweza kuona ni kama kuna 'conclusion' fulani kabla ya uchunguzi au wakati uchunguzi unaendelea. Kwa tukio la TL kunahitajika weledi kinyume chake ni kuongeza mashaka yasiyo ya lazima kwa wanaofikiri hata kama fikra zao ni mbovu
 
Kuna sababu kwa nini zipo njia zilizo rasmi za kutoa taarifa polisi.

..mimi naona yule mzee kadanganya.

..he dropped the ball and he was not a man enough to admit it.

..ngoja nikupe mfano mwingine ujue CDM wanafanya kazi ktk mazingira gani.

..mikutano ya siasa ilizuiliwa. Sasa CCM wakawa wanatimiza miaka 50 na wakafanya mkutano mkubwa wa hadhara. CDM walipohoji kwanini wenzao wameruhusiwa kufanya mkutano, wakajibiwa huo sio mkutano ni maadhimisho.

..mwezi huu CDM nao wakawa na maadhimisho lakini wamezuiliwa mikutano ya hadhara, na kuna maeneo kama Geita wamezuiliwa hata mikutano ya ndani.

..hakuna HAKI.
 
Mkuu huyo dreva kasema aliona gari likiwafatilia akamshaur Lissu asishuke sasa huon hapo anaweza kuwa kashka number za gar kchwan? pili akieleza kuwa lilianza kuwafatilia kuanzia point A mpaka C huoni polisi wakienda point A mpaka C na kuulizia watu wanaweza kuwa na description ya hiyo gar na kupata pa kuanzia?

Mwisho soma taarifa ya mara ya kwanza iliyotolewa ya watu walioenda Nairobi na mgonjwa ilielezwa ni Mbowe,Msingwa na mke wa Lissu baada ya kuona Dreva anahitajika polisi hapo hapo nae akajumuishwa kuwa yupo Nairobi hahaaaaaa
 
Labda wanafuatilia na wakishajua kulikoni wataufahamisha umma au watawafahamisha watoaji taarifa.Hayo mambo huchukua muda kuyafanyia uchunguzi.
Well said, ndiyo maana tunauliza kulikuwa na sababu gani za kutangaza wanamtafauta dereva wa TL? Kuna sababu gani za kueleza wamekamata magari 10? Kwanini wasifuatilie kimya kimya kama wanavyofanya suala la Wabunge walioripoti

Hoja yangu ni kuwa ''cherry picking' inaongeza ugumu katika kazi yao hasa suala la credibility
 
Shida ni vyombo vya dola vinapokuwa sehemu ya ccm, au umesahau ile marufuku ya vikundi vya ulinzi? Shame on you for having long term memory loss!
 
Sijui hata unazungumzia nini

Sikiliza, nimeandika kuwa dereva wa TL ni muhimu sana kwasababu matukio ya nyuma na hili la sasa amekuwa ni sehemu yake. Katika uchunguzi huyu ni mtu muhimu sana ili kupata mwongozo. Hili umeelewa nadhani na sitarajii kama utauliza tena

Pili, nikasema Polisi wanapomtaka katika hali ya 'mtuhumiwa' wanajinyima fursa
1. Anaweza kuwa shahidi mbele ya safari kwa maana hiyo unayosema ikiwemo namba, watu,aina gari, majira, ilianza lini n.k. Hili nadhani umeelewa sitarajii utauliza tena

2. Anaweza kuwa mtuhumiwa ikiwa kuna ushahidi utakao mu implicate na suala zima
Katika uchunguzi kila kitu kinakuwa mezani na kinaangaliwa kwa undani.
Hii ni nadharia tu na sidhani kama hujaelewa na utauliza tena.

3. Kwavile ni mtu muhimu kilichotakiwa ni kushirikiana naye si kuanza 'kumuonyesha kama mtuhumiwa''.

Uchunguzi ni udadidisi ambao mwisho huwa na matokeo iwe chanya au hasi

Nikueleza jambo moja ikitokea upo eneo la uhalifu kuna sababu nyingi Polisi waakuhitaji
1. Kuwapa mwongozo wa nini kimetokea ili waweze kuendelea na uchunguzi
2. Uwepo wako unaweza kuwa ni shahidi kama yule wa serikali dhidi ya kesi ya TL
3. Unaweza kuwa mtuhumiwa wa tukio pia

Nadhani umeelewa
 
wapi polisi wamesema wanamtaka dreva kama mtuhumiwa?
 
CHADEMA wanashangaza sana.

Wana mentality ya utegemezi.

Utegemezi wa serikali ya CCM.

Sijui wataamka lini tu!!
Wewe kila mtu akitembea na bastola nchi hii ulishaambiwa asilimia 90 vichaa
 
Mbona wanapotaka kufanya mikutano ya siasa au maandamano mnawataka wakaombe vibali na ulinzi mahali fulani? What BS are you talking about?
 
Kwa statement yako,unatuaminisha Tanzania si mahala salama? Kwa nini tuanze kuishi kwa hofu? Kwa nini CHADEMA wasiamini ulinzi wa serikali kwa raia wake?
Anyway,yaweza kuwa unawapa pa kuanzia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya ccm yanawashinda unadhan ya chadema utayaweza? Pambanen na hal zenu za kwetu mtuachie wenyewe.

Ya ngoswe mwachie ngoswe

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa katoa ushauri mzuri sana ..Ni vyema CDM wajitathimini Hata mimi huwa hainiingii akilini kwanini wanashindwa kujilinda wenyewe wanabaki kulalamika tu.Mungu azidi kutupa busara

Sent using Jamii Forums mobile app
 

na sio kuwa wanataka publicity?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…