CHADEMA imegawanyika lakini itaimarika

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Jan 13, 2013
192
23
UTANGULIZI

Kufuatia skendo za muda mrefu ndani ya CHADEMA, nani anastahili kuwa mwenyekiti wa chama, Zitto anatumiwa na maccm, Lema vs Zitto na Dr Slaa and Mbowe vs Julianna Shonza and Mwampamba hakuna ubishi chama nikipendacho kimegawanyika. Hivi karibuni KAMATI KUU ya CHADEMA imewavua madaraka aliyekuwa naibu Katibu Mkuu na mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Zuber Kabwe, Mjumbe wa Kamati kuu na mhadhiri wa chuo kikuu Dr Kitilla Mkumbo na aliyekuwa mwenyekiti wa chama jijini Arusha Bw. Samson Mwigamba.

Wamevuliwa madaraka kwa kile kinachoaminika kuwa ni kugudulika kwa mkakati wa mabadiriko ndani ya chama 2013, mkakati ulioratibiwa kupitia waraka maalumu ambao watuhumiwa Mwigamba na Kitila wamekiri kuutambua na kushiriki kuuandaa. Waraka huu/mkakati huu umetafsirika kikatiba ya chama kuwa ni uasi/uhaini dhidi ya chama kwa ujumla, kwa kuwa unaonekana wazi wazi kuandaa kwa siri mabadiliko ya uongozi wa ngazi za juu muhusika mkuu akiwa MM (Zitto) na wenzake, M1, M2 na M3 ambapo M2 hajajulikana na inaelekea yumo ndani ya chama katika nafasi nyeti.

Mkumbo na Mwigamba ambao wote wamekili kuwa ndiyo akina M1 na M3 wamekaririwa na vyombo vya habari wakisisitiza kuwa MM ni Zitto Kabwe ila 100% hakuwa akijua lolote kuhusu mchakato huo na ilisubiliwa mwisho wa siku ataarifiwe kuona kama yuko tayari au hayuko kuyari kukubaliana nao. Kumeibuka maswali ndani na nje ya chama kwamba ikiwa kama kweli Zitto hakujua mpango huo ameonewa na waraka huo haikuwa sababu ya kumvua madaraka na wanachama wamemkariri Zitto akiongea na waandishi wa habari kuwa hiyo sio sababu kuna sababu nyingine ambazo anaowaita hawataki mabadiriko wanazijua. Hali hii imezidi kuwasha moto wa kukigawa chama.

KUGAWANYIKA
.

Wamekuwepo wanachama ambao wameamini kila inapokaribia uchaguzi wa ngazi ya uenyekiti wa chama wanaoonesha nia ya kuwania kiti hicho ikiwa si wanaowavutia Mtei na Wakaskazini wengine wadau wakuu wa chama chetu wanapigwa zengwe la nguvu. Wanatoa mifano ya kina Chacha Wangwe na hii leo Zitto Kabwe. Wengine wanaamini kinachotokea sasa hivi dhidi ya Zitto ni kwa sababu ya ninavyomjua hata mimi kuwa ni mtu anayependa sifa za kipekee na asijue kuwa kiongozi wa taasisi kubwa kama CHADEMA inatakiwa sifa za jumla kwa maslahi ya chama na kwa hilo ni wazi ukipenda kujikweza utatoa siri uzijuazo za unaowataka wawe chini yako ili uwe juu.

Ukizitoa siri hizo na udhaifu wao ndani ya chama sioni tatizo ndiyo demokrasia, ila ukizitoa nje ya chama hasa kwa maccm ni tatizo kubwa ambalo mwenyewe Zitto anakubali ila anasema tatizo hilo hayuko tayari kulitengeneza kwa kuwa ana mapenzi makubwa na chama na ikiwa kuna mtu anaushahidi na tuhuma hizo auweka hadharani! Sijui mnaogopa nini kuuweka hadharani kama mnao jambo linalozidisha maswali yasiyo na majibu kuendeleza hisia kali za kukigawa chama. Wachache sana ambao ni muhimu sana kwa chama chetu wanaamini Zitto anapigwa vita sababu ya udini ndani ya chama eti kwa kuwa yeye ni muislamu kitu ambacho yeye mwenyewe anakikanusha ila sijui ni maccm au ni miongoni mwetu wenyewe imani zetu na ufinyu wa uwezo wa kuvumiliana vinapandikiza sumu hiyo!?

