mkuu huo uongozi wa hawa jamaa utafikiri ni uongozi wa kigango fulani kwenye jimbo fulani. yaani ni full watu wa imani moja. halafu wanatarajia tuwachague. maajabu haya. kwa kifupi chama kukubalika hapa Tanzania na watu wa jamii zote lazima kiwe na wawakilishi kutoka jamii zote. hili tatizo litawatesa sana chadema na CUF. nitasema kweli daima hata kama itawauma na kuja kunitukana humu. ndo maana jaji john tendwa kipindi akiwa bado msajili wa vyama aliwashauri vyama viungane angalau viwe na sura ya kitaifa wakaja na kejeli kibao badala ya kuufanyia kazi ule ushauri.
wakati CUF na chadema wakigawana wapiga kura/wanachama kwe misingi ya dini CCM inachukua nusu nusu kila upande na kujipatia ushindi. na kwa staili hii ccm kuondoka madarakani ni ndoto hata kama watakuja kutuibia hata macho yenu achilia mbali hayo madini na rasilimali zingine wanazoiba huko maporini, majini, vijijini na mijini.
CHAMA NI LAZIMA KIWAKILISHE JAMII ZOTE ZA WATANZANIA KUANZIA DINI ZAO, KABILA ZAO NA KANDA WATOKAKO. lakini sio kujanza wachanga tu au wapemba halafu mnatarajia tuwachugue. mtakuwa wapinzani wa milele.