chadema hili turekebishe!!

mimi sioni tatizo la nyimbo za dini kupwa kwenye mikutano ya chadema, labda kama kuna jingine. au unataka nyimbo za mapenzi?

Tatizo sio wewe mtu mmoja, ni wale ambao wanakuwa uncomfortable ambao ni wengi kuliko wewe.
 
Ebu weka clip tuone kama unatoa toka moyoni hayo malalamiko au ndio walewale.

jamaa ana malalamiko ambayo ni guneine,hamna sababu ya kum 'attack' kama hilo lipo basi lifanyiwe kazi maana hii ndo feedback kutoka kwa wanachama.
 
Kwani hili ndo unalijua leo?Hicho ni chama cha kanisa si chama cha siasa,Hukuona kampeni za Arumeru mgombea wao alivyokuwa anaombewa kwenye majukwaa,nawahurumia ambao hawalijui hilo.
 
True magamba at work!!. Nimekuwa nikuhudhuria mikutano karibia yote, ukiacha ule wa msiba wa makanda wetu ambao zilipigwa nyimbo za dini zote na hasa zile maarufu za kupigania ukombozi za kule south, sijasikia nyimbo hizi katika mikutano mingine isikuwa na misiba nyimbo hizo zikipigwa. Hata hao waislam mnaojitahidi kuwashawishi wasikipende chadema wameshawashtukia na mtaona majimbo yote ya pwani na zanzibar yatakuwa na wagombea makini kutoka huko next game!!.
 
Kwani hapo hicho na chama au watu wa PA? Sijakupata vizuri
 
Jamani wana jamvi, constructive criticism kama ya huyu jamaa aliyeanzisha huu uzi tuwe tunakubali jamani. We should not discard every idea started here. We are human beings, therefore we are not perfect by 100 p.c.

A riot is the language of the unheard.
Martin Luther King, Jr.

 

kama hili limetokea hata mimi naunga hoja mkono kwa asilimia 200. CHADEMA kitafute nyimbo maalumu za kutumika katiba mikutano ya chama. Tena ziwe ni nyimbo za kutukuza utanzania na kupigia haki kwa kila mtanzania.
 
Dah!
Mkuu Axe ahsante kwa angalizo lako, ila maadamu umejitambulisha kama ni mwanachama basi kuna vitu ungeviboresha katika angalizo lako, kwa mfano ni mikutano gani na zaidi labda ni nyimbo zipi hizo hasa (ikumbukwe kuwa kwaya ni aina ya uimbaji tu hivyo sio kwaya zote ni injili ya yesu)!

Kwanini nasema hvyo, ni wazi kuwa watu wengi hapa jamvini tunahudhuria shughuli tofauti za CDM sasa kama ukieleza kitu bila kufafanua hasa tukio mahsusi ni rahisi kwa wengine wetu kuitilia shaka dhamira yako na inawezekana ikaonekana kama unapotosha!

Je ni mikutano yote? Au huo mmoja tu? Upi??

Binafsi nilikuwepo Arusha siku ya mkesha wa kushinikiza Lema aachiwe na mikutano mingine mingi ila ntaeleza huo sababu ni mkutano uliokuwa mrefu sana hivyo kama hyo shutuma ya nyimbo za injili ya yesu, kama huwa zinapigwa makusudi (kitu ambacho unajaribu kutuonyesha hapa kwa makusudi au bahati mbaya).

Basi siku ile ya mkesha zingepigwa zote za store, ila najaribu kukumbuka hapa sikumbuki kusikia pambio wala nyimbo yoyote ya injili ya yesu ila nakumbuka MC aliwataka watu wanapoenda makwao kuchukua mashuka basi waje na CD zenye nyimbo za harakati na kushawishi mabadiliko ya watu, watu walileta CD za Bob Marley, 2pac, ROMA, Lucky Dube na wengine kibao wa namna hiyo!

Naomba nikumbushwe kama kuna pambio za injili ya yesu zilipigwa siku ile!

Ndio maana nkakutaka ufafanuzi zaidi, kama katika mikutano michache wengine tuliyoshiriki hatujaona unachosema,
Je!? unatoa nafasi ya bahati mbaya kutokana na namna ya upatikanaji wa music na dj??

