CHADEMA ime-savaivu, sasa nini?

... Huu ni wakati wa CHADEMA kuwa wazi kabisa na sera zao. Wananchi waelewe chama kinasimamia nini.
... Sidhani kama wanaweka mkazo kwenye kuhakikisha wana sera mbadala zinazoeleweka kwa wananchi.

Kwa uzoefu wangu mdogo nilioupata kuhusu siasa za Bongo, sehemu kubwa ya wananchi hawana muda hata wa kupima kitu kinachoitwa sera. Ni mihemko tu, ukiwaudhi wanakutosa kwa mihemko, ukiwateka kwa hoja nyepesi nyepesi tu, wanakupigia makofi na kukuchagua kwa mihemko pia. Sera zipo kwenye documents za vyama, ila wananchi wengi wala huwa hawana muda wa kuzitathmini. Pengine hata wewe ukiulizwa sera gani kumi zilikuvutia ukakichagua chama ulichokipigia kura, huenda ukajitahidi kukumbuka tatu tu, tena si kwa sababu umezitathmini, ila kwa sababu zimeimbwaimbwa ukazikariri
 
Tatizo lako nalijua kutokana na maandiko yako humu.

Unajibu nilichoandika kwa pupa bila kuelewa kimeelezwa kitu gani.

Ni sehemu gani ya anadiko hilo nililoweka hapo inaeleza kwamba niko CHADEMA, au kwa vile tu ninaisuta CCM?

Ndiyo, CCM tokea enzi za Mwinyi hakijawa tena chama cha kutetea maslahi ya wananchi. Kimekuwa chama cha 'opportunists' tu wanaojitafutia maslahi.
Sasa kama unadhani kwa kusema hivyo ndio kwamba nasema CHADEMA ni malaika, huo utakuwa ni upotofu wako.

CCM hadi mwisho wa Magufuli ilikuwa imekufa, lilibaki kopo tu alilotumia Magufuli kufanya yake atakayo.

Sasa sijui kama huyu mama atakuwa na lolote la kuiimarisha tena CCM kiwe chama cha kuiletea Tanzania manufaa.

Akifanya hivyo, sina tatizo kumsifu na kukisifu chama.
 

JPM hajakwapua wewe. Soma historia yake. Ndo mana ukitaka kujua CHadema waliandika taarabu ya kutafuta Kura. Ukiwa mpinzani sera yako haiwezi kuwa mbaya mana unajua hutaweza kuitekeleza mpaka Uwe madarakani. Ndo mana unaona JPM aliwachanganya sana mkawa watu wa matukio. Yeye Ni Mtendaji. Nyie kazi yenu ohh. Demokrasia. Sijui hata kama mnaelewa maana yake. Kwenu mmeshindwa. Ila kuongea mnaweza.

Hivi umefanya tathmini ya utendaji wa CHadema wakati wa Kikwete. Ile ndo Demokrasia. Kutukana na kufanya nchi isitawalike. JPM aliwasoma so alichokuja nacho Ni dawa yenu. Siasa Siasa haziwezi ijenga Tz ambayo kila mtu Ni mjuaji. Kila kijana anataka utajiri kabla hata ya jacho halali. Kila mtu anataka kuiba nk.

Acheni kuanza hoja kwa prejudices. Zinawaangusha sana. Embu jiangalieni wenyewe. Mgombea wa uraisi Yuko anaongea na Kenya kuhusu mambo ya Tz. Hivi odinga aliwahi kuja Tz kutukana wakenya. Mlipoangukia hamuoni. Ila badilikeni Ila Lissu hatawapeleka popote. Huku mnadanganyA sana. Nenda kakiwashe huko Insta na FB. Utajua
 
Mosi, naamini kwamba CHADEMA waliingia uchaguzi wa 2020 sababu hawakuamini kwamba CCM wangeendesha uporaji wa kiwango hicho katika uchaguzi mkuu. Walitarajia uwepo wa waangalizi wengi wa kimataifa. Magufuli alikwepa hili la waangalizi kwa kukataa fedha za UN, ambazo ndio huambatana na waangalizi hao. Kwa hiyo akadai kwa wananchi kwamba uchaguzi huu haitumiki fedha ya nje bali ya ndani tuuu!!! Kumbe kazima taa ili akwibe kwa amani na utulivu.
Pili CHADEMA wali-underestimate kiwango cha kukosa aibu cha Magufuli, hawakuamini angeweza kuendesha kiwango hicho cha ujambazi.

