CHADEMA irudi kwenye misingi

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,305
2,563
Imefika wakati sasa CHADEMA irudi kwenye misingi iliyokuwa ikiisimamia hapo awali kabla Mwenyekiti hajabadili gia angani, ambayo ni mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa na kujitenga na wanasiasa ambao wana makando makando.

Kwasasa hivi Dr Magufuli anafanya kazi kubwa ya kupambana na genge la manyang'au lakini bado haitoshi, CHADEMA inapaswa kwenda mbele ya hapo kwa kumwambia Mh rais kwa mfano 'mbona flani na flani huwagusi?Tunataka pia uwashughulikie wale waliohusika katika kashfa za Richmond, EPA,Meremeta ESCROW, mabilioni ya Kikwete,Radar,mabilioni ya Uswisi,nk.

Inashangaza kuona CHADEMA wapo kimya,wanashindwa kumsukuma rais Magufuli na utawala wake pale anapoonekana ameshindwa kufika,inaonekana kama chama kimekosa sauti za kuaminika zakupigia kelele maswala ya ufisadi tangu walipomleta mtuhumiwa mkuu ndani ya nyumba.
 
tetetete...acha utani cdm wazungumzie richmond....je wakiambiwa shut up and keep quiet?
 
Kwani ukumwelewa mbowe aliposema majibu makuu mzee Wa msoga mzee Wa lushoto na kuu la makatibu kuwa ndio majibu makuu chadema IPO kwenye misingi Yake Ile Ile
 
Imefika wakati sasa CHADEMA irudi kwenye misingi iliyokuwa ikiisimamia hapo awali kabla Mwenyekiti hajabadili gia angani, ambayo ni mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa na kujitenga na wanasiasa ambao wana makando makando.

Kwasasa hivi Dr Magufuli anafanya kazi kubwa ya kupambana na genge la lakini bado haitoshi, CHADEMA inapaswa kwenda mbele ya hapo kwa kumwambia Mh rais kwa mfano mbona flani na flani huwagusi?Tunataka pia uwashughulikie wale waliohusika katika kashfa za Richmond, EPA,Meremeta ESCROW, mabilioni ya Kikwete,Radar,mabilioni ya Uswisi,nk.

Inashangaza kuona CHADEMA wapo kimya,wanashindwa kumsukuma rais Magufuli na utawala wake pale anapoonekana ameshindwa kufika,inaonekana kama chama kimekosa sauti za kuaminika zakupigia kelele maswala ya ufisadi tangu walipomleta mtuhumiwa mkuu ndani ya nyumba.

Mkuu TEKNOLOJIA,

Heri ya Mwaka Mpya. Ni kweli Utawala mpya bado haujafanya lolote tangible kufumua mfumo zaidi ya talk show na maigizo tu

Hakuna Vision ,Ideological direction Economically na hakuna a serious plan for social-political transformation.

Taifa limefika "State of comfussion" kama ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2011 enzi za Babu wa Loliondo.

Mbinu zilezile zinafanywa kupitia njia zilezile dhidi ya watu wa taifa lilelile ila tofauti ni kuwa 2011 ilifanywa spiritually lakini hii ni politically.
 
Definately, Upinzani lazima iingie kwenye "state of confussion" maana huu mchakamchaka wa Magufuli umemaliza kabisa upinzani
 
CHADEMA imuulize rais kwa nini hajawagusa mafisadi fulani? Are you joking? Yeye rais hajui watu wa kuwashughulikia? Kama lengo ni Lowasa, hajui kuwa anatakiwa kumfikisha mahakamani hadi akumbushwe? Tuseme hana ubavu wa kuwachukulia hatua akina Joka lenye makengeza na marais wastaafu hadi CHADEMA waseme? Halafu aishie kudai kuwa ni "CHADEMA ndio wenye ushahidi kuwa eti nyinyi ni mafisadi"?
 
Mkuu TEKNOLOJIA,

Heri ya Mwaka Mpya. Ni kweli Utawala mpya bado haujafanya lolote tangible kufumua mfumo zaidi ya talk show na maigizo tu

Hakuna Vision ,Ideological direction Economically na hakuna a serious plan for social-political transformation.

Taifa limefika "State of comfussion" kama ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2011 enzi za Babu wa Loliondo.

Mbinu zilezile zinafanywa kupitia njia zilezile dhidi ya watu wa taifa lilelile ila tofauti ni kuwa 2011 ilifanywa spiritually lakini hii ni politically.

