CHADEMA isitafute mchawi, ni Mbowe

CHADEMA isitafute mchawi, ni Mbowe

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,504
Reaction score
911,249
Anayeiua Chadema ni Mbowe na ufisadi wake. Hela ya ruzuku anaitafuna kwa visingizio kebekebe. Utasikia alikopesha chama mabilioni wakati wa uchaguzi sasa anakidai chama mrejesho.

Swali ni vikao vipi viliidhinisha mikopo hiyo? Pili, mwenzetu ni benki? Tatu, hizo fedha alizitoa wapi kwa shughuli ipi? Nne, kwa matumizi yapi kwani sheria za uchaguzi zimeweka ukomo wa matumizi ya chaguzi.

Sasa kwa huu ufisadi Chadema imeshindwa kupeleka fedha mashinani na matokeo yake ukata umechangia baadhi ya madiwani kurubuniwa na ccm. CCM imegundua huu udhaifu wa Mbowe na wameugeuza kivuno.

Sasa wa kulaumiwa ni nani?

Pili, ujio wa Lowassa na kumkabidhi ugombea Urais aligeuza ni dili yake binafsi na kauli zake zinamtia hatiani. Alidai yeye ni nani amkatae Lowassa ambaye alikuja na wafuasi wengi.

Maswali yafuatayo hayana majibu..

Kwanza Mbowe wewe ni nani hadi uone suala la kugombea Urais ni lake binafsi? Kiongozi anayejiheshimu angesema tuwaulize wanachama kwa kura yao kupitia primaries ya mikutano ya wilaya nchi nzima waamue na kila anayetaka kugombea achukue fomu na wanachama waamue.

Pili, nafasi mbalimbali za uongozi kamati kuu ya cdm hutapika majina lakini wanachama hawaulizwi sasa ni demokrasia ipi mwenzetu anaitafuta wakati nafasi hii ndogo Mwenyezi Mungu aliyompa kashindwa kuonyesha wasifu wake wa demokrasia?

Tatu, hivi mwenzetu ulijuaje Lowassa kaja na wafuasi wengi kama siyo hisia zako binafsi? Labda utuelimishe kabla Lowassa kujiunga na cdm mlikuwa na wanachama wangapi na baada ya kujiunga mkawa na wanachama wangapi. Kwa taarifa yako, kwa takwimu nilizonazo idadi ya wanachama haikuongezeka eti kwa sababu Lowassa alijiunga na cdm. Hizi takwimu hukuziongelea kwa sababu uliona zingelikuumbua.

Maandiko yako wazi kama huaminiki kwa madogo nani atakuamini kwa makubwa hata yawe ni yako?

CCM ina matatizo yake na ingepaswa kuwajibishwa lakini kwa uongozi huu dhaifu wa Mbowe ambao sanasana ni mkao wa kula ni kheri kabisa ccm wakaendelea kutesa hadi pale wanachama wa Chadema watakapofanya kweli na kumtimua huyu fisadi mkubwa na wakajipanga upya.

Vinginevyo mtabakia kulalama badala ya kujilaumu wenyewe.

N.B:-

Dola ina jukumu kubwa la kulinda ruzuku zinazopewa vyama vyote vya siasa na kuhakikisha zinatumika kama zilivyokusudiwa na hii siyo siasa ila ni utawala bora.
 
sasa kama mbowe anaiua chadema, kwanini mnapoteza risasi zetu kwa kuwaua wapinzani, na pia mnamaliza makali ya mapanga kwa kuwakatakata kama nyama. Si musubiri mbowe amalizie kuiua taratibu
 
Mchango.jpg

Pesa kwanza uzalendo baadae.
 
Mkuu @Rutasubanyuma hili ni andiko zito sana kutoka kwa mshabiki au mwanachama wa Chadema ndani na pengine nje ya JF.
Nafahamu ulivyokuwa mtetezi mkuu wa Chadema hapa jamvini na of course kwenye field huko kwenye chimbuko la harakati kali za Siasa za upinzani kupitia Chadema.

Nakumbuka tuliwahi kuingia kwenye mikwaruzano mikali ya hoja katika threads na posts mbalimbali hapa jamvini.

Nilikuwa nashangaa sana kukuona ukiitetea Chadema iliyobadili gia angani na nikawaza hivi huyu great thinker na wengine unaofanania nao wanahitaji nini haswa kwa Taifa hili?
Yaani kuna kipindi mlikuwa mnaupinga ufisadi na magumashi ya CCM katika hali zote sasa ikawaje mkabadilika na kumuunga mkono mwanaccm aliyeichafua CCM?ikawaje mkambadilikia Slaa na kumuona ni wa hovyo kabisa?

Jibu langu likawa mtakuwa na maslahi muhimu ndani ya Chadema na hamtaki yavurugwe hata kama gharama yake ni kuusaliti ule umma uliokuwa unapinga ufisadi.

Leo hii ninapoona hii post ninashangazwa sana na kutoamini...au account yako imekuwa hacked?

Au kwa mara ya kwanza umeweza kupata fursa ya kumjua mbowe na inner cycle ya Chadema?

Kwa ufupi nakubaliana na wewe kuwa Ni heri ya ZIMWI LIKUJUALO...yaani CCM na changamoto zake ni bora sana mara 10000 kuliko Chadema iliyokaa kimaslahi zaidi.

The good thing about CCM wana machinery za kuwawajibisha mafisadi ,wezi na wahuni waliomo chamani na hivyo kuwa na uwezo wa kudhibiti Chama kuwa mateka wa watu wabaya.

Again...IAM PERPLEXED!!

