CHADEMA imethubutu, ni mfano bora kwa vyama vingine vya siasa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Naomba nianze na maneno kwamba, Hongera Chadema kwa mwenendo mzuri wa matumizi ya umma kwamjibu wa ripoti ya CAG. Unaweza kushangaa, lakini mshangao wako utakuwa halali kama wewe ni mwanaharakati tu sio mchambuzi na mkweli wa nafsi yako.

Kwawale ambao hamjasoma Ripoti ya CAG bali mnasikia tu na kulishwa maneno ya propaganda kwamba ndani ya Chadema kuna ufisadi, naomba ninukuu na niwasomee hapa ilivyoandikwa ili kuepuka upotoshaji wa ccm ambayo imethibitika kuiba bilioni zaidi ya 4.6

Nanukuu ripoti ya CAG.

"Mnamo tarehe 30 Machi 2017, Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliingia Mkataba na Kampuni ya AMC Tanzania Limited kwa ajili ya ununuzi wa gari jipya aina ya Nissan Patrol Y61 Series yenye moduli ya GRX kwa bei ya Dola za Kimarekani 63,720 (sawa na Sh.147,760,080). Kifungu cha 1 cha Mkataba uliosainiwa kilitamka gari litakalonunuliwa lisajiliwe kwa jina la Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA. Hata hivyo, gari hilo lilisajiliwa kwa jina la Mbunge, kinyume na Sharti la 1 la Mkataba uliosainiwa. Vilevile, nilipitia Rejista ya Mali za Chama na kubaini hakukuwa na kumbukumbu za gari aina ya Nissan Patrol Y61 Series yenye Moduli ya GRX kwenye Rejista ya Mali za Chama, licha ya gari hilo kutumika na CHADEMA. Zaidi ya hayo, gari lililonunuliwa liliingizwa kwenye Taarifa za Fedha za Chama kama Mkopo uliotolewa kwa Mbunge bila ya makubaliano yoyote kati ya Mbunge na Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA. Aidha, nilibaini kuwapo kwa mawasiliano ya barua kati ya Mbunge na CHADEMA kuhusu kusitishwa kwa Mkataba wa Mkopo na urejeshwaji wa gari hilo. Jambo hili lilitokea mapema tu baada ya kutoa hoja ya Ukaguzi. Hata hivyo, wakati wa ukaguzi wangu Februari 2019, Mkataba wa Mkopo huo haukuwasilishwa kwa ajili ya ukaguzi.
Maoni yangu ni kwamba, kuonesha thamani ya gari kama mkopo kwa Mbunge kunapotosha watumiaji wa Taarifa za Fedha za chama.

Kwa mantiki hiyo, usajili wa gari husika ufanyike kwa jina la mmiliki ambaye ni Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na deni hili liondolewe kwenye Taarifa za Fedha za chama. CAG (2019) "Ripoti ya Serikali Kuu" Uk. 324-325."

Sasa kwa mtu makini anayejua kuchambua mambo ya kitaasisi kwa ufasaha ni lazima atulie apime tulikotoka, tuliko na tuendako. Kwa lugha ya kihasibu, nikuwa Chadema imekutwa kuna ubadhilifu wa milioni mia moja arobaini na saba elfu, laki saba na sitini (147,760,080) katika mwaka wa 2017/2018.

Sasa ili twende sawa hebu turejee kwenye ripoti ya CAG ya 2016/2017 ili tujiridhushe kama Chadema imefanya vizuri leo au umeharibu na kwanini mimi napata ujasiri wa kuipongeza.

Ripoti ya ukaguzi wa hesabu iliyoishia Juni 30, 2017 iliyowasilishwa bungeni, ilionyesha kati ya vyama 19 vilivyopata usajili wa kudumu, tisa havikuwasilisha taarifa za fedha wakati sheria inataka viwasilishe ifikapo Septemba 30 kila mwaka.

Katika ukaguzi huo, CAG alihoji matumizi ya jumla ya zaidi ya Sh7 bilioni kwa Chadema. Na kwa upande wa ccm CAG alihoji matumizi ya zaidi ya bilioni 12. Kwa hapa nitachambua ya Chadema kwanza ili kuweka rekodi sawa.
Mchanganuo wa CAG kwa hoja hiyo ya sh.7 bilioni kwa Chadema ni kama ifuatavyo,

Katika ripoti hiyo, CAG anasema Aprili 11, 2015 Chadema iliingia makubaliano na mwanachama wake ili awakopeshe Sh2 bilioni kwa ajili ya shughuli za chama.

Hata hivyo, anasema hawakukuta nyaraka zinazoonyesha kiasi hicho cha mkopo walichokubaliana iwapo kilitolewa na kupokewa na chama husika. CAG anasema katika ukaguzi, alikuta ankara ya kodi (tax invoice) yenye namba 201508226 iliyotolewa Agosti 26, 2016 ya Sh866.6 milioni ambayo ililipwa na mwanachama kwa niaba ya chama kwa ajili ya mabango ya matangazo yaliyoletwa na mzabuni M/S Milestone International Co. Ltd.

