CHADEMA inaimarika na inasonga mbele

CHADEMA inaimarika na inasonga mbele

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Uchaguzi wa Ubunge wa Kalenga umekwisha na mshindi ameshapatikana. Ni Godfrey Mgimwa wa CCM. Waswahili walisema: yaliyopita si ndwele,tugange yajayo. Ndivyo inavyotakiwa kwa vyama vyote vilivyoshiriki ucaguzi wa Kalenga.Ni kwakuwa,wananchi wa Kalenga wamechagua waliyemchagua kwa matakwa yao na sababu zao. Kama alivyosema Mbunge Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa CHADEMA inayaheshimu maamuzi ya watu wa Kalenga. Lema alinena vyema sana na kidemokrasia.

Kufuatia ushindi wa Kalenga, wanachama na wapenzi wa CCM wamekuwa wakiibeza na kuikejeli sana CHADEMA. Wanafanya hivi katika upofu wa kidemokrasia.Hawajui ya kuwa uamuzi wa wananchi hautabiriki.Wananchi wanaweza kuamua chochote na muda wowote. Hizi mechi kali kati ya CCM na CHADEMA hazijaishia Kalenga.Mtanange bado unaendelea.

Wapo wanathubutu hata kusema kuwa sasa ni wakati wa uongozi wa CHADEMA kuachia ngazi. Eti kwakuwa CHADEMA imeshindwa Kalenga na katika kata 23 za Udiwani. Siamini kuwa Chaguzi Ndogo ni kipimo cha mwisho cha kufanikiwa au kushindwa kwa chama. Ni matayarisho tu ya mwaka 2015. Ingekuwa kwenye uchaguzi mkuu,hoja hii angalau ingekuwa na mshiko. Kwasasa,mambo bado haya jamani.

Kwanza, uongozi wa chama si kama kocha wa timu ya kandanda. Uongozi hutegemea watu na mawazo yao ya kujenga. Uongozi wa CHADEMA hadi hivi sasa unafanya kazi ya kutukuka na kupigiwa mfano. Umeweza kuwafanya CCM walale na mawazo kila uchao na katika kila uchaguzi wa sasa. Mapambano bado yanaendelea tena kwa kasi kubwa.

Kuna hoja ya kwamba kushindwa kwa CHADEMA Kalenga kumesababishwa na Zitto Z. Kabwe. Iko wazi kuwa Zitto hausiki na wala hakuna muda tena wa kumzungumzia ndani ya chama kwakuwa taratibu za kisheria na za kichama zinaendelea na hakuna haja ya 'majungu' katika hili. Zitto ni Zitto na CHADEMA ni CHADEMA.

CHADEMA itabezwa na kukejeliwa vya kutosha.Lakini,inazidi kuimarika na inasonga mbele. Subirini Jaji Damian Lubuva arekebishe Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wananchi wajiandikishe na kujihakiki kwa wingi, wananchi wawe na uchungu na shahada zao za kupigia kura na kutokubali kurubuniwa. Hapo ndipo demokrasia ya nchi hii itakapoonja ladha mpya. Na siku husika wala haipo mbali sana.

Itoshe kusema kuwa,CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, inaimarika na kusonga mbele. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke. Demokrasia haina sifa ya hichohicho kuwa pale pale.
 
Jidanganyeni tu na kujipa moyo hivyohivyo kweli mbadala wa ccm haujazaliwa nchi. Hii
 
sasa mboni kabla ya uchaguzi mlijiaminisha mtashinda?....mwanakijiji aliwashauri kama mnaamini sheria mbovu, police na tume watawabeba ccm msishiriki!! mboni mlishiriki uchaguzi?
 
Kaka yangu kushindwa au kushinda ni namna aliyeshindwa na aliyeshinda anachukulia.Ningekuwa uongozi wa CCM ningeanza kuangali namba za waliokipigia kura CCM mwaka 2010 na waliokipigia jana,na kutokea hapo ndipo nijue je,niendelee kukibeza Chadema?

Pili ningeongeza kwenye point zako siyo tu suala la daftari la kudumu lawapiga KURA ila HAKI KAMILI na DEMOKRASIA isiyokuwa na mabavu kuwe na kweli HAKI na DEMOKRASIA ya dhati kwenye suala la vyama vya siasa,wananchi wawe huru na kweli huru wa kusikia,kupokea taarifa za chama chochote cha siasa,na hata kukipigia kura chama chochote cha siasa bila vurugu,chuki na ugomvi wa polisi na raia wala vitisho vya ukipigia chama cha upinzani huwezi kupata maendeleo na mengineyo mengi.

Tatu viongozi wetu wakubalu ukweli mchungu kwamba mtanzania wa jana si wa leo.