Kwa hali hiyo, chama changu nikipendacho CHADEMA kimegawanyika. Kamwe wanaounga mkono mabadiliko ya uongozi kidemokrasia na wanaamini uongozi wa sasa unaibaka demokrasia hawatakuwa pamoja nasi katika kura za uchaguzi mkuu 2015. Kwa wale wanaoamini ukanda unachangia kubagua ukanda fulani kamwe hatutakuwa pamoja, istoshe wale wanaoamini udini unatumika vivyo hivyo hatutakuwa nao. Chama changu nikipendacho kitabaki na wale tunaoamini Zitto na wenzake wa mfano wake walikuwa wanaenda ndivyo sivyo kiutendaji na hali hiyo ni sawa na kukihujumu chama.

Jana Dr Slaa ametofautiana kidogo na Tundu Lisu anayeamini na alitangaza kuwa waraka uliokamatwa wa mkakati wa mabadiriko 2013 ndicho kisa cha Zitto na wenzake kubanwa mbavu. Akihojiana na mwandishi wa Gazeti la Mwananchi alitumia fasihi kwanza akamuuliza swali mwandishi umeoa? mwandishi akasema sijaoa. Akamwambia ungekuwa umeoa ningekuuliza, "unaweza kuwa unatoa siri za ndani? Hii alimaanisha Zitto amekuwa akitoa siri za ndani hivyo anaamini yale yaliyomo katika taarifa iliyosomeka kuwa ni siri toka CHADEMA makao makuu iliyotapakaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari ikimtuhumu Zitto kuchukua hongo kutoka kwa maccm na kutoa siri japo chama kilikanusha uvumi huo.

Hali hii ya mkanganyiko/tofauti wa maoni kutoka viongozi mbalimbali wa juu wa chama, juu ya sababu zinazowabana mbavu ZITTO na wenzie inaendeleza wimbi la kuwachanganya akili wanachama na kuzidi kukigawa chama na wanachama.

KUIMARIKA.


Inatakiwa viongozi wa juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe afunguke na kutangaza kutogombea kiti hicho kwa mara nyingine tena, vile vile tunao wasomi na waadilifu wakubwa wenye utii na mapenzi mema na chama ambao wana sifa za kuwa Mwenyekiti Taifa, wasio wakaskazini wapewe nafasi. Vile vile ikiwa kuna ushahidi wa Zitto kushirikiana na maccm utolewe hata kiduchu mwingine ibaki kuwa siri kwa sababu za kiusalama pande zote. Zaidi ya hayo wale waislamu wenye weledi mkubwa walioko chamani wapite mikoani kote kufafanua kuwa hakuna udini bali ni hisia hasi zilizotawala.

Nadhani hili halihitaji ufafanuzi mkubwa mnaona wenyewe waziwazi sehemu ambazo kuna waislamu wengi walivyolipokea jambo hili kwa upinzani mkubwa mpaka baadhi ya viongozi kujiuzuru na wengine wamo njiani kujiuzuru. Viongozi wa ngazi za juu wawe na kauli moja sio huyu anasema hili na yule anasema lile. Matumizi ya Ruzuku ya chama yawe yenye uwiano mzuri chini mpaka juu, kwenye mashina, matawi, wilaya, mikoa, mpaka Taifa wakati huo huo nyaraka za mapato na matumizi ya chama viwe wazi 100% HAPO TUTAIMARIKA.
 
Back
Top Bottom