CHADEMA iko Wapi Hapa?

CHADEMA iko Wapi Hapa?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,200
Reaction score
7,568
Chama chochote cha upinzani; kinapo karibia kushika dola ni lazma kiwe kime wiva ndani ya sifa za mzingi sita (06). Sifa hizo ndio kama viashiria kwamba sasa Chama kimefika mahala pake na sasa kilichobakia ni kuhakikisha hakirudi nyuma. Kama ni usiku; tunasema jua linaanza kuchomoza upande wake. Sifa hizo ni;


1. Mshikamano ndani ya Chama .Mshikamano ndani ya Chama husaidia katika suala zima la kutekeleza shughuli za chama katika hali ya mshikamano mkuu, bila kusalitiana na kulinda siri na mipango mikakati ya chama.Kiashiria cha kigezo hiki, ni pale unapoona viongozi wa chama wanafanya operesheni pamoja, wakikubaliana jambo hutekeleza pamoja,kwenye kampeni huenda pamoja wakipata majanga wanaomboleza pamoja .N.K.


2. Mshikamano miongoni mwa wanachama na wapenzi wa chama (wasio wanachama). Ikumbukwe kuwa ili chama cha upinzani kuweze kufanya shughuli zake vizuri na hata kiweze kushinda uchaguzi; rasilimali watu na fedha huhitajika sana. Hivyo basi ni kupitia mshikamano wa wanachama na wapenzi jambo hilo linaweza kutimia. Viashiria vya kigezo hiki ni pale tunapoona wanachama na wapenzi wanaanza kukichangia chama chao kwa hiari, wanajitokeza kugombea nafasi mbali mbali (kila mahali), wanajitokeza kwa wingi sana kwenye shughuli za chama kama mikutano bila mashinikizo, n.k

3. Kuwekeza zaidi katika kuitegemea jamii; Kwa kuwa chama ni watu na watu hutoka katika jamii, chama chochote kinacho karibia kushika dola huwa na uhusiano mzuri na mkubwa sana na jamii. Kiashiria cha kigezo hiki ; ni kuona wanajamii wakionesha mapenzi yao ya wazi kwa chama kwa kujitoa hadharani kutoa maoni yao, wanajamii kushiriki kwenye masuala ya kuki wezesha chama n.k. Katika mazingira haya chama hupata kitu kinachoitwa nguvu ya umma.

4. Uongozi imara. Chama chochote cha upinzani kinapo karibia kushika dola ni lazma kiwe na uongozi imara. Viashiria vya kigezo hiki ni pamoja na, kupanga mambo kisha wote wakafuata, viongozi wake kuweza kuwashawishi wanachama na kuchukua hatua, kuonesha msimamo thabiti pale chama kinapopatwa na msiba (mtihani/changamoto) n.k


5. Uwazi. Uwazi husaidia watu kukijua vizuri chama kilivyo. Viashiria vya kigezo hiki ni chama kutoa taarifa mara kwa mara kupitia vyombo vya habari pale inapo hitajika, kupendelea sana kufanya midahalo (japo mara nyingi waalikwa wa upande wa pili wanaweza kukwepa kushiriki), kukaribisha maoni ya wananchi wa kawaida n.k

6. Chama kuwa na viongozi wa kifikra "vision leaders"wa kutosha. Ikumbukwe kuwa chama pinzani kinakuwa hakijashika dola kwa hiyo ni lazma kiwe na watu walioko pembeni wenye mawazo mazuri yanayoweza kuongoza wengine na hiyo inakuwa ni dalili kwamba wakipewa dola wataweza kuwa na rasilimali watu ya ukweli kwa ajili ya kuongoza sasa. Kiashiria cha kigezo hiki ni pale unapoona kuna watu wengi wanaotoa mawazo mazuri (ya ki uongozi) nao si viongozi huku wengi wao wakiwa ni wa chama cha upinzani. Katika kupima tunaweza kufanya marejeo ya mijadala mbalimbali katia media.

Kimsingi Chama cha kisiasa kinapoweza kuwa na sifa tajwa hapo juu tegemea kuona mabadiliko karibuni. Kwa hiyo kama kwenye nchi yetu kuna chama chenye sifa hizo basi ujue ....!. Je; CHADEMA,Ina baadhi ya sifa tajwa hapo juu?

Aghhhh! Mimi sijui bwana!
 
CHADEMA ndo chenye sifa tajwa mkuu
 
chadema hapo hakina sifa hata moja ila ungeweka ishu za mandamano,vurugu,kususa na kusalitiana wangekuwepo.
 
Sifa zote chadema inazo nadhani unasisitiza kiendelee kuzilinda sifa hizo hongera
 
Vianzio vya sifa hizi vinahitajika na mahali vilipotumika kuingiza upinzani madarakani
 
Sifa kuu ya chadema ni kumwagia watu tindikali na kutembea na sumu kuwalisha wenzake hadi bar
 
Vianzio vya sifa hizi vinahitajika na mahali vilipotumika kuingiza upinzani madarakani
Soma Political parties Streghs kutoka "Instute for Education in Demogracy" ya Kenya. soma Election strategies of political parties🙁2013) by amr sluy, Soma Multy -party elections in Africa; paper py Sharis Taroor (2001); Tokyo conference; Kisha za kuambiwa changanya na zako.Usipende sana kuuliza reference kwenye uzi wenye mawazo ya jumla.Refference si muhimu; muhimu ni kama hoja inaeleweka na ina mantiki.(au kama mada inahusu tukio).Katika mazingira ya mijadala ya humu, hala huwezi ukaenda kuhakiki refference.Tuwaachie walioko darasani.