Kama ndio mbona hujaweka ufafanuzi huo kwenye thread yako??

Tuwe makini kwenye aina ya kukosoa kwa wapendwa wetu, wakati mwingine unaweza ukamjeruhi na kumuumiza badala ya kuokoa,

msiikadilie kwa chini nguvu ya JF!!

Bandiko lako ambalo lina mapungufu ya msingi sana linaweza kutumika kama silaha kwa chama chako!

Pia unaweza kuulizwa kama we ni mwanachama hai umelifikisha wapi katika ngazi stahiki za chama?
 
Last edited by a moderator:
..inawezekana hizo nyimbo za "kidini" ni jitihada za CDM kuonyesha kwamba wao ni chama cha AMANI. LOL!!

..kitu kingine nawaomba wa-Tanzania tujifunze kusikiliza "ujumbe" na siyo kukwazika tu kwasababu mtoa mada ni wa imani tofauti na yako.

..kuna kipindi Sheikh Mkuu, Mufti Hemed Bin Jumaa Bin Hemed alikuwa na wasikilizaji[mawaidha ya kiislamu ijumaa] wengi sana hata wa imani tofauti na yake kwasababu watu walivutiwa na "ujumbe" mzima ktk mazungumzo yake na siyo kum-dismiss moja kwa moja kutokana na imani yake.


NB:

..mimi napenda vionjo vya reggae ktk mikutano ya Arusha.
 
Sijawahi kuhudhuria mikutano ya Chadema kumbe huwa wanapiga Kwaya!

unashangaa cdm kupiga kwaya unaacha kushangaa ccm wamekuwa wakitumia kwaya ya john komba tokea enzi hizooo, au hujui maana ya kwaya weye?
 
si busara kupinga kila kitu kinachozungumzwa humu kwenye jf na si busara kukubaliana na kila kitu kinachaletwa hapa jf, kama uliyoyasema ni sahihi cdm kuna haja ya kurekebisha haya ili kuleta picha ya utaifa zaidi.
 
unachoongea ni kweli kama unaipenda CDM UTAIKOSOA NA KUIONESHA NJIA KAMA MKUU ALIYE ANZISHA UZI HUU, LAKINI MWINGNE BILA HATA CHEMBE YA UKUFIKIRIA ANAKURUPUKA NA HOJA KURUPUSHI NA MANENO REJAREJA NA KASHIFA HARAFU ANASEMA NANAKIPENDA CHAMA KAMA UNAKIPENDA CHAMA UTAKIRINDA. SIO UPENDO WA KINAFIKI USIO NA TIJA NA WAKUTUPWA. CHADEMA CHAMA CHANGU SIWEZ KUKAA KIMXA KINAPO HARIBU. CDM FOR HARAKATI.
 
hiyo ni kweli viongoz fanyien kaz!
Mimi ni mkristo lakn sikufurahia hata maombi yaliotolewa wakat WA kampen kumnad nassar Kwan mwombaj aliomba katka jina la yesu na stahili za kukemea mapepo za kilokole! 4 shure haipendez hiz ni kasoro tulekebishe!
 
Kaka hapo bado hujasema kitu zipo nyimbo nyingi tu zenye ujumbe unaoweza kufananisha na tukio hilo lakini kwa nini watumie wa dini?Usipeleke wazo hili pembeni suala linalojadiliwa ni kutumiwa nyimbo za dini kwenye mikutanao kumbe unathibitisha hadi kwenye Cd zimo?Kaka hapo hakuna njia nyingine zaidi ya kuacha kutumia hizo nyimbo.Usifafanue jambo ambalo uhalisia wake unajulikana
 
Reactions: Axe
Kuna kitu kimejificha! but i,m sure very soon mbichi na mbivu itajulikana.But what is interesting is how they can stop play gospal while SLAA ni Padri aliyekiuka maadili
 
Nunua cd za mikutano iliyofanyika recently utapata majibu yote!lakini haya mambo yanahitaji marekebisho kidogo,natumaini viongozi wetu wamesikia,lakini kikubwa tunachohitaji ni ukombozi ili tuondokane na hili gari bovu lenye miaka hamsini haiwezi kutufikisha safari tunayotaka kwenda cause it's way far!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…