Mwanzo CHADEMA ilikuwa inavuma Arusha na Moshi,baadae Mbeya na Morogoro kidogo,kwa kampeni za mwaka huu naona maeneo mengi ambayo sikuyatarajia naona hamasa kubwa za watu kuhudhuria mikutano ya CHADEMA,sasa hivi kila anapotembelea Lissu anavunja rekodi ya mkutuno uliopita.
Leo Kagera naweza kusema wamevunja rekodi ya kuhudhuria mkutano wa Lissu.
Tusione ajabu sehemu nyingine ikavunja rekodi ya Kagera. Hongereni watanzania na viongozi wote wa CHADEMA kwa uvumilivu wenu.Sifa za pekee ziende kwa Lissu na Mbowe