Anasema nje ya deni hilo, Sh715 milioni zililipwa kwa mwanachama kama marejesho ya fedha iliyokopwa kulipia ununuzi wa mabango bila ya kuambatishwa makubaliano ya kisheria.

Pia, anahoji matumizi ya Sh2.3 bilioni ambazo ni makusanyo ya Chadema kwa wanachama wake kwa mwaka 2014/15 na 2015/16, fedha ambazo zinadaiwa kutopelekwa benki na matumizi yake kutotolewa kwa ajili ya ukaguzi.

Ripoti ya CAG inaonyesha kuwa Chadema ilifanya ununuzi wa Sh2.1 bilioni bila ushindani; malipo ya Sh240.1 milioni yenye nyaraka pungufu; na Sh558.9 milioni ambazo ni masurufu ambayo hayakurejeshwa.
_________
Saaa turejee kwenye hoja ya msingi, Mwaka jana Chadema ilibainika kuwa na kasoro ya bilioni 7 za kitanzania katika matumizi yake, huku ccm ikibainika kuwa na kasoro ya bilioni 12 katika matumizi yake.

Ccm inapokea ruziku kati ya milioni 800 hadi 1b kwa mwezi, hii ni sawa na bilioni 17. 2 kwa mwaka. Na Chadema inapokea ruzuku kati ya milioni 200 hadi 240 kwa mwezi hii ni sawa na bilioni 2.4 kwa mwaka. Hivi ndivyo sheria ya vyama vya siasa inavyotaka kulinga na idadi ya kura za urais kwa kila chama na idadi ya wabunge wa kila chama.

Ukichukua taarifa ya fedha ya mwaka jana yenye ubadhirifu wa 7bilioni na kulinganisha na taarifa ya fedha ya mwaka huu yenye ubadhirifu wa milioni 147,760,080 utaona kwamba, Chadema imejirekebisha sana kwa wastani wa asilimia 99.89.

Huu ni mwenendo mzuri kwa chama kinachojipambanua kupigana na rushwa na ufisadi na chama ambacho kinajiandaa kushika dola. Hivyo tunapoichambua Chadema kupitia ripoti ya CAG, ni lazima tuwe na cha kulinganisha, na kwa vyovyote vile tutatumia ripoti ya mwaka uliopita na sio vinginevyo. Kinyume na hapo tutakuwa wanamihemko tu na sio wanasiasa na wachambuzi wa mambo anuwai. Tuendelee kuikosoa Chadema ili ijisahihishe zaidi lakini tuna uhuru wa kuipongeza kwa hatua hii. Katika hili nathubutu kusema Chadema imefanya vizuri sana kuliko chama chochote cha siasa kulingana na ripoti hii ya CAG.

Na Yericko Nyerere
 
Hali ya mgonjwa inaendelea vizuri naomba tuzidishe michango
Screenshot_2019-04-11-21-44-58-1.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ya mgonjwa inaendelea vizuri naomba tuzidishe michangoView attachment 1068986

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani wewe ulichanga?
Kama hukuchanga you have got no right kujadili matumizi
Ulitaka awe mnyonge asifurahie maisha kwa sababu tu kachangiwa
Acha roho ya kimaskini
Enjoy your moment Lissu umepitia magumu mengi kwa ajili ya watu kama hawa lakini hawajitambui...
Ya Sudan yatawakuta nyie haya!
 
Nimechanga ndiyo maana nahimiza nyie mliobaki mchange pia huoni afya yale imeimalika? Au umeelewa nini hapo?

Mkuu hawa wafuasi wa CCM siasa nyepesi zinazofanywa na viongozi wao hasa was awamu hii zimeshaharibu ubongo kwa kiwango Cha lami hawatakuelewa.Ni rahisi kwao kushangilia hasara ya ATCL kuliko kuelewa ukweli huu.Mungu aisaidie tu nchi yetu
 
Ni kama umezidi kukivua nguo chama chako cha Chadema.

Wizi ni wizi tu hata ukiiba kijiko!
 
Naam imethubutu magari matatu ya chama yanamilikiwa na mbunge-CAG report 2017/18

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio maana ccm inatumia zaidi vyombo vya dola kufanya siasa kwani uwezo wa kujenga hoja kuanzia mwenyekiti wake taifa mpaka nyie wavimba macho ni mdogo mno. Mwenzako Yericko kaja na uchambuzi wake na kuonyesha hao cdm toka matumizi mabovu ya 7b ripoti iliyopita mpaka 147m ya ripoti hii tena kwa taarifa halisi ya mkaguzi wa serikali. Ww unakuja na utoto eti magari matatu kwenye ripoti unayoifahamu ww.
 
Vijana wa mbowe kazini
Mtu anajisifia kua kaiba kidogo tu mil 147
Wizi ni wizi tu,haswa ukiwa wa pesa za umma
Nyerere aliwahi kumfunga Walter Bugoya,aliekua.meneja mkuu.wa Tanzania Publishing House kwa kujichotea shilingi.500 kwenye shirika
 
Back
Top Bottom