Na mwsiho vyama vya upinzani vijifunze sasa,bila kupeleka kesi mahakamani ya haki sawa nyakati za uchaguzi na kufanyika kwa uandikishaji wa wapiga kura kila mara if not kila siku basi waandike maumivu,na hii si kwa CDM bali kwa vyama vyote ACT-Tanzania,CUF,NCCR nk.Leo ACT-Tanzania ikiwa na nguvu basi itegemee yatokeayo kwa CDM yatatokea kwao pia.Tuikumbuke historia ya CUF maneno yaliyosemwa juu yake na mwisho wa siku CUF imekufa na maneno yameisha je tujiulize kwa nini kama watanzania hatukuzitupilia mbali kauli dhidi ya CUF?Tuliamini yaliyosemwa bila kujua kwa nini waliazimia kutoa propoganda za chuki juu ya CUF,leo CDM ipo huko ilikokuwa CUF lakini vyama vingine vya upinzani vinakubali tena propaganda zile zile kutoka chama kile kile na watu wale wale je hatuoni kuwa hatujitendei haki?

Viongozi wa upinzani amkeni sasa muda unaisha.
 
Ni kweli tulikuwa na matumaini makubwa !. Ila nadhani tuli-underestimate athari za daftari la kudumu la wapiga kura kutokuboreshwa.....Hebu fikiri kati ya walioandikishwa miaka minne iliyopita ambao ni 71 alfu ni 29 alfu tu ndio waliopiga kura.

Kuna wengine wengi tu ingawa walikuwa wanaiunga mkono CDM hapo, walibaki kuwa watazamaji wakati wa kupiga kura !. Hii si sawa kabisa !

sasa mboni kabla ya uchaguzi mlijiaminisha mtashinda?....mwanakijiji aliwashauri kama mnaamini sheria mbovu, police na tume watawabeba ccm msishiriki!! mboni mlishiriki uchaguzi?
 
Hivi mnavyosema kuwa tusubiri daftari la wapiga kura lirekebishwe mna maana gani? ??? Kwa akili zenu fupi mnadhani watakao andikishwa ni wapiga kura wa chadema peke yake. Fungueni akili acheni kuwa misukule watu wengine wafikirie kwa niaba yenu.
 
Hapana watajiandikisha na wa CCM, ila CDM tunajua watu wengi ambao ni wapenzi wetu ndio hawajaandikishwa ! Anyway cha muhimu waandikishwe na hapo ndio ukweli na uhalisia wa matokeo ya uchaguzi utaonekana !

Kwani watajiandikisha chadema peke yao?
 
Jidanganyeni tu na kujipa moyo hivyohivyo kweli mbadala wa ccm haujazaliwa nchi. Hii

MAJIBU SAHIHI
--------------------
Jibu ni kuboreshwa kwa Daftali la wapiga kura tuu.

Karenga ni mabibi ndio yamepiga kura kalenga sasa unafikili maCCM yangefeli kweli....

Makamanda piganieni maboresho ya daftali sasa chaguzi hizi, kwa mjini kama chalinze tutashinda tu ata kwa daftali hili.

Hongera chadema kwakushinda (ingawa hakutangazwa), kama TISS wote walikuwa pale, police nao, kauli ya mkuu wa kaaya lazima kushinda, vitisho vywa green guard na CCM mkoa, na nguvu kubwa ya kutisha vijana na watu makini kutopiga kura.... Nasema tena hongereni sanaa, SASA TUELEKE CHALINZE HAKUNA KUKATA TAMAAAAAAA...

Mungu bariki Tanzania
Mungu bariki Tendega for 2015
 
Uchaguzi wa Ubunge wa Kalenga umekwisha na mshindi ameshapatikana. Ni Godfrey Mgimwa wa CCM. Waswahili walisema: yaliyopita si ndwele,tugange yajayo. Ndivyo inavyotakiwa kwa vyama vyote vilivyoshiriki ucaguzi wa Kalenga.Ni kwakuwa,wananchi wa Kalenga wamechagua waliyemchagua kwa matakwa yao na sababu zao. Kama alivyosema Mbunge Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa CHADEMA inayaheshimu maamuzi ya watu wa Kalenga. Lema alinena vyema sana na kidemokrasia.

Kufuatia ushindi wa Kalenga, wanachama na wapenzi wa CCM wamekuwa wakiibeza na kuikejeli sana CHADEMA. Wanafanya hivi katika upofu wa kidemokrasia.Hawajui ya kuwa uamuzi wa wananchi hautabiriki.Wananchi wanaweza kuamua chochote na muda wowote. Hizi mechi kali kati ya CCM na CHADEMA hazijaishia Kalenga.Mtanange bado unaendelea.

