Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ajizi nyumba ya njaa, nayakumbuka maneno ya Dr.Slaa Sep, 01 2015 pale Serena wakati akielezea sababu za kuondoka Chadema, alitoa neno moja zito kwamba 'siasa ni sayansi'. Wengi walimpiga vita badala ya kutafakari.
Baada ya mfanyabiashara na diwani wa Mbagala kupitia CCM ndugu manji kuingia hatiani katika masakata mbali mbali ambayo kimsingi wabunge wa Chadema ndiyo walikuwa wakiyaibua huku wakilalamika kwanini serikali haichukui hatua. Kwa kifupi kuna hoja hizi nne,
Kumbe yeyote anayekiuka maadili, mbadhirifu ni mfuasi wa Lowassa.

- Mosi ni ile kasha ya maji kununua kwa bei ndogo kiwanja cha NSSF na kuwauzia NSSF kwa bei ya 'kutupwa' baada ya muda mfupi,
- Pili ni jinsi manji alivyotaka kujimilikisha jengo la PSPF lililopo Nyerere Rd. kiujanja ujanja na
- Tatu ni kutaka kumiliki ufukwe wa Coco kwa njia zisizo halali na
- Nne ni kugombea udiwani kupitia CCM ili aukwae u-Meya na kisha kujimilikisha baadhi ya ardhi za kimkakati jijini DSM kiasa cha baadhi ya watu kulalamika pengine atakuwa ni meya wa kwanza asiyejua kiswahili fasaha.
- Eti vitendo bya serikali kurudisha ufukwe wa Coco,jengo la PSPF vimeongozwa na chuki na kukomoana.
- Eti, Manji ni mwema sana, ila anaadhibiwa sababu alikuwa mfuasi wa Lowassa,
- Eti, Manji anaonewa sababu alikataa kuchangia kampeni za JPM
- Eti, Serikali inawaonea matajiri na haitaki wafanyabiashara
- Eti, hata Sethi na Ruge wa IPTL wanaonewa tu serikali iache uonevu ili wawekezaji waendelee kuwa na imani na mazingira ya uwekezaji.
Kumbe yeyote anayekiuka maadili, mbadhirifu ni mfuasi wa Lowassa.