 
LWAKATARE: Kuna unafiki CHADEMA


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, WILFRED LWAKATARE amesema kuwa siasa za chuki na majungu ndani ya chama hicho zimetawala hali inayokwamisha harakati mbalimbali za kisiasa za chama hicho hadi kufikia kusalitiana hatua iliyofanya hata mipango mbalimbali kukwama. Alitolea mfano wa video aliyorekodiwa kuwa ililenga kumuumbua yeye.


Aidha taarifa za ndani za chama kutolewa nje kwa maadui wa CHADEMA kisiasa nyingi zinatolewa na viongozi na wanachama wasio waaminifu.


Hayo aliyasema wakati wa Mkutano na wanachama wa chama hicho uliofanyika Juni 19, 2013 kwenye Viwanja vya mashujaa maarufu kwa jina la Mayunga mjini Bukoba.


Aidha, Lwakatare aliwaambia wananchi waliokusanyika katika viwanja hivyo vya mashujaa kuwa nafasi yake na Ukurugenzi wa Ulinzi na Usalama inamsaidia kuwagundua maadui wake.


SOURCE:Gazeti la FAHAMU, JUMANNE Juni 25 - Julai 1, 2013
 
wewe n gamba huo unafiki ndani ya CHADEMA umeuonaje kama sio umbea? Narudia tena mwanaume wewe!
 
Tuuchukieni uongo, uzushi na unafiki mkubwa wa Chadema


Tuuchukieni uongo, uzushi na unafiki mkubwa wa Chadema Na Charles Charles MBUNGE wa Rombo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Selasini aliusifia utendaji maridadi wa kazi unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete. Selasini alitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Mkuu – Tarakea wilayani humo, siku chache zilizopita na kuwashambulia hadharani wanasiasa ambao alisema wamezoea kudandia migongoni mwa wenzao. “Nina kila sababu ya kukushukuru na kukupongeza”, alisema mbunge huyo na kuongeza kuwa kama angekuwa na uwezo angeipa barabara hiyo “jina la Jakaya Kikwete” kwa vile ndiye ametoa fedha zilizotumika katika ujenzi huo, ule uliotimiza ndoto ya miaka mingi ya wananchi wa Rombo. “Barabara hii imekuwa kwenye makabrasha tangu enzi za ukoloni, lakini Rais Kikwete ametimiza ndoto ya Warombo ya kuungana tena na wenzao kwa shughuli za kibiashara”, alibainisha. Kesho yake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe naye alimsifu hadharani Rais Kikwete alipokwenda na kuzindua Barabara ya Kwa Sadala – Masama iliyopo katika jimbo hilo. Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Nne kwa kazi kubwa na yenye mafanikio ya kujenga miundombinu ya barabara nchini na kumuunga mkono Rais Kikwete binafsi na kuongeza: “Huyu ndiye kiongozi wetu, ndiye mkuu wetu, mkuu wa nchi yetu na haijapata kutokea katika historia ya Tanzania. Mmefanya kazi kubwa sana katika kuiunganisha nchi yetu kwa mtandao mkubwa wa barabara. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais”. Wakati viongozi hao waandamizi wa Chadema wakisema hivyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa wa Chama hicho, John Mnyika alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akitaka aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), William Mhando ashtakiwe mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma. Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, amekuja na msimamo huo mpya wa Chadema miezi miwili tu baada ya Naibu Katibu Mkuu wake (Tanzania Bara), Zitto Kabwe aseme kuwa hatua zote zilizochukuliwa na serikali dhidi Mhando zilifanywa kinyume cha taratibu. Aidha, Zitto yuleyule ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea kwa nguvu zake zote kiongozi huyo wa zamani wa TANESCO akidai alikuwa amegeuzwa na serikali kuwa “mbuzi wa kafara”. Hao ndio viongozi wa Chadema ambao ukimwondoa Selasini, watatu waliobaki wote wanapozungumza chochote ndio msimamo wa chama chao kwa vile ni Mwenyekiti wa Taifa, Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Taifa wa Habari na Uenezi. Nimeshangazwa na kauli zao mpya kutokana na ukweli kuwa wote katika ujumla wao ni mitambo inayotegemewa kuzalishia uongo, fitina, uzushi, uchochezi na umbeya unaolenga kuwapandikizia hasira na chuki Watanzania ili waichukie serikali inayotawala hivi sasa. Wote wamejitokeza kuwa mabingwa wa kuhamasisha uasi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wake, lakini kazi hiyo yote inafanywa kwa makusudi na malengo ya kutaka nchi isitawalike katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015. Mbowe na Selasini waliomsifu Rais Kikwete na serikali yake, wakampamba kwa vinywa vyao majukwaani, wakakiri ubora na utendaji wake maridhawa ndio walewale ambao walifanya uchochezi mkubwa na kuongoza maandamano ya vurugu, ghasia na uhalifu wa aina zote katika jiji la Arusha hapo Januari 5, mwaka jana. Walifanya hivyo wakishirikiana na viongozi wengine wa Chadema kama vile Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa; Wajumbe wa Kamati Kuu akina Philemon Ndesamburo, Godbless Lema, Grace Kiwelu, Peter Msigwa na kundi zima la wabunge walionao. Kutoka Arusha waliendeleza vurugu zao hizo katika mikoa mingine ikiwemo ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Iringa, Njombe na kadhalika ambako pia walikwenda wakitangaza kila aina ya uzushi, unafiki pamoja na uzandiki wote unaoweza kuwatoka midomoni mwao. Walikuwa wakitangaza kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo yoyote wananchi katika kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru uliopatikana Desemba 9, 1961, na kutaka mwaka 2015 wapewe madaraka hayo wao ili waiendeleze kwa kasi. Walisema Tanzania haina miundombinu ya barabara hasa za lami au changarawe, maji safi na salama ya kunywa huku pia ikizidi kurudi nyuma katika maendeleo mengine yakiwemo ya elimu. Kibaya zaidi walifikia mpaka kudai kuwa Serikali ya Awamu ya Nne ikiongozwa na Rais Kikwete yuleyule ndiyo “ziro zaidi”. Waliwataka Watanzania bila ya kujali itikadi zao za kisiasa waitikie wito wao wa kutaka nchi isitawalike katika kipindi chake hiki cha pili, na pia wakamwambia yeye mwenyewe hatafika mwaka 2015. Wamekuwa wakipandikiza kila aina ya uasi, fitina, uzushi, hasira na chuki kwa rais huyo mwenyewe, CCM na serikali yake wakitaka wananchi wawaunge mkono na kumwondoa madarakani ikibidi hata kinyume cha katiba ya nchi! Wanatumia njia zote wanazodhani zinafaa, moja kati yake ni kile kinachoitwa ‘Operesheni Sangara’ iliyokuja kuongezewa jina kuwa ni ‘Vuguvugu la Mabadiliko’ au ‘Movement for Change (M4)’, kazi ambayo siku zote imekuwa ikitumika kutengenezea uongo na fitina za kijinga. Pamoja na kusafiri kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara na kadhalika kwa kupita kwenye lami huku wakisinzia sehemu kubwa ya safari, viongozi wa Chadema wanapofika waendako husahau hayo yote utadhani kuku wa kisasa. Wanaanza kuzitukana barabara walizopita wakidai kuwa ni mbovu huku nyingi kati yake zimejaa mashimo na mabonde, zile ambazo utakuta wanadai wanalazimika kusafiri kutoka mwanzo hadi mwisho wakiwa wamefunga vioo vyote vya magari yao ili kukwepa vumbi. Hawasemi ukweli kwamba wanafunga madirisha yote ili kukwepa upepo kwa sababu zina lami na hivyo magari yao yanakwenda kasi zaidi. Hawataki kusema kwamba siku zote wanaamshwa wakiwa tayari wameshafika waendako na kubaki wanashangaa wamefikaje kwa haraka namna hiyo! Usingizi mzito wanaolala wakati wote wanapokuwa safarini, huwafanya wasione kwa uhakika namna gani barabara za nchi hii zilivyojengwa katika kiwango cha lami, hali inayosababisha waseme uongo wanapopanda majukwaani. Wanazungumzia hadithi za miaka mingi iliyopita walipokuwa wakisafiri kuelekea shuleni kama Mbowe aliyekuwa akitokea kwao Hai, Kilimanjaro au Dar es Salaam kwenda Shule ya Sekondari ya Kahororo, Bukoba. Anadhani hali bado iko vilevile kwa sababu akisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, au Singida anakuwa amelala kwa muda mwingi kwenye gari na kushindwa kuyaona maendeleo makubwa ya miundombinu ya barabara yaliyofanywa na serikali ya CCM. Ndiyo maana anapofika huko anaanza kuwadanganya wakulima na wafugaji ambao kwao wanapokwenda mbali sana ni kutoka vijijini mwao hadi makao makuu ya kata zao, tarafa zao, wilaya zao au mikoa yao ambapo kwa kawaida huwa siyo zaidi ya kilomita angalau 10 tu. Mwanasiasa mwandamizi kama Mbowe kwa mfano akitangaza kwamba ametokea Dar es Salaam hadi Iringa na kujionea ubovu wa barabara alimopita, akadai imejaa mashimo kila mahali, mabonde na majani utadhani ina mashamba hakika mwananchi anayeishi siku zote maeneo ya Kihesa, Ruaha, Kitwiru, Mtwivila, Mwangata, Mkwawa au Nduli inakuwa kazi rahisi mno kuuamini uongo huo na kwenda kuutangaza kwa majirani zake. Hivyo ndivyo wanavyofanya viongozi waandamizi wa Chadema akina Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Peter Msigwa, Godbless Lema, Vencent Nyerere, Grace Kiwelu, Joseph Mbilinyi au ‘Mr. Sugu’ na kadhalika. Ndiyo maana pia miezi mitano tu iliyopita, Mbowe aliwaambia wananchi wa Lindi kuwa anakerwa na kushangazwa na miundombinu mibovu ya barabara nchini. Alisema hali hiyo haiwezi kurekebishwa hata iweje kama CCM itaendelea kutawala, hivyo akatangaza kwamba atazunguka kila kona akiwaomba wananchi wakiunge mkono chama chake ili mwaka 2015 kitawale na kusema anaamini wataelewa, kisha akaahidi kujiuzulu endapo watashindwa tena katika uchaguzi huo mkuu. Alisema kuwa atafanya hivyo kwa vile Watanzania watakuwa “wamemwambia kwamba wamezoea kuishi kwa taabu” bila ya barabara ambazo zimejengwa kwa lami. Atakuwa ameelewa kwamba “hawataki nchi yao ipate maendeleo” isipokuwa vinginevyo. Katika hali hiyo, Mbowe ambaye kuna wengine wanamwelezea kuwa ni rasta wa zamani ndipo akaahidi kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisiasa, nafasi ambayo itatoa fursa kwake ya kurudi upya kwenye shughuli za kasno la Billicanas Night Club kusimamia tena disko lake kama mwanzo. Lakini kwa vile uongo siku zote haudumu kwa muda mrefu, yeye na Selasini hatimaye wametubu kuwa yote wanayokwenda wakiyasema nchini ni unafiki mkubwa walionao vinywani, uzushi na uzandiki uliojaa kila aina ya ushetani midomoni mwao. “Nina kila sababu ya kukushukuru na kukupongeza Mheshimiwa Rais”, alisema Selasini na kuongeza kwamba endapo angekuwa na uwezo angeipa Barabara ya Mkuu – Tarakea “jina la Jakaya Kikwete” ili kuutambua, kuuthamini, kuuhesimu na kuuenzi uongozi wa serikali yake. Mbunge huyo alisema kuwa angefanya hivyo kutokana na ukweli kwamba barabara hiyo ilishindakana tangu utawala wa kikoloni, lakini imekuja kujengwa na Serikali ya Awamu ya Nne, tena baada ya Rais Kikwete kuahidi hivyo kiasi cha miaka miwili tu. Aidha, Mbowe naye alimsifu pia Rais Kikwete kwa kicheko chote alipozindua Barabara inayotoka Kwa Sadala kwenda Masama, akaipongeza Serikali akisema kwamba imefanya kazi kubwa na ya mafanikio kwa kujenga miundombinu ya barabara nchi nzima. “Huyu ndiye kiongozi wetu, ndiye mkuu wetu, mkuu wa nchi yetu na haijapata kutokea katika historia ya Tanzania. Mmefanya kazi kubwa sana katika kuiunganisha nchi yetu kwa mtandao mkubwa wa barabara. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais”, alibainisha mbunge huyo wa Hai, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema. Kama nilivyoainisha mwanzo, huo ndio ujuzi na utalaamu wa unafiki mkubwa walionao viongozi wa Chadema. Wamejaliwa vipaji vya hali ya juu wanavyoweza kuvitumia wakati wowote, mahali popote na kwa namna yoyote ile kuwapandikizia hasira na chuki wananchi ili kukidhi matakwa yao, lakini wanafanya hivyo wanapokwenda nje ya kwao. Hawataki wanapokuwa majimboni kwao waonekane waongo, wanafiki wala wazushi kwa kuhofia kukosa kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo wanalazimika kusema ukweli kwamba serikali ya CCM imefanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi, moja kati yake ni kujenga mtandao mkubwa wa barabara nchini kote kama alivyobainisha Mbowe. Wanakiri uongozi bora, umakini na uchapakazi mkubwa alionao Rais Kikwete na serikali yake, ile ambayo inajitahidi kutekeleza haraka ahadi inazotoa na kutamani apewe heshima zote anazostahili kama kumbukumbu ya kizazi kilichopo na vijavyo. Nani alitarajia kuwa Mbowe au Selasini wangetamka maneno hayo hadharani, tena ikiwa ni siku chache tu baada ya kutoka kuwapandikizia hasira, uchochezi na chuki wananchi dhidi ya CCM na serikali yake, kazi waliyokuwa wakiifanya usiku na mchana wakati wa kampeni za chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika nchini kote hivi karibuni? Mbali na hayo, vilevile niligusia unafiki mkubwa wa Chadema kuhusiana na suala zima la mgogoro wa kikazi uliokuwa ukimkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando ambaye hatimaye aliondolewa katika wadhifa huo, Jumatatu ya wiki iliyopita. Wakati aliposimamishwa na serikali ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, viongozi wa Chadema wakiwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wao, Zitto Kabwe walijitosa kumtetea sana wakidai kwamba alikuwa “ametolewa sadaka” au “mbuzi wa kafara”. Walifanya kila wanavyoweza ili kuwadanganya Watanzania eti kwamba serikali ya CCM inakumbatia uozo katika shirika hilo la umma, hivyo kwa vile Mhando alitaka kupambana nao kwa juhudi na maarifa yake yote akaundiwa tuhuma za kutunga ili hatimaye afukuzwe kazi. Walijaribu kufanya hivyo ili kuendeleza mfumo wao wa siku zote wa kufanya siasa za kitapeli, uzushi, uchochezi na ubaguzi unaolenga kuwagawa Watanzania katika misingi ya ukabila, ukanda na kutaka wakati wote waipinge serikali hata kama inatimiza wajibu wake kwa njia zote halali. Chadema iliyokuwa mstari wa mbele kumtetea kwa upotoshaji sana wakati huo ndiyo ileile iliyokuja kuwa ya kwanza kutaka ashtakiwe mahakamani. Imefanya hivyo kwa kutafuta umaarufu ili baadaye endapo atafunguliwa kesi ije iwadanganye watu kuwa imeilazimisha yenyewe serikali. Nasema huu ni unafiki kwa sababu haiwezekani mwanzo chama hicho kisimame kidete na kuwatangazia uongo wa makusudi wananchi, kikamtetea sana kuwa ametolewa sadaka au mbuzi wa kafara ili kuficha uozo wa serikali, lakini ilipokuja kuthibitika kuwa ana tuhuma za jinai kiwe cha kwanza kumnyoshea kidole. Chama cha siasa kinachokuwa na viongozi wanafiki wakubwa kiasi hicho, kisha siku zote kikawataka wapiga kura wakiamini ili wakiweke madarakani ni hatari. Kama vinavyosema vitabu vitukufu, mtu anaposhuhudia uovu wa aina yoyote ukitendeka mbele yake hana budi aukemee kwa ulimi wake mwenyewe. Kama hawezi kuukemea anapaswa auzuie kwa mikono yake mwenyewe, lakini kama hawezi pia kuuzuia kwa njia hiyo basi angalau aukasirikie tu. Hivyo ndivyo Watanzania wanavyopaswa kufanya dhidi ya viongozi wa Chadema. Inabidi angalau wauchukie uongo, uzushi na unafiki wao wote!
 
na sifa ya kutembea na mihuri ya wizara kwenye mahoteli ya Uswis kasahau eti?
na kugawa ubwabwa kwenye mikutano nayo kaisahau; huyu msahaulifu sana huyu...

View attachment 101480

du mpunga unalindwa huo! nahic kama mkutano wa CCM naona kuna njano na kijani hapo kwny milingoti. njaa ndo huwa inatuponza si mnakumbka igunga?
 
nakushauri kama unakuwa huna cha kuchangia kwenye uzi ni bora ukaacha mpaka utakapokuwa na chakuchangia.Ni ushauri tu lakini.
Huu ndio unafiki wenyewe, ww umeanzisha uzi na kubwa hapa umeuliza sifa za chadema, tulia acha kuweweseka tukupatie sifa halisi za hiki chama.
 
Huu ndio unafiki wenyewe, ww umeanzisha uzi na kubwa hapa umeuliza sifa za chadema, tulia acha kuweweseka tukupatie sifa halisi za hiki chama.
Charles .......vipi? UDC walikunyima mpaka leo ......tafakari kwani wanaona uwezo wako mdogo ndio maana hawakupi hata ukatibu kamili wa chama , unakuwa katibu msaidizi mpaka lini rafiki? Tukutane Rose garden jioni.......
 
asante sana kwa kuendelea kutufikirisha , bali cdm ndiyo yenye sifa hizo , ndani ya upande wa pili kuna makundi 6 .
 
