Joseph Ludovick
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 382
- 506
Amos Makala akipokea wanachama waliotoka CHADEMA na kujiunga CCM Mbeya leo tar 27/03/2025
CPA Amos Makalla Katibu wa NEC Siasa, itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM amegeuka mwiba kwa CHADEMA.Ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliyejipambanua kwa uongozi thabiti na mikakati bunifu inayokijenga chama na kuhakikisha kinaendelea kuwa na mvuto kwa wananchi.
Makalla ameshika nafasi mbalimbali za uongozi. Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, alihudumu kama Mkuu wa Mikoa kadhaa ambapo alionyesha uwezo mkubwa wa kiutawala na kusimamia maendeleo ya mikoa hiyo nafasi zilizomjengea umahiri na uelewa wa kina kuhusu mahitaji ya wananchi na namna ya kuyashughulikia kupitia sera za chama. Amewahi pia kuwa katibu wa Uchumi na fedha.
Wana CHADEMA mkoani Mbeya waliofika leo kumueleza Amosi Makala kusikitishwa kwao na namna ambavyo mwenyekiti wao Tundu Lissu alivyowahadaa wakatumia gharama zao kusomba watu kuwaleta kwenye mkutano lakini akaondoka bila kuwarudishia fedha zao.
Akiwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Makalla ameweka mikakati madhubuti inayolenga kuimarisha chama na kuhakikisha kinaendelea kuwa na ushawishi katika siasa za Tanzania katika maeneo ya Kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM, Kuhimiza siasa za kistaarabu na kuheshimiana kuendana na mtazamo wa mwenyekiti wa Chama wa 4R, na Kujibu hoja za upinzani kwa weledi.
Uwezo huu wa Makalla umeifanya CHADEMA kuwa na wakati mgumu katika uwanja wa siasa. Mikakati yake imewafanya viongozi wa CHADEMA kushindwa kupambana naye. Makalla amebainisha kuwa CHADEMA inakabiliwa na migogoro ya ndani na ukosefu wa maandalizi, hali inayowafanya washindwe kushindana na CCM yenye uongozi imara na mikakati thabiti. Ni hivi majuzi tu, genge la wahuni limempora mwenyekiti Mbowe chama kwa njia haramu.
Makalla amewakosoa viongozi wa CHADEMA kwa kushindwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, jambo linalowaondolea sifa ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi na hivyo kuwafanya washindwe kwa haki kila uchaguzi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa kuwa Makalla anajibu hoja za upinzani kwa ushahidi na weledi, CHADEMA imejikuta ikikosa hoja zenye nguvu za kupambana na CCM, hali inayoongeza hofu na kushindwa kwao katika uwanja wa siasa. Hivi majuzi akiwaonyesha kuwa hawawezi kuzuia Uchaguzi labda kama watatumia njia za Kigaidi. Kauli ambayo waliitafsiri vibaya na sasa wanalia kila mahali wakitaka msaada.
Kwa namna mambo yanavyokwenda na kwa aina ya uongozi dhaifu uliopo CHADEMA, ni wazi CCM itapata ushindi wa Kimbunga huku CHADEMA wakiendelea kukunja ngumi.