Mkuu Ben habari za siku, naona kama umekwepa hoja ya msingi ya mleta mada lakini anyway hivyo ndio inavyopaswa kukitetea chama. Naomba nikuambie ukweli mchungu, mimi ni shabiki wa cdm wakutupwa ila ndugu yangu kwa kumleta EL kwenye chama hapo tulicheza karatu mbovu kupindukia. Kwa jinsi chama chetu kilivyokuwa na mvuto na nguvu ya kuikemea serekali na yenyewe ikanywea kabla ya kuja EL ni tofauti kabisa na sasa. Ki ukweli hata EL asingekuja cdm bado tungepata kura nyingi hata kama tungekosa urais lakini tungekuwa na wabunge wengi kuliko ilivyo sasa.

Siamini chama chetu ndio kimegeuka eti kuwa kimya kuhusu ufisadi simply kwa kumleta mtu mmoja tu ambaye sisi kama chama tulimtolea lugha zote mbaya. Wengi wa wabunge wetu leo hii zile kauli zao kuhusu huyo EL hata zikiwekwa hapa jukwaani na huko kwenye mitaa wanafunga midomo na kubaki na blabla tu. Asikutanie mtu kisa cha ccm kumchagua Magufuli ni kutokana na hofu ya cdm kwani walijua tu iwapo watamsimamisha EL au Membe basi cdm kwa haki ingetinga ikulu. Ajabu iliyoje sisi ndio tukamchukua EL, siku ile ndio tulizima nyota ya chama na nguvu yake halisi ukiachia mbali ushabiki na idadi ya watu waliokuwa wanakuja kwenye mikutano yetu. Kwa taarifa yako cdm haikuwa na shida ya nyomi, bila hata EL cdm ilikuwa ina nyomi tena inayojiamini na kuikemea serekali. Haya tumemchukua huyo EL hata jukwaani kwenyewe hakuwa na sera zaidi ya kuongea kiccm kumwaga ahadi tena akicheza na jukwaa chini ya kiwango, ghafla makamanda tukawa wapole kwa kuingiza garasa uwanjani. Kwa kweli kitendo hiki kama chama tumekosea na ni jambo litakalotugharimu kupita kiasi.

Kuonyesha chama kimepoteza muelekea kwa sasa, mpaka tunavyoongea hatuna katibu mkuu wa chama kama katiba inavyotaka. Hili ni kosa jingine la wazi, huyo EL hafahamiki ni nani chamani lakini imekuwa kama vile ni virtual leader. Ukweli mchungu kuendelea kuwa na EL chamani ni kuharibu haiba ya chama taka msitake, kwa hili mwenyekiti anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi ili mtu mwingine aingie na aijenge haiba ya chama, vinginevyo tutaula wa chuya.

cc: mtazamo, John Mnyika
 
Sasa CHAGA-DEMA
imesha uzwa na mnunuzi Ndio KIRANJAA WA MAJIZI AFRIKA
hakuna tena namna
 
Mkuu TEKNOLOJIA,

Heri ya Mwaka Mpya. Ni kweli Utawala mpya bado haujafanya lolote tangible kufumua mfumo zaidi ya talk show na maigizo tu

Hakuna Vision ,Ideological direction Economically na hakuna a serious plan for social-political transformation.

Taifa limefika "State of comfussion" kama ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2011 enzi za Babu wa Loliondo.

Mbinu zilezile zinafanywa kupitia njia zilezile dhidi ya watu wa taifa lilelile ila tofauti ni kuwa 2011 ilifanywa spiritually lakini hii ni politically.
Habari hapo ni CHAGA-DEMA
mjipime Akili
wapi mlipo na mmetoka wapi
Wacha porojo
 
Mkuu Ben habari za siku, naona kama umekwepa hoja ya msingi ya mleta mada lakini anyway hivyo ndio inavyopaswa kukitetea chama. Naomba nikuambie ukweli mchungu, mimi ni shabiki wa cdm wakutupwa ila ndugu yangu kwa kumleta EL kwenye chama hapo tulicheza karatu mbovu kupindukia. Kwa jinsi chama chetu kilivyokuwa na mvuto na nguvu ya kuikemea serekali na yenyewe ikanywea kabla ya kuja EL ni tofauti kabisa na sasa. Ki ukweli hata EL asingekuja cdm bado tungepata kura nyingi hata kama tungekosa urais lakini tungekuwa na wabunge wengi kuliko ilivyo sasa.

