Niko hapa Kilombero kwa muda kwani ni msimu wa kilimo;
Nimefanya kaudadisi kadogo baada ya kuona kwa asilimia kubwa toka Mikumi hadi Chita (huko mbele sikuendelea) kuna bendera nyingi pembezoni mwa Barabara ambazo ni za CHADEMA na kugundua kwamba hiki chama kinakubalika sana huku (mm sio mfuasi wake) na kwamba zaidi ya yote idadi kubwa ya madiwani wanatoka chama hiki, hapa Chita nilizungumza na wadau kadhaa wakaniambia moja ya sababu za kuchagua CHADEMA ni kwamba wanakasirika sana umeme unatoka jirani na kwao (Kihasi) halafu unakwenda viunga vingine vya mbali ilihali wao wanawasha vibatari.......sababu nyingine ni kwamba wanaisi wamewekwa pembezoni na rasilimali muhimu za nchi na hasa ubovu wa barabara ambao hata hakuna dalili ya kutengewa fungu japokuwa wao ni wazalishaji wakubwa wa mchele
Watu wa Mngeta na Mbingu wanahasira ya umeme kwenda kwa mwekezaji wa Kilombero Plantation Limited (KPL) ilihali wao wakiambulia jenereta la mhisani mwanakijiji mwenzao
Nimewauliza vipi kuhusu sakata la Zitto linawagusaje na mustakabali wao chamani wakanijibu Zitto atapita na mambo yake lakn CHADEMA itaendelea kuwepo hIvyo wanakaza buti na Chama chao hicho.
Yeyote aliyebahatika/atakayebahatika kutembelea maeneo haya anaweza kuthibitisha haya
Besides; Simba inakubalika sana huku sababu wanachukia rangi ya kijani na njano na ninafanya mpango wa kufungua TAWI
cc: Makoye Matale, Ulimakafu, Mandieta ..................
...
....Mkuu namalizia kukamilsha ripoti ya huko...nakubalina na wewe 100% Chadema inakubalika huko kwa sana tuuu
ila Kilombero Plantation LTD wanazalisha umeme wao na wanagawa katika vijiji jirani kwa bei ndogo...
ila kwa hii Grid ya Taifa kupita juu kwa juu imenisikitisha sana...
...Mkuu ulisika ile meli iliyomwaga mchele toka ng'ambo na kuvunja soko la mchele Tanzania ?
Hata mimi nimefanya udadisi nimegundua Chadema ni chama cha kikanda.Udadisi ni sehemu ya kupata data kwenye scientific research rejea methods of data colllection in scientific research........usikosoe kitu usichokijua gamba we.....!
Hata mimi nimefanya udadisi nimegundua Chadema ni chama cha kikanda.
Mkuu Ritz, nimekuwa makini sana kutumia neno Udadisi na si UTAFITI kwani naelewa complications, implications na repucations zake
hili nililifanyia kazi mkuu, ambao wanaweza ku afoord still ni wachche sana, jirani kabisa na mchombe kuna Guest ndipo ina huo umeme, nitauliza ziadi kwa sababu umepita barabarani tu nadhani huwezi kuupata kirahisi, hili la mchele kwa kwakweli wananchi wanalia sana huku, sasa hivi ni msimu lakn wamekosa hela ya kulimia kwa sababu waliuza kwa hasara, wakati nakuja walau niliona malori yanaanza kusogea huku kwani mengi sana yanaishia Ifakara mjini lakn wengi walikata tamaa wameshauza mchele wao kwa hasara, tena nasikia aliyeingiza huo mchele ni mtoto wa kigogo hivyo kuua soko la ndani na mchele wenyewe ulitoka Thailand
[/COLOR][/B]
Umemmaliza ritzone sijui kama atarudiSasa mbona ulikuwa una disqualify ujumbe wa mleta post kuwa hajafanya utafiti bali udadisi....? Kwa hiyo kilombero ni kanda gani we gamba?
....ha ha ha ha Mkuu salute wewe!! Ulilala pale kwa Ngosha!!!
Soko la Mchele Tanzania:
Mkuu hata hao Kilombero Plantation wanalia sana baada ya Mchele wa Thailand kumwagwa bandarini!! Mkuu nilifika maeneo ya Mofu, ijiya mpaka kwa gavana ndulu hali ni mbaya sana!!! Wakulima wa mpunga hata kurudi shambani msimu huu ni hati hati!!! ....Mkuu hii nchi ilishaozaa kabisa .....
Mkuu ntarusha hewani siku zijazo hii kitu...leo nipo kwenye heka heka za kampeni hapa Arusha...
...Mkuu again salute wewe!!!
Uwingi wa kamasi hauendani na ukubwa wa pua.na kama ni kweli naomba unikumbushe mbunge wao ni wa chama gani?kumbuka kura ni siri,unaweza ona mikutano imejaa ukajua wote ni wamoja kumbe ni maafara wa mamba
Mkuu Amavubi hana lolote huyo gamba udadisi ni moja ya njia ya kisayansi ya kupata data tofauti wewe kuwa huku document mahali vinginevyo hata kuona tu bendera za chadema njiani ungeweza kuanza kupata picha halisi hiyo ni observation method......ktk tathmini ya hali ya chakula wataalamu upita mashambani wakiangalia ustawi wa mazao na kutoa tathmini ya upatikanaji wa hali ya chakula kwa msimu husika bila kujali mazao hayo yataliwa na wadudu au la........hawa vijana wa lumumba ttz lao ni matumbo yao tu
Dah, umenitisha sana, kwa Ngosha pale ndio walau unaweza kupata Jamii Forum kwani pana umeme wa Gridi ya Taifa