CHADEMA...hii trend sio

Viongozi wa Chadema mliopo hapa jamvini Songoka amesema kweli tupu. Imefika mahali sasa mfanye vema kwa upande wa akina mama. Wabunge wenu wanawake wako passive sana. Pia BAWACHA tunasikia ipo ila it is also passive. Wekeni mwanamke shupavu pale ambaye hawezi kununulika na UWT na baba yao. Kipeni kitengo fungu ili kianze kazi mara moja kabisa. Vinginevyo 2015 si mbali!!! Mambo yote yafanyike 2014. Songoka asante sana kwa kuliona hili. Sincerely presented here for immediate action!!! Power to you, CDM.
 

mkuu[MENTION]bundimkubwa[/MENTION] kila siku vijana wanafikisha miaka 18 na kina mama ni nguzo muhimu sana katika kuwajenga vijana hawa kisiasa kama chadema watawatumia katika hili, hasa katika ngazi za familia
 

naunga mkono hoja yako mkuu
 

Hapa ndo chama kina fail..huwezi kusema unataka kuongoza nchi yenye watu wa jinsia zote tena wanawake wakiwa wengi kuliko wanaume, na takwimu zikionyesha kuwa wanawake wanapiga kula kwa wingi kuliko wanaume alafu unadanganyika na wanaume wanao hudhuria mikutano. Wanaume ni waongo sana mfano mzuri ni ZITTO ZUBERI KABWE..watu kama zitto ni wengi sana katika mikutano ya chadema...chadema you need to invest on WOMEN

salam kwa [MENTION]Dr. Slaa[/MENTION]
 
Mleta mada ni mbumbumbu wa siasa za chadema....nakukumbusha kidogo tu

mwaka jana katika mlipuko wa bomu uliotokea soweto...mmoja wa makamanda aliyeaga dunia alikuwa ni mwanamke!

Usiifananishe chadema na vilaza TANU bana...
 
Mleta mada ni mbumbumbu wa siasa za chadema....nakukumbusha kidogo tu

mwaka jana katika mlipuko wa bomu uliotokea soweto...mmoja wa makamanda aliyeaga dunia alikuwa ni mwanamke!

Usiifananishe chadema na vilaza TANU bana...

umekurupuka, tena umekurupuka sana....tunaongelea uwiano wa wafuasi wa chadema. Kwani ALIMA Mdee sio mwanamke?? tunajua. na hata uyo aliyekufa alikua kiongozi wa chama. SWALI ni je walikuepo wanawake wangapi? Je chama kina wafuasi wanawake wa ngapi? Je chama kina juhudi gani kuongeza wanawakendani ya chama? je chama kina ideology gani towards women??

Nna shaka na elimu yako.....kama umeshindwa kuelewa mada lahisi kama hii...itakuaje hesabu za matrix
 
Josephine alipigwa kwa ajili ya kiherehere chake, huwezi kuwatukana Polisi eti kisa wewe ni Mchumba wa Katibu Mkuu wa Chadema, halafu wakakuacha hivi hivi.

Heshimu sana mdomo wako maana ,maneno yako ndiyo shimo lako.
siku yaja na si mbali maneno ya vinywa vyenu yatawahukumu.

asanteni sana kwa maneno yenu ya dhihaka za namna zote.Ndiyo yanayotupa afya.

ashukuriwe aliye tuumba na kutufanya tuishi mpaka leo,kwani yeye anaijua kesho yetu ndiyo maana anatupa afya na nguvu nyingi za kuishi kwa uvumilivu.
 

Waonye kwanza misukule wenu wanaoshinda mtandaoni kutukana raia wema.
 
Ni kweli kuna umuhimu kwa viongozi wakuu wa CDM kuongeza nguvu katika kujenga jumuiya ya kina mama wa cdm.

Sina shaka wanawake wengi wanaunga mkono cdm na watakipigia kura, ila wanaogopa kuhudhuria mikutano. Wanadhani ni ya mapigano na polisi. Na tukumbuke watu wanakwenda na combat huko.

Ila tusisubiri Slaa na Mbowe wafanye kila kitu. Viongozi wa cdm matawini waanzishe vikundi vya kina mama.
 
vyovyote iwavyo ukombozi upo njiani. kwa taarifa yako ni kuwa akina mama wapo underground, wao watafanya maziko ya ccm kwenye sanduku tu, baada ya hapo ndo utaona uimara wao.
 

Unalalamika nini??fanya jitihada za kuhamasisha wanawake CHADEMA si kulia lia tuu hapa...unatake kuonewa huruma??????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…