Siamini chama chetu ndio kimegeuka eti kuwa kimya kuhusu ufisadi simply kwa kumleta mtu mmoja tu ambaye sisi kama chama tulimtolea lugha zote mbaya. Wengi wa wabunge wetu leo hii zile kauli zao kuhusu huyo EL hata zikiwekwa hapa jukwaani na huko kwenye mitaa wanafunga midomo na kubaki na blabla tu. Asikutanie mtu kisa cha ccm kumchagua Magufuli ni kutokana na hofu ya cdm kwani walijua tu iwapo watamsimamisha EL au Membe basi cdm kwa haki ingetinga ikulu. Ajabu iliyoje sisi ndio tukamchukua EL, siku ile ndio tulizima nyota ya chama na nguvu yake halisi ukiachia mbali ushabiki na idadi ya watu waliokuwa wanakuja kwenye mikutano yetu. Kwa taarifa yako cdm haikuwa na shida ya nyomi, bila hata EL cdm ilikuwa ina nyomi tena inayojiamini na kuikemea serekali. Haya tumemchukua huyo EL hata jukwaani kwenyewe hakuwa na sera zaidi ya kuongea kiccm kumwaga ahadi tena akicheza na jukwaa chini ya kiwango, ghafla makamanda tukawa wapole kwa kuingiza garasa uwanjani. Kwa kweli kitendo hiki kama chama tumekosea na ni jambo litakalotugharimu kupita kiasi.

Kuonyesha chama kimepoteza muelekea kwa sasa, mpaka tunavyoongea hatuna katibu mkuu wa chama kama katiba inavyotaka. Hili ni kosa jingine la wazi, huyo EL hafahamiki ni nani chamani lakini imekuwa kama vile ni virtual leader. Ukweli mchungu kuendelea kuwa na EL chamani ni kuharibu haiba ya chama taka msitake, kwa hili mwenyekiti anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi ili mtu mwingine aingie na aijenge haiba ya chama, vinginevyo tutaula wa chuya.

cc: mtazamo, John Mnyika
Habari hapo ni CHAGA-DEMA
mjipime Akili
wapi mlipo na mmetoka wapi
Wacha porojo
 
Imefika wakati sasa CHADEMA irudi kwenye misingi iliyokuwa ikiisimamia hapo awali kabla Mwenyekiti hajabadili gia angani, ambayo ni mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa na kujitenga na wanasiasa ambao wana makando makando.

Kwasasa hivi Dr Magufuli anafanya kazi kubwa ya kupambana na genge la manyang'au lakini bado haitoshi, CHADEMA inapaswa kwenda mbele ya hapo kwa kumwambia Mh rais kwa mfano 'mbona flani na flani huwagusi?Tunataka pia uwashughulikie wale waliohusika katika kashfa za Richmond, EPA,Meremeta ESCROW, mabilioni ya Kikwete,Radar,mabilioni ya Uswisi,nk.

Inashangaza kuona CHADEMA wapo kimya,wanashindwa kumsukuma rais Magufuli na utawala wake pale anapoonekana ameshindwa kufika,inaonekana kama chama kimekosa sauti za kuaminika zakupigia kelele maswala ya ufisadi tangu walipomleta mtuhumiwa mkuu ndani ya nyumba.
Chadema hawana ubavu huo
 
Mkuu TEKNOLOJIA,

Heri ya Mwaka Mpya. Ni kweli Utawala mpya bado haujafanya lolote tangible kufumua mfumo zaidi ya talk show na maigizo tu
JINIAS WA UKAWA Akisema wengine inabidi muitikie,Hakuna HAJA YA Kwenda shule wakati MaPHD Holders wanakuchukulia wewe kama Role model.Hoja YETU sasa na AGENDA ni MFUMO na kila mtu auiimbe

Hakuna Vision ,Ideological direction Economically na hakuna a serious plan for social-political transformation.
Msomi wa INDIA??????????????????????
Taifa limefika "State of comfussion" kama ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2011 enzi za Babu wa Loliondo.
AISEEEEEEEEEEEEEEEEE
Mbinu zilezile zinafanywa kupitia njia zilezile dhidi ya watu wa taifa lilelile ila tofauti ni kuwa 2011 ilifanywa spiritually lakini hii ni politically.
CCM CHAMA KIBOVUUUUUUU na kilichoshindwa pamoja na UBOVU NA UDHAIFU WAKE Kikaona baadhi ya MAKADA WAKE Pamoja na ubovu wao HAWAFAI.MAKADA HAO ni miungu watu Ndani ya UPINZANI.Magufuli ana siku 100 IKULU Agenda ya UPINZANI NI mfumo.mAAJABUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Mkuu TEKNOLOJIA,

Heri ya Mwaka Mpya. Ni kweli Utawala mpya bado haujafanya lolote tangible kufumua mfumo zaidi ya talk show na maigizo tu

Hakuna Vision ,Ideological direction Economically na hakuna a serious plan for social-political transformation.

