Barongo E
Member
- Apr 10, 2014
- 26
- 7
Lissu bungeni anasema kuwa suala la hati ya muungano limekwisha yaani amekubali kushindwa!Lakini baada ya hapo mwanasheria huyu akachemsha.
Anasema muungano unawaonyesha waasisi wawili tu yaani Mwl.Nyerere na Mzee Karume huku ukiacha kuwatambua watu muhimu walioshiriki kuunda muungano kama vile Oscar Kambona,Job Lusinde,Hanga na Othman Sharrif.
Watanzania waambiwe ukweli wa kwanini watu hawa wamekuwa sidelined wakati mchango wao ulikuwa mkubwa.Bwana Lissu toa kwanza kibanzi kilichopo machoni pako kabla ya kutoa vibanzi vilivyopo kwenye macho ya wenzio.
Mbele ya safari masuala hayo hayo ya kuwa sideline watu yatakuja kuwaandama wote mnaowanyonga kisiasa vijana wenzenu wa Chadema kina Zitto Zubeir Kabwe,Habib Mchange,Dkt.Kitilla Mkumbo na Samson Mwigamba huku wakiwa wametoa mchango mkubwa sana kwenye chama cha Chadema na kwenye Taifa.
Badala ya kujenga mshikamano ndani ya chama cha Chadema,mnakimbilia kujenga mshikamano na vyama ambavyo havina hata nguvu ya kisiasa nchini!Yetu macho!