Miaka yote Chadema imeshinda chaguzi kwa kutumia nguvu ya Umma tu sio Tume ya Uchaguzi wala mbeleko nyingine yoyote.
Mbowe na Vijana wake wanataka kuwadanganya Watanzania kwa kutoa visingizio hafifu. Hakuna uchaguzi ambao haujawa na matukio ya vurugu tangu nimeingia kwenye siasa za upinzani. Watu wamefungwa, wameuawa, wamedhalilishwa, wametezwa na kufanyiwa kila lililo baya.
Ukweli ni kuwa
1. chama hakina fedha za kushiriki uchaguzi. Unahitaji zaidi ya 1.6 bilioni kushiriki uchaguzi uliotangazwa na ni fursa kubwa ya kufanya siasa kwa wale wanaolalamikia uminywaji wa demokrasia.
2. Nguvu ya Umma imekufa. Mgawanyo wa fursa za viti Maalum ngazi ya Ubunge na Udiwani, dhuluma katika Chaguzi za ndani , mgawanyo wa kinyonyaji wa ruzuku na tofauti kubwa ya kipato kati ya viongozi wa makao makuu na ngazi za chini vimewavunja moyo Makamanda wengi. Hawako tayari kuumia au kufa kwa ajili ya Chama tena maana wamegundua wanawanufaisha wachache
3. Woga wa viongozi wa Sekretarieti.
Sekretarieti inaongozwa na waoga, wasaka fursa wenye kuangalia Pesa tu. Hawako tayari kurisk maisha yao kwa ajili ya Chama. Matokeo take wanamdanganya Mwenyekiti na kumtia hofu.
4. Kamati kuu Butu.
Kamati kuu ya sasa ni rubber stamp. Akishaamua Mh. Mbowe, John Mrema, Regy wengine wanaitikia tu. Wachache wanaohoji wanatiwa msukosuko na wengine hususan Maprofesa wameamua kukaa kimya maana hawasikilizwi wala kupewa heshima
Wanachama Wabunge na Viongozi wasipochukua hatua Chama kinakufa na wote tutakuwa tumepoteza muda na rasilimali nyingine.