Taifa limefika "State of comfussion" kama ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2011 enzi za Babu wa Loliondo.

Mbinu zilezile zinafanywa kupitia njia zilezile dhidi ya watu wa taifa lilelile ila tofauti ni kuwa 2011 ilifanywa spiritually lakini hii ni politically.
 
Mkuu TEKNOLOJIA,

Heri ya Mwaka Mpya. Ni kweli Utawala mpya bado haujafanya lolote tangible kufumua mfumo zaidi ya talk show na maigizo tu

Hakuna Vision ,Ideological direction Economically na hakuna a serious plan for social-political transformation.

Taifa limefika "State of comfussion" kama ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2011 enzi za Babu wa Loliondo.

Mbinu zilezile zinafanywa kupitia njia zilezile dhidi ya watu wa taifa lilelile ila tofauti ni kuwa 2011 ilifanywa spiritually lakini hii ni politically.
Kuna siku ulijitambulisha kwenye mdahalo wa MNF mwaka jana kama afisa sera wa chadema,baadae nikakamsikia Prof.Baregu akitamba kwamba mliamua kumchukuwa EL sababu ni jambazi aliyetoroka ugomvi CCM kwahiyo mmemchukuwa ili awasaidie kuingia ikulu,mwezi mmoja baadae ukaandika kituko kutetea utafiti wa Tadip dhidi ya Twaweza na Synovate na Prof.Baregu akadanganya umma kwamba kuna rafiki yake yupo Oxford kamwambia Chadema ingeshinda kwa asilimia 51...baadaye nikaona makala yako Raia Tanzania ukisema kwamba ni mwanafunzi wa uzamivu (Phd) bahati nzuri Prof.Baregu ni mwalimu wangu wa DS udsm,2001.Jifunze yafuatayo;
1.Usijatambulishe tena kama mwanafunzi wa Phd,...labda kama unasoma phd za kina makongoro...Phd ni utafiti!
2.Ni sera gani unasimamia chadema?..manake chama hakina sera...hata Guninita hujamfikia kisera pamoja na umbumbumbu wake.
3.Siasa zako za kutengeneza migomo,maandamano fake,kama ulivyofanya rombo kumtisha DC kutetea wanywa gongo kupindukia zinajenga "negative legacy" dhidi yako.
3.Ulijaribu sana kujilinganisha na ZZK na hata kupiga ramli mtandaoni lakini humfikii hata asilimia 1.
4.jifunze kuweka akiba ya maneno.
5.Prof.Baregu nitaongea naye nikikutana naye japo maandiko yake mengi ya tafiti nayahofia...!

Grow up!
 
Mkuu Ben habari za siku, naona kama umekwepa hoja ya msingi ya mleta mada lakini anyway hivyo ndio inavyopaswa kukitetea chama. Naomba nikuambie ukweli mchungu, mimi ni shabiki wa cdm wakutupwa ila ndugu yangu kwa kumleta EL kwenye chama hapo tulicheza karatu mbovu kupindukia. Kwa jinsi chama chetu kilivyokuwa na mvuto na nguvu ya kuikemea serekali na yenyewe ikanywea kabla ya kuja EL ni tofauti kabisa na sasa. Ki ukweli hata EL asingekuja cdm bado tungepata kura nyingi hata kama tungekosa urais lakini tungekuwa na wabunge wengi kuliko ilivyo sasa.

Siamini chama chetu ndio kimegeuka eti kuwa kimya kuhusu ufisadi simply kwa kumleta mtu mmoja tu ambaye sisi kama chama tulimtolea lugha zote mbaya. Wengi wa wabunge wetu leo hii zile kauli zao kuhusu huyo EL hata zikiwekwa hapa jukwaani na huko kwenye mitaa wanafunga midomo na kubaki na blabla tu. Asikutanie mtu kisa cha ccm kumchagua Magufuli ni kutokana na hofu ya cdm kwani walijua tu iwapo watamsimamisha EL au Membe basi cdm kwa haki ingetinga ikulu. Ajabu iliyoje sisi ndio tukamchukua EL, siku ile ndio tulizima nyota ya chama na nguvu yake halisi ukiachia mbali ushabiki na idadi ya watu waliokuwa wanakuja kwenye mikutano yetu. Kwa taarifa yako cdm haikuwa na shida ya nyomi, bila hata EL cdm ilikuwa ina nyomi tena inayojiamini na kuikemea serekali. Haya tumemchukua huyo EL hata jukwaani kwenyewe hakuwa na sera zaidi ya kuongea kiccm kumwaga ahadi tena akicheza na jukwaa chini ya kiwango, ghafla makamanda tukawa wapole kwa kuingiza garasa uwanjani. Kwa kweli kitendo hiki kama chama tumekosea na ni jambo litakalotugharimu kupita kiasi.

