CHADEMA itoe kwanza boriti kwenye jicho lake kabla haijatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzie

magu sam

Member
Jul 20, 2018
62
50
Katika ripoti ya CAG imefichua mambo mengi ya siri na hasa ufisadi wa kutisha ndani ya CHADEMA. Taarifa hiyo imeonyesha kiasi cha Tshs. 2,302,305,500/- zilizokusanywa kutoka kwa wahisani mbalimbali hazikupita katika akaunti ya bank ya chama na wala matumizi yake hayajaandikwa popote pale, Fedha hizo zilikusanywa kwa miaka miwili tofauti.

Kipindi cha 2014/2015 CHADEMA ilikusanya kiasi cha Tshs. bilioni 4 na 2015/2016 ilikusanya Tshs. 2,297,885,500/-. Fedha hizi zote zilikusanywa bila kupitia bank na matumizi ya fedha hizo hayajulikani kinyume na kifungu cha 15(1) cha sheria Na. 5 ya mwaka 1992 ya Vyama vya Siasa.

Matumizi ya Tshs. 24,216,625,390/- (bilioni 24) yalifanyika bila ya kufuata utaratibu kama inavyoagizwa kwenye sheria ya usimamizi wa fedha ya CHADEMA kifungu Na. 16.2.2.

Kwa hili lazima watu macho yawatoke kwenye Muswada wa Vyama vya Siasa maana kuna ulaji unabanwa pale. Sasa na mambo kama haya basi nategemea Lisu atayaongelea pia kwani amekuwa akijifanya anapinga ufisadi.

Nakumbuka jinsi Lissu alivyomuita Lowassa kuwa ni fisadi mkubwa tena papa na baadaye akawa anapata kigugumizi cha namna ya kumsafisha. Inabidi sasa badala ya kuzunguka tu Ulaya kuichafua Serikali ya awamu ya tano, pia akemee ufisadi mkubwa unaoendelea kwenye chama chake na wazungu wausikie (asiwe biased).


Na Munir Omary
 
Back
Top Bottom