CHADEMA imepigiwa ngoma, ikacheza halafu ikashtuka

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kama ilivyo kawaida ya Kitengo cha Propaganda cha chama tawala,Ndugu Edward Lowassa alitumika kuwavuruga CHADEMA. Kitengo kilikuwa kikiwatumia waandishi wapenda nakshinakshi kuwapigia ngoma CHADEMA ili waicheze. Waandishi walikuwa wakiandika habari kila uchao kuwa CHADEMA inamkaribisha na hata kutaka kumpa nafasi ya kugombea Urais Ndugu Lowassa. Si mliamini?

Waandishi walitakiwa kuwafuata popote walipo,kama njia ya kuwachokoza ili ngoma kuicheza,viongozi waandamizi wa CHADEMA. Ngoma ilishaanza kupigwa kwa ufundi usio na makundi. Lowassa akatumika kuchochea moto ili CHADEMA waonekane hawana mgombea isipokuwa yeye mkatwaji wa Dodoma. Raha ya CCM, siku zote ni kuwaweka CHADEMA 'bize' ili mambo yetu tuyamalize. CHADEMA wameshtuka.

Ukweli wa mambo ni tofauti na ngoma-chonganishi iliyokuwa ikipigwa kupitia vyombo vya habari. Waandishi wabishi bado wanaendelea. Wengine wameshajua. Wamejua kuwa CHADEMA haikuwahi kuwa na mazungumzo,ya siri au dhahiri,na Lowassa. Wamejua kuwa Kitengo kilikuwa kinapiga ngoma za kizamani ambazo zilipigwa wakati wa Zitto. Ngoma-chonganishi.

CHADEMA mna bahati sana. Intelijensia yenu iko vizuri. Lakini,si mcheze tu? Mbona ngoma zinanoga tu? Acheni kujifanya wajanja kama wenye mkwanja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
mkuu una maoni gani juu ya lembeli na esther kuwakimbia?ina maana ccm wabunge wanaojenga hoja zenye masilahi kwa wananchi ni adui kwenu?
 
Mzee TUPATUPA wewe ni shushu unayeifanya Kazi yako kwa usitadi wa hali ya juu saana.
Kwa kulitambua hilo, Umenishinda.
Wewe ni kichwa.
 
Kwa hiyo mzee Tupatupa unachotaka kutuambia ni kuwa kumbe hata yale maneno kuwa kuna ugomvi mkubwa sana umezuka kati ya Dr Slaa na Mbowe, kumbe ilikuwa ni propaganda na uchonganishi wa wale jamaa wa KITENGO?

Kweli sasa nimeanza kuyaamini maneno ya Dr kuwa intelejensia yao ni kali mno kiasi kwamba wakati jambo bado linajadiliwa na KITENGO, tayari wao wanakuwa na taarifa ya kila kinachojadiliwa.
 
Chadema walikuwa wameshatolewa posa na CUF...baada ya kusikia kuna fisadi mwenye pesa ameachika (EL), wakamua kusitisha maandalizi ya harusi!
 
ccm iliweza kwa NCCR mageuz then ikaweza pia kwa CUF nw wanajaribu kwa chadema bt watashindwa kwan chadema inapitia njia zile zile walizopitia ccm mpaka imefika hapo walipo ni ngum kumpiga kiwepesi m2 mliepitia dojo moja na mwalim wenu alikuwa mmoja
 
Hao wala hatuna shida nao kwa mtaji gani walio nao huku bara?Huyo mbunge mmoja wa jimbo na mmoja viti maalum? Wakaungane na Act kwani walishawahi kuhutubia mkutano wa pamoja huko kusini hivi karibuni.
 
Kama ilivyo kawaida ya Kitengo cha Propaganda cha chama tawala,Ndugu Edward Lowassa alitumika kuwavuruga CHADEMA. Kitengo kilikuwa kikiwatumia waandishi wapenda nakshinakshi kuwapigia ngoma CHADEMA ili waicheze. Waandishi walikuwa wakiandika habari kila uchao kuwa CHADEMA inamkaribisha na hata kutaka kumpa nafasi ya kugombea Urais Ndugu Lowassa. Si mliamini?

Waandishi walitakiwa kuwafuata popote walipo,kama njia ya kuwachokoza ili ngoma kuicheza,viongozi waandamizi wa CHADEMA. Ngoma ilishaanza kupigwa kwa ufundi usio na makundi. Lowassa akatumika kuchochea moto ili CHADEMA waonekane hawana mgombea isipokuwa yeye mkatwaji wa Dodoma. Raha ya CCM, siku zote ni kuwaweka CHADEMA 'bize' ili mambo yetu tuyamalize. CHADEMA wameshtuka.

Ukweli wa mambo ni tofauti na ngoma-chonganishi iliyokuwa ikipigwa kupitia vyombo vya habari. Waandishi wabishi bado wanaendelea. Wengine wameshajua. Wamejua kuwa CHADEMA haikuwahi kuwa na mazungumzo,ya siri au dhahiri,na Lowassa. Wamejua kuwa Kitengo kilikuwa kinapiga ngoma za kizamani ambazo zilipigwa wakati wa Zitto. Ngoma-chonganishi.

CHADEMA mna bahati sana. Intelijensia yenu iko vizuri. Lakini,si mcheze tu? Mbona ngoma zinanoga tu? Acheni kujifanya wajanja kama wenye mkwanja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Lakini na wewe mzee Tupatupa umeshasahau kuwa wewe ndie ulikuwa mstari wa mbele kutuaminisha kuwa Lowassa atajiunga upinzani kati ya chadema au Act. Nilikujibu wazi wazi kuwa Lowassa hawezi kujiunga upinzani kwa vyovyote vile. Unawaona hata madiwani wa Monduli ambao hawakumsoma Lowassa japo wako nae jimboni walivyojidanganya eti wamepata hasira zaidi ya mwathirika na kutimkia chadema. Unawaona wanavyohaha kurudi ccm kwa viapo vibaya kuwa walidanganyika?
 
Mzee tupatupa kwa bahati mbaya hicho kitengo kimebaki kinaongozwa na wazee, wanatumia mbinu za kizee sana ndio maana wamebaki na uwezo wa kung'oa kucha na meno tu. Ki ukweli uwezo hawana bali wamebaki kulazimisha madaraka kwa kutumia nguvu za giza. Hawajajua siku hizi mazoba wameamka, matokeo yake wamebaki wao ndio wamelala wakidhani bado watu ni wajinga.
 
Mkuu sijawahi kusema na hata kufikiri jambo hilo. Nianike hapa kwa ushahidi

Mzee Tupatupa
 
Mzee tupatupa kwa bahati mbaya hicho kitengo kimebaki kinaongozwa na wazee, wanatumia mbinu za kizee sana ndio maana wamebaki na uwezo wa kung'oa kucha na meno tu. Ki ukweli uwezo hawana bali wamebaki kulazimisha madaraka kwa kutumia nguvu za giza. Hawajajua siku hizi mazoba wameamka, matokeo yake wamebaki wao ndio wamelala wakidhani bado watu ni wajinga.

Ngoma mmeicheza au hamjaicheza?? Jibu swali
 
ccm iliweza kwa NCCR mageuz then ikaweza pia kwa CUF nw wanajaribu kwa chadema bt watashindwa kwan chadema inapitia njia zile zile walizopitia ccm mpaka imefika hapo walipo ni ngum kumpiga kiwepesi m2 mliepitia dojo moja na mwalim wenu alikuwa mmoja

Mbowe mbona amechezeshwa hiyo ngoma mkuu??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom