Chadema igeni mfano huu

Chadema igeni mfano huu

Joined
Jan 9, 2014
Posts
7
Reaction score
2
Ndugu MAKAMANDA wa chadema na wa Tanzania wapenda mabadiliko ktk taifa hili,naomba muige mfano kutoka inchi maskini ya Zambia lakini yenye utajiri wa siasa safi.
Ikumbukwe kuwa toka Rais wa kwanza wa Zambia Dr,Keneth Kaunda kuondoka madarakani na chama chake kumfia mkononi,Kilikuja chama cha MMD,kikafa na sasa ni PF chini ya Raisi Michael Sata.
Michael sata kabla hajashinda urais na chama chake kuingia madarakani alisha jaribu mara tatu na kushindwa.
Wafuasi wake baadhi waliotaka madaraka hakuwaamini,na hakika angewaachia chama kingefia njiani kwani hawakujua uchungu na dhahama ambazo zilimkumba akiwa anatengeneza chama.

Wanachama wote baada ya kuona hataki kuondoka madarakani,walimuelewa na kuamua kukuzana kukijenga chama kwa maslahi ya nchi.Leo hii tukimuondoa mh, MBOWE na Dr SLAA Chama kitakufa ndani ya mwaka tu.Kinachotakiwa ni kukijenga chama ili kiingie madarakani baada ya hapo faida yenu na kwa vizazi vyenu mtaipata.

Niko Ziarani Zambia nafanya utafiti zaidi hawa wenzetu wanafanyaje mpaka wanaondoa vyama kandamizi kirahisi
nikirudi nitawajuza.:clap2::clap2:
 
Rais 2015 ni Dr W.P.Slaa!

Hamtaki mnaachaaaaaa!
 
Yaan post zote zilizotumwa leo zote ni chadema tu si mjadili ht tembo wetu wanapotea? Chadema itazid kusonga mbele tu
 
Suala sio ushabiki wa majina tauangalie kwa sasa tunaitaka Tanzania gani? Tuangalie ni nani atatufikisha pale tunapohitaji kufika.
 
labda raisi wa karatu.raisi wetu watanzania wapenda amani ni edward lowassa

Hivi hizi kauli za ubaguzi unazitoa wapi! undhani Lowasa kura za raia wa Monduli peke yake zitatoshakumfanya ashinde Urais?. Tunatakiwa kuongea hoja kama mtu hafai au nafaaa kuwa Rais kwa sababau zipi! Tuache kubaguana undhani ubaguzi wako utakufikisha wapi, jaribu kuwa unafikiria ukiwa unachangia hoja.
 
Back
Top Bottom