Anayeiua Chadema ni Mbowe na ufisadi wake. Hela ya ruzuku anaitafuna kwa visingizio kebekebe. Utasikia alikopesha chama mabilioni wakati wa uchaguzi sasa anakidai chama mrejesho.
Swali ni vikao vipi viliidhinisha mikopo hiyo? Pili, mwenzetu ni benki? Tatu, hizo fedha alizitoa wapi kwa shughuli ipi? Nne, kwa matumizi yapi kwani sheria za uchaguzi zimeweka ukomo wa matumizi ya chaguzi.
Sasa kwa huu ufisadi Chadema imeshindwa kupeleka fedha mashinani na matokeo yake ukata umechangia baadhi ya madiwani kurubuniwa na ccm. CCM imegundua huu udhaifu wa Mbowe na wameugeuza kivuno.
Sasa wa kulaumiwa ni nani?
Pili, ujio wa Lowassa na kumkabidhi ugombea Urais aligeuza ni dili yake binafsi na kauli zake zinamtia hatiani. Alidai yeye ni nani amkatae Lowassa ambaye alikuja na wafuasi wengi.
Maswali yafuatayo hayana majibu..
Kwanza Mbowe wewe ni nani hadi uone suala la kugombea Urais ni lake binafsi? Kiongozi anayejiheshimu angesema tuwaulize wanachama kwa kura yao kupitia primaries ya mikutano ya wilaya nchi nzima waamue na kila anayetaka kugombea achukue fomu na wanachama waamue.
Pili, nafasi mbalimbali za uongozi kamati kuu ya cdm hutapika majina lakini wanachama hawaulizwi sasa ni demokrasia ipi mwenzetu anaitafuta wakati nafasi hii ndogo Mwenyezi Mungu aliyompa kashindwa kuonyesha wasifu wake wa demokrasia?
Tatu, hivi mwenzetu ulijuaje Lowassa kaja na wafuasi wengi kama siyo hisia zako binafsi? Labda utuelimishe kabla Lowassa kujiunga na cdm mlikuwa na wanachama wangapi na baada ya kujiunga mkawa na wanachama wangapi. Kwa taarifa yako, kwa takwimu nilizonazo idadi ya wanachama haikuongezeka eti kwa sababu Lowassa alijiunga na cdm. Hizi takwimu hukuziongelea kwa sababu uliona zingelikuumbua.
Maandiko yako wazi kama huaminiki kwa madogo nani atakuamini kwa makubwa hata yawe ni yako?
CCM ina matatizo yake na ingepaswa kuwajibishwa lakini kwa uongozi huu dhaifu wa Mbowe ambao sanasana ni mkao wa kula ni kheri kabisa ccm wakaendelea kutesa hadi pale wanachama wa Chadema watakapofanya kweli na kumtimua huyu fisadi mkubwa na wakajipanga upya.
Vinginevyo mtabakia kulalama badala ya kujilaumu wenyewe.
N.B:-
Dola ina jukumu kubwa la kulinda ruzuku zinazopewa vyama vyote vya siasa na kuhakikisha zinatumika kama zilivyokusudiwa na hii siyo siasa ila ni utawala bora.