Wapo wanathubutu hata kusema kuwa sasa ni wakati wa uongozi wa CHADEMA kuachia ngazi. Eti kwakuwa CHADEMA imeshindwa Kalenga na katika kata 23 za Udiwani. Siamini kuwa Chaguzi Ndogo ni kipimo cha mwisho cha kufanikiwa au kushindwa kwa chama. Ni matayarisho tu ya mwaka 2015. Ingekuwa kwenye uchaguzi mkuu,hoja hii angalau ingekuwa na mshiko. Kwasasa,mambo bado haya jamani.

Kwanza, uongozi wa chama si kama kocha wa timu ya kandanda. Uongozi hutegemea watu na mawazo yao ya kujenga. Uongozi wa CHADEMA hadi hivi sasa unafanya kazi ya kutukuka na kupigiwa mfano. Umeweza kuwafanya CCM walale na mawazo kila uchao na katika kila uchaguzi wa sasa. Mapambano bado yanaendelea tena kwa kasi kubwa.

Kuna hoja ya kwamba kushindwa kwa CHADEMA Kalenga kumesababishwa na Zitto Z. Kabwe. Iko wazi kuwa Zitto hausiki na wala hakuna muda tena wa kumzungumzia ndani ya chama kwakuwa taratibu za kisheria na za kichama zinaendelea na hakuna haja ya 'majungu' katika hili. Zitto ni Zitto na CHADEMA ni CHADEMA.

CHADEMA itabezwa na kukejeliwa vya kutosha.Lakini,inazidi kuimarika na inasonga mbele. Subirini Jaji Damian Lubuva arekebishe Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wananchi wajiandikishe na kujihakiki kwa wingi, wananchi wawe na uchungu na shahada zao za kupigia kura na kutokubali kurubuniwa. Hapo ndipo demokrasia ya nchi hii itakapoonja ladha mpya. Na siku husika wala haipo mbali sana.

Itoshe kusema kuwa,CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, inaimarika na kusonga mbele. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke. Demokrasia haina sifa ya hichohicho kuwa pale pale.
on the way to chalinze mpaka tubaki 3
 
Kwani dalili ya chama kustawi ni nini.ustawi wa chama chochote ni kuungwa mkono na jamii inayoifanyia kazi,na kipimo rahisi ni kupigiwa kua nyigi sasa nyie kila kukicha mnazidi kutoungwa mkono halafu unajipa moyo.upende au ufiche uso zitto ni muhimu kwa chadema.heri uwatoe slaa na mbowe chama kitaendelea lakini zitto itachukua muda kustabilize.
 
Sasa kwa nini serikali ya CCM imehakikisha daftari haliboreshwi kwa miaka 4 ! Can you imagine, watu wanapiga kura na daftari la miaka minne iliyopita !

Ni ukweli ulio wazi watu wengi wanaokubali mabadiliko yanayoletwa na CDM ni vijana na ninaposema hivyo sina maana kwamba vijana wote ni CDM. CCM nao wana vijana wao na kinachotakiwa wao waboreshe daftari na hapo tutapata uchaguzi unaonyesha matakwa halisi ya wapiga kura kuliko kutumia uhalisia wa 2010 wakati sasa ni 2014.

Hivi mnavyosema kuwa tusubiri daftari la wapiga kura lirekebishwe mna maana gani? ??? Kwa akili zenu fupi mnadhani watakao andikishwa ni wapiga kura wa chadema peke yake. Fungueni akili acheni kuwa misukule watu wengine wafikirie kwa niaba yenu.
 
Wahenga walisema 'be willing to loose a battle in order to win the war' hizi chaguzi ndogo ni battles na kwa chama cha siasa kilichokomaa kinazi-treat kama pilot projects. The real war is only a year to come.

Ajidhaniaye amesimama na aangalie asianguke maana anguko lake huwa kuu! Nitarejea baada ya uchaguzi mkuu
 
Uko sahihi mh!ni kwa nini waijadili chamema kila mara wasijadili cuf au nccr mageuzi?hicho ndicho chama shindani ndani ya tanzania!itafahamika.songa mbele

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Wahenga walisema 'be willing to loose a battle in order to win the war' hizi chaguzi ndogo ni battles na kwa chama cha siasa kilichokomaa kinazi-treat kama pilot projects. The real war is only a year to come.

Ajidhaniaye amesimama na aangalie asianguke maana anguko lake huwa kuu! Nitarejea baada ya uchaguzi mkuu

Sahihi kabisa. Ngoma hunoga.....
 
zito ameondoka na chadema yake. chadema bila zito ni sawa na gari bila injini
 
Back
Top Bottom