Tuuchukieni uongo, uzushi na unafiki mkubwa wa Chadema


Tuuchukieni uongo, uzushi na unafiki mkubwa wa Chadema Na Charles Charles MBUNGE wa Rombo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Selasini aliusifia utendaji maridadi wa kazi unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete. Selasini alitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Mkuu – Tarakea wilayani humo, siku chache zilizopita na kuwashambulia hadharani wanasiasa ambao alisema wamezoea kudandia migongoni mwa wenzao. "Nina kila sababu ya kukushukuru na kukupongeza", alisema mbunge huyo na kuongeza kuwa kama angekuwa na uwezo angeipa barabara hiyo "jina la Jakaya Kikwete" kwa vile ndiye ametoa fedha zilizotumika katika ujenzi huo, ule uliotimiza ndoto ya miaka mingi ya wananchi wa Rombo. "Barabara hii imekuwa kwenye makabrasha tangu enzi za ukoloni, lakini Rais Kikwete ametimiza ndoto ya Warombo ya kuungana tena na wenzao kwa shughuli za kibiashara", alibainisha. Kesho yake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe naye alimsifu hadharani Rais Kikwete alipokwenda na kuzindua Barabara ya Kwa Sadala – Masama iliyopo katika jimbo hilo. Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Nne kwa kazi kubwa na yenye mafanikio ya kujenga miundombinu ya barabara nchini na kumuunga mkono Rais Kikwete binafsi na kuongeza: "Huyu ndiye kiongozi wetu, ndiye mkuu wetu, mkuu wa nchi yetu na haijapata kutokea katika historia ya Tanzania. Mmefanya kazi kubwa sana katika kuiunganisha nchi yetu kwa mtandao mkubwa wa barabara. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais". Wakati viongozi hao waandamizi wa Chadema wakisema hivyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa wa Chama hicho, John Mnyika alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akitaka aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), William Mhando ashtakiwe mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma. Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, amekuja na msimamo huo mpya wa Chadema miezi miwili tu baada ya Naibu Katibu Mkuu wake (Tanzania Bara), Zitto Kabwe aseme kuwa hatua zote zilizochukuliwa na serikali dhidi Mhando zilifanywa kinyume cha taratibu. Aidha, Zitto yuleyule ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea kwa nguvu zake zote kiongozi huyo wa zamani wa TANESCO akidai alikuwa amegeuzwa na serikali kuwa "mbuzi wa kafara". Hao ndio viongozi wa Chadema ambao ukimwondoa Selasini, watatu waliobaki wote wanapozungumza chochote ndio msimamo wa chama chao kwa vile ni Mwenyekiti wa Taifa, Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Taifa wa Habari na Uenezi. Nimeshangazwa na kauli zao mpya kutokana na ukweli kuwa wote katika ujumla wao ni mitambo inayotegemewa kuzalishia uongo, fitina, uzushi, uchochezi na umbeya unaolenga kuwapandikizia hasira na chuki Watanzania ili waichukie serikali inayotawala hivi sasa. Wote wamejitokeza kuwa mabingwa wa kuhamasisha uasi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wake, lakini kazi hiyo yote inafanywa kwa makusudi na malengo ya kutaka nchi isitawalike katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015. Mbowe na Selasini waliomsifu Rais Kikwete na serikali yake, wakampamba kwa vinywa vyao majukwaani, wakakiri ubora na utendaji wake maridhawa ndio walewale ambao walifanya uchochezi mkubwa na kuongoza maandamano ya vurugu, ghasia na uhalifu wa aina zote katika jiji la Arusha hapo Januari 5, mwaka jana. Walifanya hivyo wakishirikiana na viongozi wengine wa Chadema kama vile Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa; Wajumbe wa Kamati Kuu akina Philemon Ndesamburo, Godbless Lema, Grace Kiwelu, Peter Msigwa na kundi zima la wabunge walionao. Kutoka Arusha waliendeleza vurugu zao hizo katika mikoa mingine ikiwemo ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Iringa, Njombe na kadhalika ambako pia walikwenda wakitangaza kila aina ya uzushi, unafiki pamoja na uzandiki wote unaoweza kuwatoka midomoni mwao. Walikuwa wakitangaza kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo yoyote wananchi katika kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru uliopatikana Desemba 9, 1961, na kutaka mwaka 2015 wapewe madaraka hayo wao ili waiendeleze kwa kasi. Walisema Tanzania haina miundombinu ya barabara hasa za lami au changarawe, maji safi na salama ya kunywa huku pia ikizidi kurudi nyuma katika maendeleo mengine yakiwemo ya elimu. Kibaya zaidi walifikia mpaka kudai kuwa Serikali ya Awamu ya Nne ikiongozwa na Rais Kikwete yuleyule ndiyo "ziro zaidi". Waliwataka Watanzania bila ya kujali itikadi zao za kisiasa waitikie wito wao wa kutaka nchi isitawalike katika kipindi chake hiki cha pili, na