Kuhusu wananchi kulinda kura zao, ni vile tu kwamba hawajafikia kiwango hicho, ipo siku watafikia. Lakini pengine matokeo ya wizi huo ni kutengwa kimataifa kiasi kwamba kuendesha nchi sasa ni ngumu zaidi. Serikali inazidi kuwapora wananchi wake. Angalia package za bima ya afya za Magufuli. Ni wizi mtupu. Ni mradi wa kukusanya fedha ya miradi yake na siyo huduma ya Afya kwa wote.

Sidhani, kama ulivyosema pia, kwamba serikali itathubutu kuiba kura tena kwa viwango vya serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020. Inahitaji 'kichaa' na sidhani kama hao waliopo CCM sasa ivi kuna mwenye kiwango hicho cha ukichaa.

Ni kweli CHADEMA wanaendelea kuenjoy kura za chuki na pia sympathy. Wanateseka mno na pia maisha kwa wote ni magumu sana. Wakiboresha meseji yao itakuwa vema zaidi
 
Mbona Chadema wanakuwaga na sera nzuri kuliko vyama vingine vyote, Mfano ilani ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 ya CHADEMA ilikua moja ya sera zilizokua zinakitisha chama cha kijani kuondoka madarakani, hata hivyo kura hazikutosha ila uchaguzi uliofanyika hivi 2020 ulikua uchafuzi.Bi samia atuletee katiba mpya ikiwa na tume huru ya uchaguzi
 
Nimekusoma vyema.

Wananchi kutowachagua viongozi kufuatana na sera za vyama vyao, sio kosa la wananchi, ni kosa la viongozi wa vyama hivyo na vyama vyao kiujumla.
Kazi ya kuwaelimisha wananchi kuacha kuchagua viongozi kwa mihemuko, ni ya vyama vyenyewe na viongozi wao. Wananchi hawajakataa kujifunza na kuelewa hizo sera.
Kwa hiyo, tukubali tu kwamba kwa kuwa vyama vinashindwa kutimiza wajibu wao, basi tuliache tu mradi linakwenda?

Umedadisi kama hata mimi nikiulizwa sera gani kumi - huhitaji kuniuliza sera kumi. nieleze mbili tu zitakazonipa uwezo wa kujua unasimamia wapi, na ziwe za msingi kabisa, nitakuunga mkono. Huhitaji kunipa rundo la sera zote hizo kupata ufahamu wa kipi unakisimamia kwa maslahi ya taifa letu.
 
Chadema imewekeza sana kwenye mitaa na vijiji,ushahidi kamili ni uchaguzi wa uliopita. Bila figisu CCM ingeng'oka
 
Niseme tu mkuu wangu 'Mindi'; mada hii ni kuwahimiza CHADEMA "Wagange yajayo", yaliyopita liwe fundisho.

Wizi wa kura hautakoma, utaendelea kuwepo, hata kama utakuwa ni wizi wa kistaarabu chini ya utawala mpya.

CHADEMA walijue hili, na wawe tayari kufanya kazi nzito zaidi kuwavuta wananchi upande wao ili kufidia kura zinazoingia upande mwingine kwa wizi.

Ni kazi ngumu sana, lakini ni kazi inayowezekana kwa viongozi waliojizatiti kuifanya kwa ufanisi.

Hakuna mbadala wa kuwaendea wananchi kila kona ya nchi walipo na kuwaelimisha chama chao kinasimamia nini. Wananchi wakielimika, sina shaka watachagua kwa utashi wao wanachokitaka.
 
Umeandika mengi mkuu why unazungukazunguka?waambie chama dola wa LEVEL playing field na itisha mechi even today uone makali ya CDM,inasikitisha mno middle class wetu kuingiza vichwa vyao mchangani,walete tume huru ya uchaguzi ,kampeni huru(cdm wanahitaji mikutano 10 tu nchi nzima.
 
Huko unakotaka twende tulishafika na kumaliza kazi , hii ndio sababu ya Mahera kupokea maagizo ya ccm ( Bashiru , Polepole na Magufuli ) ya kuondoa wagombea wa Chadema nchi nzima na kwingine kupeleka kura za mabegi , labda nikutoe shaka , Chadema imo mpaka ndani ya ccm na atakayejaribu kuihujumu atakiona cha mtemakuni , nimemaliza
 
Wizi kistaarabu ndio nini? Hivi huwa una akili timamu?
 