Kuonyesha chama kimepoteza muelekea kwa sasa, mpaka tunavyoongea hatuna katibu mkuu wa chama kama katiba inavyotaka. Hili ni kosa jingine la wazi, huyo EL hafahamiki ni nani chamani lakini imekuwa kama vile ni virtual leader. Ukweli mchungu kuendelea kuwa na EL chamani ni kuharibu haiba ya chama taka msitake, kwa hili mwenyekiti anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi ili mtu mwingine aingie na aijenge haiba ya chama, vinginevyo tutaula wa chuya.

cc: mtazamo, John Mnyika
Katiba ya CHADEMA inasema Katibu Mkuu hupatikana baada ya Baraza kuu kukaaa.Hateuliwi kama vile anavyoteuliwa Mwenyekiti au katibu wa kamati za Harusi au inavyofanyika kwenye vyama vidogovidogo visivyofuata katiba
 
Kuna siku ulijitambulisha kwenye mdahalo wa MNF mwaka jana kama afisa sera wa chadema,baadae nikakamsikia Prof.Baregu akitamba kwamba mliamua kumchukuwa EL sababu ni jambazi aliyetoroka ugomvi CCM kwahiyo mmemchukuwa ili awasaidie kuingia ikulu,mwezi mmoja baadae ukaandika kituko kutetea utafiti wa Tadip dhidi ya Twaweza na Synovate na Prof.Baregu akadanganya umma kwamba kuna rafiki yake yupo Oxford kamwambia Chadema ingeshinda kwa asilimia 51...baadaye nikaona makala yako Raia Tanzania ukisema kwamba ni mwanafunzi wa uzamivu (Phd) bahati nzuri Prof.Baregu ni mwalimu wangu wa DS udsm,2001.Jifunze yafuatayo;
1.Usijatambulishe tena kama mwanafunzi wa Phd,...labda kama unasoma phd za kina makongoro...Phd ni utafiti!
2.Ni sera gani unasimamia chadema?..manake chama hakina sera...hata Guninita hujamfikia kisera pamoja na umbumbumbu wake.
3.Siasa zako za kutengeneza migomo,maandamano fake,kama ulivyofanya rombo kumtisha DC kutetea wanywa gongo kupindukia zinajenga "negative legacy" dhidi yako.
3.Ulijaribu sana kujilinganisha na ZZK na hata kupiga ramli mtandaoni lakini humfikii hata asilimia 1.
4.jifunze kuweka akiba ya maneno.
5.Prof.Baregu nitaongea naye nikikutana naye japo maandiko yake mengi ya tafiti nayahofia...!

Grow up!

Huwa inaandikwa Ph.D............

Kama Umeweza kunifuatilia koote huko then huoni unajiumbua mwenyewe? Kama nilitetea Utafiti wa TADIP dhidi ya utafiti wa TWAWEZA na Mwalimu wako Prof.Baregu akafanya hivyohivyo huoni kwamba utafiti unapaswa kupingwa/Kutetewa kwa utafiti mwingine tofauti na wewe unayeandika kwa mihemko bila kuwa na facts za kitafiti kama unavyofanya hapa?

Maana ungetafiti kwa undani ungejua ilani ya CHADEMA iliyoungwa mkono na vyama washirika wa UKAWA iliandikwa juu ya misingi ya kisera.

Hata sera mpya ya Elimu ya serikali ni zao la Zaidi ya asilimia 80 ya sera yetu ya Elimu tuliyozindua mwaka 2014 Mwezi septemba

Jifunze kuandika vitu ambavyo una uhakika navyo.Kwa mfano unasema niliandika makala Raia Tanzania.Ukweli ni kuwa sijawahi kuandika makala yoyote Raia Tanzania. Punguza hasira ili uongeze umakini zaidi
 
Back
Top Bottom