Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
CHADEMA sasa haileweki ni chama cha siasa au 'nyumba ya ibada', kwani imekuwa ni kimbilio la 'wapigaji'. Mbowe alipotakiwa na kuhama NHC walizua mjadala mzito kuwa anaonewa, wengine wakisema anadhulumiwa nyumba ya urithi alioachiwa na Babake. Sumaye alipotaifishiwa mashamba kwa kushindwa kukidhi matakwa ya sharia walimiminika kumtetea na kulaani.
Ajizi nyumba ya njaa, Manji naye kaamriwa na Mahakama kuondoka kwenye nyumba ya PSPF kwa kushindwa kulipa kodi ya zaidi ya Bil.13 wanamiminika wakidai kuwa serikali inauwa wafanyabiashara....eti..'sasa kampuni tano zikiondoshwa hao waajiriwa waende wapi?', ghafla huruma imewajaa, wao hawaoni huruma mabilioni ya wastaafu yanaliwa, wazee wetu wanachelewa kupata malipo yao kwa ujanja ujanja. Ni dhahiri sasa hata Manji akiamua kujiunga na CHADEMA atafutiwa dhambi zake, hii ni balaa.