Mimi siamini kama wapiga kura wa nchi hii wanachagua viongozi baada ya kusoma,kuchambua na kuelewa Sera za vyama vyao.Sidhani kama tumefikia umakini wa kiwango hicho kama taifa.
 
Sidhani, na wala sitegemei kuona uhujumu kiasi ya tuliouona chini ya Magufuli, sidhani.

Ndiyo maana sasa CHADEMA wajizatiti zaidi kuvuna walichopanda, kama kweli mbegu ilishapandwa kama unavyoeleza.

Wakati huo huo, usisahau kwamba CCM ni chama kikongwe sana na wana miundo mbinu kila mahala.

Wao pia wanayo nafasi ya kuji-'re-invent'; kama kuvua gamba hivi kwa kutumia miundo mbinu nyingi walizonazo kujisafisha kwa wananchi.

Hizi ndizo tahadhari tunazowaeleza mzijue
 
Mimi siamini kama wapiga kura wa nchi hii wanachagua viongozi baada ya kusoma,kuchambua na kuelewa Sera za vyama vyao.Sidhani kama tumefikia umakini wa kiwango hicho kama taifa.
Ninakubaliana na wewe kwa kiasi; lakini haitakuwa hivyo milele.

Wakati ndio huu.

Lakini pengine tunaweza kudadavua maana ya sera hasa ni nini. Wananchi hawana shida ya kudadavua kiundani maana ya sera hizo ndipo waelewe chama kinasimamia nini.

Hata tokea enzi zile za akina Mtemvu na Mwalimu Nyerere, bila shaka wananchi waliweza kujua TANU na Chama cha Mtemvu walisimamia nini, hata kama haikuwa kwa undani zaidi.
 
kuna vyama kazi yao ni kupima upepo ataenata na biti ndo uyouyo 2010 2015 2020 hata na 2025
kuna vyama haviaminiki wanachama wake hawana msimamo yani muda wowote wanasaliti,wengine ofisi haifanani na jina lao, haijulikani wanapigania nini mara watutishie mabeberu mara watutishie kenya mara waseme barabara,umeme sio maendeleo

uzalendo wa wapinzani unatiashaka
kwenye mambo makubwa ya kuisaidia nchi wanajitenga na kuicheka inchi inapokosea na kuiombea nchi mabΓ ya

sera ya majimbo hii kitu badilisheni asee wabongo hawaipendi na wanaambukizana kuichukia sera iyo

always upinzani ni malalamiko tuu na kueneza chuki zenu binafsi dhidi ya viongozi wa nchi kuongea point ni kwa bahatimbaya

wananchi wanaona hayohapo juu na ndo maana wanawatosaga na nyie mkitoswa mnaanza kuwatukana tena wapigakura😁😁😁😁😁
hamuwezi kuibua agenda yenu always mnadandiaga matukio mnasubiriaga myb DC achape watu ndo muibuke asipochapa mtu hamuonekani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
uhuni panyaroad wote wapo upinzani muangalie hata mayor Jacob alivokua πŸ˜‚πŸ˜‚ mara mbowe kamkula sjui nani mara lipumba karuka ukuta kajifungia ofisini mara rungwe anasema ubwabwa buree πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mara zito kamtongoza diva


asee upinzani kwa kifupi jipangeni sana
 
wakina Mbowe kinawauma zile mali na miradi yao ambayo ilibanwa kwelikweli na nyingine mpaka kupigwa mnada hii iliwauma kwelii hapo wakaona wamefanyiwa udikteta wa hali ya juu wakasahau kuwa kuna wafuasi wao walikua wanashinda bila hata kula hukoo mikoani kwa ajili wa matumbo yao Ruzuku ya kila mwezi lakini walirudi kwa wafuasi wao na kupitisha tena bakuri kwa ajili ya chama kifupi walikua wanajali maslahi yao hawakujua kula na vipofu kabisaa ila kwa fimbo hii imewapiga kweli kweli sijui watakuja na sera gani tena sidhani kama wanaweza muhubiria mwananchi kuhusu demokrasia wakati tayari wameshaonja utamu wa kasi ya hayati JPM uongozi uliokua na msingi wa kazi mbele kwa Maslahi mapana ya Taifa
 
Tulionya mapema sana kwamba shetani hajawahi kumshinda Mungu , nadhani sasa somo linaanza kueleweka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…