Chadema is not perfect but it is ideal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema is not perfect but it is ideal

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Mar 19, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mtanisamehe kwa kukosa maneno fasaha ya Kiswahili kutuma ujumbe uliobebeka katika kichwa cha habari, Lakini nadhani tafsiri ya kuungaunga ni kwamba CHADEMA sio MALAIKA ila ni afadhali kuliko CCM. Mtanisamehe kwa upungufu nilionao katika Lugha ya Taifa, nadhani ujumbe umewafikia.

  Nijielekeze kwenye hoja ya msingi, Ghafla, katika namna ambayo mfuatiliaji yeyote wa maswala ya siasa angeitegemea kumetokea Watanzania wenzetu wengi waliojikita hasa hapa JF katika kukipaka matope Chama cha Democrasia na Maendeleo bila shaka lengo kuu likiwa ni ama kuonyesha kwamba hata chenyewe ni chama kichafu kama chao ama Viongozi wake nao ni wachafu kama wao.

  Japokuwa hii hoja ni pana sana, naomba niifupishe kwa kuweka wazi kwamba, Watanzania tuna options mbili tu, ama kuichagua CCM ama kuichagua CHADEMA, na katika hili niseme wazi kabisa kwamba vyama vingine vyote ni hovyo hovyo kama tulivyozoa kumsikia MR BEN a.k.a undertaker majukwaani siku za karibuni.

  Viongozi wa CCM na CHADEMA na mfumo mzima wa uendeshaji wa vyama hivi viwili sio PERFECT, wao kama binaadamu wanamapungufu yao na vyama hivi viwili kama matokeo ya Fikra za Mwanaadamu sio PERFECT. kuna mapungufu mengi tu na ukichukulia mfumo mzima unaoitwa wa kidemocrasia ulivyokuwa mfumo wenye misingi mibovu kuliko mifumo mingine haishangazi kabisa matokeo ya mfumo huo kuwa mabovu kwa maana ya vyote viwili, vyama shiriki vya democrasia na wanasiasa wenyewe.

  Kwa hapa tulipofikia watanzania, hakuna namna tunaweza tukasema tuutupilie mbali mfumo wa kidemocrasia ili tuachane na vyama hivi wala wanasiasa hawa, bahati nzuri Jamii kubwa ya Watanzania imeonyesha kuwa na imani na mfumo huu, hivyo bila shaka tutafaidika na labda tunafaidika nao.

  Misingi ya mfumo huu ni kuchagua mwanasiasa huyu na kuachana na mwanasiasa huyu au kuchagua chama hiki na kuachana na chama hiki, Watanzania tuko kwenye mchakato wa kuchagua na ni lazima tuchague, HATA VYAMA HIVI VIKIENDELEA NA MIKAKATI YA KUCHAFUANA NI NGUMU SANA KUICHAGUA CCM. ZAIDI WANACHOKIFANYA CCM NI KAMA VILE KUFURUGA HALI YA HEWA ILI WATU WASHINDWE KUCHAGUA. HAIWEZEKANI.

