Chama chochote cha upinzani; kinapo karibia kushika dola ni lazma kiwe kime wiva ndani ya sifa za mzingi sita (06). Sifa hizo ndio kama viashiria kwamba sasa Chama kimefika mahala pake na sasa kilichobakia ni kuhakikisha hakirudi nyuma. Kama ni usiku; tunasema jua linaanza kuchomoza upande wake. Sifa hizo ni;
1. Mshikamano ndani ya Chama .Mshikamano ndani ya Chama husaidia katika suala zima la kutekeleza shughuli za chama katika hali ya mshikamano mkuu, bila kusalitiana na kulinda siri na mipango mikakati ya chama.Kiashiria cha kigezo hiki, ni pale unapoona viongozi wa chama wanafanya operesheni pamoja, wakikubaliana jambo hutekeleza pamoja,kwenye kampeni huenda pamoja wakipata majanga wanaomboleza pamoja .N.K.
2. Mshikamano miongoni mwa wanachama na wapenzi wa chama (wasio wanachama). Ikumbukwe kuwa ili chama cha upinzani kuweze kufanya shughuli zake vizuri na hata kiweze kushinda uchaguzi; rasilimali watu na fedha huhitajika sana. Hivyo basi ni kupitia mshikamano wa wanachama na wapenzi jambo hilo linaweza kutimia. Viashiria vya kigezo hiki ni pale tunapoona wanachama na wapenzi wanaanza kukichangia chama chao kwa hiari, wanajitokeza kugombea nafasi mbali mbali (kila mahali), wanajitokeza kwa wingi sana kwenye shughuli za chama kama mikutano bila mashinikizo, n.k
3. Kuwekeza zaidi katika kuitegemea jamii; Kwa kuwa chama ni watu na watu hutoka katika jamii, chama chochote kinacho karibia kushika dola huwa na uhusiano mzuri na mkubwa sana na jamii. Kiashiria cha kigezo hiki ; ni kuona wanajamii wakionesha mapenzi yao ya wazi kwa chama kwa kujitoa hadharani kutoa maoni yao, wanajamii kushiriki kwenye masuala ya kuki wezesha chama n.k. Katika mazingira haya chama hupata kitu kinachoitwa nguvu ya umma.
4. Uongozi imara. Chama chochote cha upinzani kinapo karibia kushika dola ni lazma kiwe na uongozi imara. Viashiria vya kigezo hiki ni pamoja na, kupanga mambo kisha wote wakafuata, viongozi wake kuweza kuwashawishi wanachama na kuchukua hatua, kuonesha msimamo thabiti pale chama kinapopatwa na msiba (mtihani/changamoto) n.k
5. Uwazi. Uwazi husaidia watu kukijua vizuri chama kilivyo. Viashiria vya kigezo hiki ni chama kutoa taarifa mara kwa mara kupitia vyombo vya habari pale inapo hitajika, kupendelea sana kufanya midahalo (japo mara nyingi waalikwa wa upande wa pili wanaweza kukwepa kushiriki), kukaribisha maoni ya wananchi wa kawaida n.k
6. Chama kuwa na viongozi wa kifikra vision leaderswa kutosha. Ikumbukwe kuwa chama pinzani kinakuwa hakijashika dola kwa hiyo ni lazma kiwe na watu walioko pembeni wenye mawazo mazuri yanayoweza kuongoza wengine na hiyo inakuwa ni dalili kwamba wakipewa dola wataweza kuwa na rasilimali watu ya ukweli kwa ajili ya kuongoza sasa. Kiashiria cha kigezo hiki ni pale unapoona kuna watu wengi wanaotoa mawazo mazuri (ya ki uongozi) nao si viongozi huku wengi wao wakiwa ni wa chama cha upinzani. Katika kupima tunaweza kufanya marejeo ya mijadala mbalimbali katia media.
Kimsingi Chama cha kisiasa kinapoweza kuwa na sifa tajwa hapo juu tegemea kuona mabadiliko karibuni. Kwa hiyo kama kwenye nchi yetu kuna chama chenye sifa hizo basi ujue ....!. Je; CHADEMA,Ina baadhi ya sifa tajwa hapo juu?
Aghhhh! Mimi sijui bwana!