mtechnical
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 356
- 877
Kwa huzuni kubwa niseme kuwa chama cha CHADEMA ni kama kimeshajifia.
CHADEMA imebaki hasa hasa kwa wanaharakati wa demokrasia tu ila imepoteza kwa kiasi kikubwa uungwaja mkono wa wananchi, huu ni ukweli mchungu.
CHADEMA ILIFIA WAPI?
Kifo cha CHADEMA kilianza kwenye uchaguzi wa 2015 pale walipo mpokea Lowasa kuwa mgombea wao, lile lilikuwa kosa kubwa la kutosha kabisa kuwaua, na bahati mbaya wakaendelea kujipiga risasi wenyewe kipindi cha Magufuli na Magufuli wa udikteta wake akawachimbia kaburi kabisa.
CHADEMA ilipata uungwaji mkono mkubwa wa wananchi kwa vita yake dhidi ya ufisadi na wizi wa rasilimali za nchi, iliwaaminisha waTanzania kuwa hii nchi haitakuwa masikini kama ufisadi ukikomeshwa muda huo huo ikiwatuhumu viongozi kadhaa kuwa ni mafisadi papa na namba moja akiwa Lowasa.
CHADEMA walipo mkubali Lowasa wakalazimika kuachana na ajenda iliyo wapa uungwaji mkono ya ufisadi wakabaki kumsafisha Lowasa. Baada ya uchaguzi kuisha na Lowasa kurudi CCM wakakosa ujasiri wa kuendelea na hoja ya ufisadi.
Bahati mbaya Magufuli akawa dikteta akawapa hoja mpya ya demokrasia ambayo ndio wanaendelea nayo hadi hivi leo. Bahati mbaya kwao ni kuwa hoja ya demokrasia haina mvuto kwa asilimia kubwa ya watanzania isipokuwa wanasiasa na wanaharakati tu.
Mtanzania ambaye hana hata mpango wa kupiga kula ukija na hoja ya NO REFORM NO ELECTION yani unamshawishije? Kwanza nakuona kama unawaza kushika madaraka tu.
CHADEMA ndio ilikuwa tumaini pekee la kuiondoa CCM ila kwa sasa watanzania wameshakata tamaa. Ili CHADEMA ifufuke basi irudi kwenye misingi yake ambayo ni vita dhidi ya ufisadi na ubadhilifu wa mali ya uma.