  LAZIMA TUCHAGUE
   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tunaposema ideal maana yake ni halisi, safi, isiyo na mawaa, isiyo na kosa, nyoofu, iliyofikia viwango vya juu kabisa. Mfano wake ni kupata mtu ambaye hatendi dhambi. Mtu huyo atakuwa ideal. Ideal kisayansi ideal ni hali ambayo kila kitu kinachoathiri jaribio au kitendo hakibadiliki badiliki.
  Kimsingi kupata kitu cha namna hii hapa duniani haiwezekani. Hii ni kwa sababu kama vitu vikiwa ideal maisha hayawezekani. Hebu fikiri kama barabara zizingekuwa na msuguano gari zingeweza kutembea? Ama fikiri kusingekuwa na msuguano kati ya hewa na eropleni angani. Je ndege zingepigaje kona, na je zingetuaje kama barabara zao zisingekuwa na msuguano. Hii ina maana kwamba zingeenelea tu kutembea.
  Niseme nini basi. Chadema kama chama kina mapungufu, lakini misingi yake inalenga kuwa na kitu ambacho ni ideal. Kwa sababu kinaendeshwa na watu ambao si perfect basi hatuwezi kusema kwamba hawafanyi makosa. Lakini pia tuangalie, kuna makosa ambayo kisayansi tunaita errors na kuna mengine tunaita blander. Error ni hitilafu ndogo kutoka kwenye kizio au lengo. Lakini blander ni kwenda mbali kabisa na kizio. Mfano unatoka Mwanza kwenda dara halafu unakwenda kutua Kinshasa. Hii ni blander. Lakini erro ni sawa na kusafiri kutoka Dar badala ya kutua kia unatua Kiwanja cha Moshi mjini.
  Sasa tukiangalia CCM na nia yao ya ufisadi, wamefanya blander, tukiangalia nia yao ya maisha bora wamefanya blander, tukiangalia nia yao ya umeme wa uhakika wamefanya blander, .......
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Chadema ndio cha pekee kilichobaki hapa Tanzania kuwakomboa wanyonge but ccm ilishakufa since Nyerere alokufa na hila za Mkapa.
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Siasa zinazoendeshwa na CCM hivi sasa ni hatari zaidi kwao wenyewe kuliko wanavyotegemea, wanashindwa kuelewa kwamba Nyuma ya CHADEMA kuna nguvu kubwa sana ambayo sio nguvu ya kisiasa. Nyuma ya CHADEMA kuna watu wanaotaka mabadiriko hawataki kusikia siasa.

  Kwanza watu wamegundua kwamba wamefanywa kama mandondocha kwa muda mrefu sana, kisha wamegundua kwamba ni Kweli kabisa Maisha bora kwa Kila mtanzania yanawezekana, na wamegundua kikwazo ni CCM, watu wanataka kuona watoto wao, watoto zao na wao wenyewe wanapata elimu bora inayokidhi changamoto za kuchangamana na Jamii nyingine, watu wanataka huduma bora za afya, watu wanataka umeme na maji ya uhakika, watu wanataka kuwa na uhakika wa kula na kuvaa, watu wanataka makazi bora, SASA UNAPOONA WATU WANAHUSISHA MAMBO HAYA NA PROPAGANDA ZA KISIASA UNASHINDWA KUELEWA WANAFIKIRIA NINI.

  Mimi niwashauri CCM kuwa kama wanawake, katika changamoto za maisha wanazopitia wanawake ama mabinti kwa ufasaha zaidi ni misukosuko ya kutongozwa na wanaume tofauti tofauti, hivyo wanachokifanya wanajifanya wao swala na wanaume simba, then wanaamua kujilegeza kwa simba aliyenona na kukamatwa kuliko kukamatwa na simba choka mbaya, huyu anakula mpaka mifupa. hii ni kwa mjibu wa x-class mate wangu mmoja binti chuoni.

  sasa CCM waamue kuondolewa au kukabidhi madaraka kwa CHADEMA ili kuwe na smooth transition, au la watakabiliana na unorganized pressure kutoka kwa UMA kama inayoendelea kuzikumbuka nchi za kiarabu na kuwafikisha watawala kwenye vifo vya aibu au kujificha mapangoni kama mahayawani.

  CCM wasifikiri kwamba kushinda uchaguzi kuna mantiki yoyote ile kwa maisha ya watanzania, watanzania wanakiu kubwa sana ya mabadiriko. mimi nasema maneno haya kwa uoga mkubwa sana, sababu bado nina watoto wadogo, ntawaficha wapi dhoruba likitokea hapa jamani.

  CHONDE CHONDE CCM, HATA HUSSEIN MUBARAK WIMBI LA UMA LILIMKUTA AKIWA NDO ANATOKA KUSHINDA UCHAGUZI KWA KISHINDO. KWELI NASEMA, NI BORA MUACHIE MADARAKA JAPO HASIRA ZA WATU ZITULIE ZIKINGALI KINDA.

  CHELEA MWANA KULIA, ULIA MWENE
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kungekuwa na kitufe cha 'likes' ingetosha na mimi kushiriki kwenye hii thread. Kwa kifupi mdau umenena ila kuna ambao sasa povu linawatoka, kwa bahati mbaya hakuna namna hivyo ndivyo ilivyo.
   
Loading...