pia wakamwambia yeye mwenyewe hatafika mwaka 2015. Wamekuwa wakipandikiza kila aina ya uasi, fitina, uzushi, hasira na chuki kwa rais huyo mwenyewe, CCM na serikali yake wakitaka wananchi wawaunge mkono na kumwondoa madarakani ikibidi hata kinyume cha katiba ya nchi! Wanatumia njia zote wanazodhani zinafaa, moja kati yake ni kile kinachoitwa ‘Operesheni Sangara' iliyokuja kuongezewa jina kuwa ni ‘Vuguvugu la Mabadiliko' au ‘Movement for Change (M4)', kazi ambayo siku zote imekuwa ikitumika kutengenezea uongo na fitina za kijinga. Pamoja na kusafiri kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara na kadhalika kwa kupita kwenye lami huku wakisinzia sehemu kubwa ya safari, viongozi wa Chadema wanapofika waendako husahau hayo yote utadhani kuku wa kisasa. Wanaanza kuzitukana barabara walizopita wakidai kuwa ni mbovu huku nyingi kati yake zimejaa mashimo na mabonde, zile ambazo utakuta wanadai wanalazimika kusafiri kutoka mwanzo hadi mwisho wakiwa wamefunga vioo vyote vya magari yao ili kukwepa vumbi. Hawasemi ukweli kwamba wanafunga madirisha yote ili kukwepa upepo kwa sababu zina lami na hivyo magari yao yanakwenda kasi zaidi. Hawataki kusema kwamba siku zote wanaamshwa wakiwa tayari wameshafika waendako na kubaki wanashangaa wamefikaje kwa haraka namna hiyo! Usingizi mzito wanaolala wakati wote wanapokuwa safarini, huwafanya wasione kwa uhakika namna gani barabara za nchi hii zilivyojengwa katika kiwango cha lami, hali inayosababisha waseme uongo wanapopanda majukwaani. Wanazungumzia hadithi za miaka mingi iliyopita walipokuwa wakisafiri kuelekea shuleni kama Mbowe aliyekuwa akitokea kwao Hai, Kilimanjaro au Dar es Salaam kwenda Shule ya Sekondari ya Kahororo, Bukoba. Anadhani hali bado iko vilevile kwa sababu akisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, au Singida anakuwa amelala kwa muda mwingi kwenye gari na kushindwa kuyaona maendeleo makubwa ya miundombinu ya barabara yaliyofanywa na serikali ya CCM. Ndiyo maana anapofika huko anaanza kuwadanganya wakulima na wafugaji ambao kwao wanapokwenda mbali sana ni kutoka vijijini mwao hadi makao makuu ya kata zao, tarafa zao, wilaya zao au mikoa yao ambapo kwa kawaida huwa siyo zaidi ya kilomita angalau 10 tu. Mwanasiasa mwandamizi kama Mbowe kwa mfano akitangaza kwamba ametokea Dar es Salaam hadi Iringa na kujionea ubovu wa barabara alimopita, akadai imejaa mashimo kila mahali, mabonde na majani utadhani ina mashamba hakika mwananchi anayeishi siku zote maeneo ya Kihesa, Ruaha, Kitwiru, Mtwivila, Mwangata, Mkwawa au Nduli inakuwa kazi rahisi mno kuuamini uongo huo na kwenda kuutangaza kwa majirani zake. Hivyo ndivyo wanavyofanya viongozi waandamizi wa Chadema akina Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Peter Msigwa, Godbless Lema, Vencent Nyerere, Grace Kiwelu, Joseph Mbilinyi au ‘Mr. Sugu' na kadhalika. Ndiyo maana pia miezi mitano tu iliyopita, Mbowe aliwaambia wananchi wa Lindi kuwa anakerwa na kushangazwa na miundombinu mibovu ya barabara nchini. Alisema hali hiyo haiwezi kurekebishwa hata iweje kama CCM itaendelea kutawala, hivyo akatangaza kwamba atazunguka kila kona akiwaomba wananchi wakiunge mkono chama chake ili mwaka 2015 kitawale na kusema anaamini wataelewa, kisha akaahidi kujiuzulu endapo watashindwa tena katika uchaguzi huo mkuu. Alisema kuwa atafanya hivyo kwa vile Watanzania watakuwa "wamemwambia kwamba wamezoea kuishi kwa taabu" bila ya barabara ambazo zimejengwa kwa lami. Atakuwa ameelewa kwamba "hawataki nchi yao ipate maendeleo" isipokuwa vinginevyo. Katika hali hiyo, Mbowe ambaye kuna wengine wanamwelezea kuwa ni rasta wa zamani ndipo akaahidi kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisiasa, nafasi ambayo itatoa fursa kwake ya kurudi upya kwenye shughuli za kasno la Billicanas Night Club kusimamia tena disko lake kama mwanzo. Lakini kwa vile uongo siku zote haudumu kwa muda mrefu, yeye na Selasini hatimaye wametubu kuwa yote wanayokwenda wakiyasema nchini ni unafiki mkubwa walionao vinywani, uzushi na uzandiki uliojaa kila aina ya ushetani midomoni mwao. "Nina kila sababu ya kukushukuru na kukupongeza Mheshimiwa Rais", alisema Selasini na kuongeza kwamba endapo angekuwa na uwezo angeipa Barabara ya Mkuu – Tarakea "jina la Jakaya Kikwete" ili kuutambua, kuuthamini, kuuhesimu na kuuenzi uongozi wa serikali yake. Mbunge huyo alisema kuwa angefanya hivyo kutokana na ukweli kwamba barabara hiyo ilishindakana tangu utawala wa kikoloni, lakini imekuja kujengwa na Serikali ya Awamu ya Nne, tena baada ya Rais Kikwete kuahidi hivyo kiasi cha miaka miwili tu. Aidha, Mbowe naye alimsifu pia Rais Kikwete kwa kicheko chote alipozindua Barabara inayotoka Kwa Sadala kwenda Masama, akaipongeza Serikali akisema kwamba imefanya kazi kubwa na ya mafanikio kwa kujenga miundombinu ya barabara nchi nzima. "Huyu ndiye kiongozi wetu, ndiye mkuu wetu, mkuu wa nchi yetu na haijapata kutokea katika historia ya Tanzania. Mmefanya kazi kubwa sana katika kuiunganisha nchi yetu kwa mtandao mkubwa wa barabara. