CHADEMA itabaki kuwa CHADEMA tu

Ni mawazo yangu niombe radhi kutoa maoni yangu,

Lowassa na Duni waligombea wenyekiti?

Leo brother utalala na viatu, hutaki mimi nijadili nje ya Mbowe, lakini yoyote akijadili unahusisha na nafasi ya uenyekiti!!
 
Kwahiyo kama tumedandia mada ulitaka uanzishe mada uchangie peke yako tu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ndiye niliyeanzisha sijalazimisha mtu kuchangia, asipochangia yeye atachangia mwingine na mimi siyo mgeni humu sijawahi kumuita mtu aje kuchangia.
 
Leo brother utalala na viatu, hutaki mimi nijadili nje ya Mbowe, lakini yoyote akijadili unahusisha na nafasi ya uenyekiti!!
Point yako ni moja tu unataka Mbowe aachie madaraka kwa vile kakaa muda mrefu, umeeleweka.

Mimi nimekujibu kuwa Mbowe hawezi kutolewa kwa propaganda za CCM atatolewa na wana Chadema wenyewe.
 
Nimekuelewa, nilikuwa nawakumbusha historia ya Chadema watu walioanza kusema kwa ujio wa ACT Chadema inakwenda kufa.
 
Mali ngapi za Mbowe zimevurugwa na hana lolote alilofanya? Ukiniambia viongozi wa cdm hakuna anayetaka kugombea uwenyekiti nitakuelewa lakini sio kwamba Mbowe ndio mwenye uwezo kulingana na wakati wa sasa
Tindo, naona hutaki kuelewa ninachokieleza.
Kwa hali kama hiyo, najikuta sina njia nzuri ya kujieleza kwako ili 'ukubali' kuelewa ninachoandika, hata kama hukiafiki.

Tumekwishakubaliana umhimu wa kuwa na uchaguzi ndani ya CHADEMA, ili hata kama Mbowe akitakiwa aendelee kuongoza pasiwepo na lawama kama hizi unazoleta humu.

Sasa naona hata hiyo subira tu, ya kuruhusu hizi chaguzi zipite salama bado unaona huridhiki! Kuna agenda yoyote inayokupa msukumo huo? Hii haiwezi kutokana tu na kuwa shabiki mkereketwa wa chama!

Napenda pia ujue maslahi yangu ninayoyasimamia katika mijadala kama hii. Kukikosekana upinzani wenye nguvu Tanzania, tutaingia katika hali ngumu zaidi kuliko tuliyo nayo sasa hivi. Maslahi yangu ni kuona kukiwa na vyama imara zaidi ya chama kimoja. CHADEMA wakifanikiwa kushinda na kuunda serikali, bado nitatamani kuiona CCM na/au vyama vingine vikiendelea kutoa michango yao katika siasa za nchi hii. Sitapenda CHADEMA waivuruge/waifute CCM. Nitawapinga kwa nguvu zote.

Sasa nashindwa kuelewa hasa matakwa yako ni yapi.
 
Kama cdm ni taasisi basi utetezi wa kwamba Mbowe ndio anayefaa tu kwenye uenyekiti ni utani wa mchana kweupe.
Maneno haya yametoka wapi? "Mbowe ndio anayefaa tu kwenye uenyekiti".
Unapojadili mada na kuja na njia za namna hii kukazia hoja inakuondolea uhalali wa hoja zako.
 
Tutofautishe kumtetea Mbowe na kukitetea chama.

Hakuna anayemtetea Mbowe bali maslahi ya chama, hata Mbowe akiondoka bado wapenda demokrasia wataendelea kukitetea chama.
 
Nguo ikichafuka dawa yake siyo kuitupa ni kuisafisha hatuwezi kujua hata kuondoka kwa Lowassa inawezekana ni njia mojawapo ya kukisafisha chama.

Wakati wa magamba matatu CCM ilifanya kosa la kutaka kuwafukuza kina Lowassa, Rostam na Change lkn walikuja kugundua baadae wamekosea, leo hayo magamba ndiyo yamekuwa lulu kwa CCM.
 
ACT Wazalendo wanahitaji muda ili kujiimalisha hasa vijijini Chadema haijafika hapa over a single night.
 
Lowassa hakuletwa Chadema na Mbowe, tunavyojua tangu mwanzo Mbowe alikataa lkn kwa kuheshimu maamuzi ya kamati ilibidi akubali
 
Ulimsikia MBOWE akisema hatoki kwenye ueNYEKITI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…