Cc: BAK Crashwise Pascal Mayalla @TumainMakene wilbrod slaa Tundu Lissu
Yericko Nyerere Mchambuzi @mzeemwanakijiji
 
sasa kama mbowe anaiua chadema, kwanini mnapoteza risasi zetu kwa kuwaua wapinzani, na pia mnamaliza makali ya mapanga kwa kuwakatakata kama nyama. Si musubiri mbowe amalizie kuiua taratibu
Hii hoja ni nzito kwako tulia uelimike
 
mbona mnahanagaika sana ? dawa zinawaingia taratibu msijali
 
MBOWE si kiongozi bali ni shimo la urubuni lenye vichwa viwili vya habari....kimoja kujipendekeza kama mwanademokrasia..cha pili mchonganishi ambaye baada ya muda asipodhibitiwa atakuwa ni joka la mdimu litakalosababisha machafuko yasio na mwisho
 
Bandiko zito hili, wenye upeo mdogo wa kuchambua hoja hawatakubaliana na wewe. Ila Mbowe kadri alivyofanikiwa kujenga taswira nzuri ya chama, alikuja kuharibu sana 2015.

Mbowe namfananisha na Arsene Wenger, meneja wa Arsenal FC. Anaishi kwa past glory, lakini kwa sasa he's got nothing to offer.
 
Unaweza jiuliza maswal mengi lakin labda tu nikuambieni Mbowe ni CCm kabsaaaa
 
N.B:-

Dola ina jukumu kubwa la kulinda ruzuku zinazopewa vyama vyote vya siasa na kuhakikisha zinatumika kama zilivyokusudiwa na hii siyo siasa ila ni utawala bora
Una kiwango cha chini sana cha uelewa au unatumika kipropaganda. Fedha zote za chama zinaidhinishwa kwa mfumo rasmi na pia zinakaguliwa kila mwaka na CAG na kutoa ripoti. Jee hayo unayosema ya matumizi mabaya umeyatoa kwenye ripoti ya CAG au katika vibaraza vya Lumumba?
Hizo story zenu mbona zimeshachacha?
 
Anayeiua Chadema ni Mbowe na ufisadi wake. Hela ya ruzuku anaitafuna kwa visingizio kebekebe. Utasikia alikopesha chama mabilioni wakati wa uchaguzi sasa anakidai chama mrejesho.

Swali ni vikao vipi viliidhinisha mikopo hiyo? Pili, mwenzetu ni benki? Tatu, hizo fedha alizitoa wapi kwa shughuli ipi? Nne, kwa matumizi yapi kwani sheria za uchaguzi zimeweka ukomo wa matumizi ya chaguzi.

Sasa kwa huu ufisadi Chadema imeshindwa kupeleka fedha mashinani na matokeo yake ukata umechangia baadhi ya madiwani kurubuniwa na ccm. CCM imegundua huu udhaifu wa Mbowe na wameugeuza kivuno.

Sasa wa kulaumiwa ni nani?

Pili, ujio wa Lowassa na kumkabidhi ugombea Urais aligeuza ni dili yake binafsi na kauli zake zinamtia hatiani. Alidai yeye ni nani amkatae Lowassa ambaye alikuja na wafuasi wengi.

Maswali yafuatayo hayana majibu..

Kwanza Mbowe wewe ni nani hadi uone suala la kugombea Urais ni lake binafsi? Kiongozi anayejiheshimu angesema tuwaulize wanachama kwa kura yao kupitia primaries ya mikutano ya wilaya nchi nzima waamue na kila anayetaka kugombea achukue fomu na wanachama waamue.

Pili, nafasi mbalimbali za uongozi kamati kuu ya cdm hutapika majina lakini wanachama hawaulizwi sasa ni demokrasia ipi mwenzetu anaitafuta wakati nafasi hii ndogo Mwenyezi Mungu aliyompa kashindwa kuonyesha wasifu wake wa demokrasia?

Tatu, hivi mwenzetu ulijuaje Lowassa kaja na wafuasi wengi kama siyo hisia zako binafsi? Labda utuelimishe kabla Lowassa kujiunga na cdm mlikuwa na wanachama wangapi na baada ya kujiunga mkawa na wanachama wangapi. Kwa taarifa yako, kwa takwimu nilizonazo idadi ya wanachama haikuongezeka eti kwa sababu Lowassa alijiunga na cdm. Hizi takwimu hukuziongelea kwa sababu uliona zingelikuumbua.

Maandiko yako wazi kama huaminiki kwa madogo nani atakuamini kwa makubwa hata yawe ni yako?

CCM ina matatizo yake na ingepaswa kuwajibishwa lakini kwa uongozi huu dhaifu wa Mbowe ambao sanasana ni mkao wa kula ni kheri kabisa ccm wakaendelea kutesa hadi pale wanachama wa Chadema watakapofanya kweli na kumtimua huyu fisadi mkubwa na wakajipanga upya.

Vinginevyo mtabakia kulalama badala ya kujilaumu wenyewe.

N.B:-

Dola ina jukumu kubwa la kulinda ruzuku zinazopewa vyama vyote vya siasa na kuhakikisha zinatumika kama zilivyokusudiwa na hii siyo siasa ila ni utawala bora.
Hizi akili za kusaidiwa kufikiri sasa...sasa kama anaiua chadema Kuna shida gani,si mkakati ni kuiua CDM? Si ina maana anawasaidia kuimaliza? Sasa mbona nyinyi wenyewe mwa mlalamikia yule Atekeleza tamanio lenu? Kila siku mwabadili headings but content ile ile tu
Mbowe ni usalama wa taifa
 
Back
Top Bottom