Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,267
- Thread starter
- #61
Hapo kwenye vijiji, kuna taratibu za kisheria kupata hati miliki ya ardhi ya kijiji na inabidi ninyi wasomi muongioze jahazi kwa kutoa muongozo, kwa sheria ya sasa kama pori la ardhi halijatumika linaweza kutwaliwa wakati wowote kuwa ardhi ya jumla ama badu bado hata kama mwekezaji amepewa eneo na watu kuhamishwa kwa nguvu pia kuna taratbu zake na kisheria,
Endelea kuchunguza kuhusu hayo malori wacha ku-operate kwa hear say
Endelea kuchunguza kuhusu hayo malori wacha ku-operate kwa hear say
Mkuu haya malori tunayaona huku Kilombero kila siku na hatujui ni ya nani ingawa kuna watu wansema chinichini kwamba ni mali ya "Prince".
Ni kweli kabisa mwekezaji amepewa kipaumbele kuliko sisi wananchi. Kuna wananchi wanavunjiwa nyumba zao na kufukuzwa kwenye maeneo yao ili kumpisha huyu mwekezaji. Wananchi wameishi maeneo hayo ambayo walipewa na serikali wakati wa kuunda vijiji vya ujamaa, hivyo familia zimezaana hapo na kuzikana (makaburi) hapo. Leo hii watu wanafukuzwa kama wanyama. kwa mfano kuna vijiji vya Msolwa stesheni na katurukila vilivyo kando kando ya reli ya Uhuru. Wananchi waliletwa hapo kwa ajili ya kuanziasha vijiji vya ujamaa na pia kulinda reli ya uhuru. Sasa leo serikali hiyo hiyo inawafukuza katika maeneo hayo na kumpa mwekezaji, jamani haki iko wapi?
Kilombero - Chadema Forever