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais", alibainisha mbunge huyo wa Hai, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema. Kama nilivyoainisha mwanzo, huo ndio ujuzi na utalaamu wa unafiki mkubwa walionao viongozi wa Chadema. Wamejaliwa vipaji vya hali ya juu wanavyoweza kuvitumia wakati wowote, mahali popote na kwa namna yoyote ile kuwapandikizia hasira na chuki wananchi ili kukidhi matakwa yao, lakini wanafanya hivyo wanapokwenda nje ya kwao. Hawataki wanapokuwa majimboni kwao waonekane waongo, wanafiki wala wazushi kwa kuhofia kukosa kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo wanalazimika kusema ukweli kwamba serikali ya CCM imefanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi, moja kati yake ni kujenga mtandao mkubwa wa barabara nchini kote kama alivyobainisha Mbowe. Wanakiri uongozi bora, umakini na uchapakazi mkubwa alionao Rais Kikwete na serikali yake, ile ambayo inajitahidi kutekeleza haraka ahadi inazotoa na kutamani apewe heshima zote anazostahili kama kumbukumbu ya kizazi kilichopo na vijavyo. Nani alitarajia kuwa Mbowe au Selasini wangetamka maneno hayo hadharani, tena ikiwa ni siku chache tu baada ya kutoka kuwapandikizia hasira, uchochezi na chuki wananchi dhidi ya CCM na serikali yake, kazi waliyokuwa wakiifanya usiku na mchana wakati wa kampeni za chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika nchini kote hivi karibuni? Mbali na hayo, vilevile niligusia unafiki mkubwa wa Chadema kuhusiana na suala zima la mgogoro wa kikazi uliokuwa ukimkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando ambaye hatimaye aliondolewa katika wadhifa huo, Jumatatu ya wiki iliyopita. Wakati aliposimamishwa na serikali ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, viongozi wa Chadema wakiwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wao, Zitto Kabwe walijitosa kumtetea sana wakidai kwamba alikuwa "ametolewa sadaka" au "mbuzi wa kafara". Walifanya kila wanavyoweza ili kuwadanganya Watanzania eti kwamba serikali ya CCM inakumbatia uozo katika shirika hilo la umma, hivyo kwa vile Mhando alitaka kupambana nao kwa juhudi na maarifa yake yote akaundiwa tuhuma za kutunga ili hatimaye afukuzwe kazi. Walijaribu kufanya hivyo ili kuendeleza mfumo wao wa siku zote wa kufanya siasa za kitapeli, uzushi, uchochezi na ubaguzi unaolenga kuwagawa Watanzania katika misingi ya ukabila, ukanda na kutaka wakati wote waipinge serikali hata kama inatimiza wajibu wake kwa njia zote halali. Chadema iliyokuwa mstari wa mbele kumtetea kwa upotoshaji sana wakati huo ndiyo ileile iliyokuja kuwa ya kwanza kutaka ashtakiwe mahakamani. Imefanya hivyo kwa kutafuta umaarufu ili baadaye endapo atafunguliwa kesi ije iwadanganye watu kuwa imeilazimisha yenyewe serikali. Nasema huu ni unafiki kwa sababu haiwezekani mwanzo chama hicho kisimame kidete na kuwatangazia uongo wa makusudi wananchi, kikamtetea sana kuwa ametolewa sadaka au mbuzi wa kafara ili kuficha uozo wa serikali, lakini ilipokuja kuthibitika kuwa ana tuhuma za jinai kiwe cha kwanza kumnyoshea kidole. Chama cha siasa kinachokuwa na viongozi wanafiki wakubwa kiasi hicho, kisha siku zote kikawataka wapiga kura wakiamini ili wakiweke madarakani ni hatari. Kama vinavyosema vitabu vitukufu, mtu anaposhuhudia uovu wa aina yoyote ukitendeka mbele yake hana budi aukemee kwa ulimi wake mwenyewe. Kama hawezi kuukemea anapaswa auzuie kwa mikono yake mwenyewe, lakini kama hawezi pia kuuzuia kwa njia hiyo basi angalau aukasirikie tu. Hivyo ndivyo Watanzania wanavyopaswa kufanya dhidi ya viongozi wa Chadema. Inabidi angalau wauchukie uongo, uzushi na unafiki wao wote!
Ufinyu wa Mawazo majukumu ya serikali yeyote ni pamoja na ujenzi wa barabara unadhani nani ajenge barabara? hizo kodi za wananchi ziende wapi?
 
Dalili ya chama kinachokufa/kuanguka;
1.kutoa motivation kwa wapiga kura kama, t-shirt, kanga/kitenge, kofia, ubwabwa n.k
2.kusafirisha kwa malori watu kwenda kwenye mikutano yake
3. Wanafunzi ni zaidi ya watu wazima kwenye mikutano
4.chama kugawanyika na kuwa na makundi
5.wizi na ufisadi kushamiri
6.wananchi wapata mateso zaidi,mfano kuuawa, kubambikiwa kesi, kuteswa, kudhulumiwa n.k bila serikali kujali
7. Serikali kutumia vyombo vya dola zaidi kudhibiti upinzani na raia

ndugu msomaji ongezea, halafu tuone kama kuna nchi hasa katika africa ambayo chama tawala imepitia stage hizo
 
Back
Top Bottom