Chadema!,hii ni provocative politics ,tunawaona!

Chadema!,hii ni provocative politics ,tunawaona!

Jibu au hoja yako ni hoja za kichadema zaidi yaani chonganishi na wewe ni mmoja wa niliowataja kwenye topic yangu.
Nyinyi ndio aina ya wapiga deal makazini niliowataja pia.
Eti wapiga deal makazini...ni wazi kuwa wewe mwenyewe utakuwa ni piga deal tu, na unachokifanya hapa ni kama jamaa zako akina Musiba, mmegundua upigaji deal wa awamu ya tano...kusifia! Nchi imeelekezwa kibra nyie mnapiga mapambio! Hovyo kabisa...
 
Hahaha! Hii Nchi Ina Vituko Sana. Yaani Ni Usanii Usanii Tu!

Mtu Anakwambia Anapambana Na Ufisadi Wakati Kuna Mafisadi Yanadunda Tu Mpaka Leo Tena Mengine Yapo Ndani Ya Chama Chake. Kwenye Masakata Mbalimbali Ya Ufisadi Wapo Waliopiga Hela Na Bado Wapo Uraiani. Vipi Kuhusu Zile Tuhuma Za Nyumba Za Serikali?

Swala La Vyeti Feki Ni Double Standard. Mfano Tu, Kuna Mmoja Wao Alikingiwa Kifua Akaambiwa 'Chapa Kazi' Pamoja Na Kuwa Alikuwa Na Tuhuma Za Vyeti Feki.

Tukija Swala La Rushwa Ni Kiini Macho. Mfano, Kuna Mmoja Alinaswa Hadi Na Kamera Akishawishi Mtu Kupokea Rushwa, Watu Wakategemea Atachukuliwa Hatua Za Kisheria Au Kuchunguzwa Lakini Kilichotokea Alipandishwa Na Cheo.

Na Mengine Mengi Ni Kizungumkuti Mfano Hilo La Makinikia Pia Shirika La ATCL Bado Halijaweza Kujiendesha Kwa Faida Bali Kilichofanyika Ni Manunuzi Ya Ndege.

Siku Hizi Hata Mafisadi Nao Wamekuja Na Gia Ya Kujifanya Kupambana Na Ufisadi Kumbe Wao Nao Wamo Humo.

Watanzania Kitakacholiponya Taifa Ni Elimu. Elimu Ndio Msingi Katika Kila Jambo, Ujinga Hautalisaidia Taifa Bali Utaliangamiza.


ELIMU!!!
Mleta mada amesahau kuwa wakoloni walikua wanauwezo makubwa sana wa kufanya Tanganyika iwe kama Uholanzi kimiundo mbinu, kudhibiti ufisadi, kuzuia vyeti feki, kuzuia Rushwa, kuzuia watanyakazi hewa, nidhamu kazini , Elimu bora n.k .
Pamoja na yote hayo lakini Wakoloni walituliwa mbali na mabavu yao yote.

Wakoloni wazungu waliondoka sasa wameibuka wakoloni weusi wanyonyaji wasio na maono ,waliojawa na umaskini kwenye familia zao wanataka kutimia kodi za wanyonge kutajirika huku wakiwa hawalipi kodi kwenye mishahara yao. Wanatumia nguvu kubwa kupata madaraka , wamebaki kusingizia nchi za magajaribi utafikiri nchi za magharibi ndio zinatoa Elimu duni ya Darasa la kwanza mpaka la saba au Wakoloni ndio wanaoiba mitihani au utafikiri wakoloni ndio wanaweka double standard kwenye kanuni za mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo wanaotumika muda mfupi kama wanasiasa wanapewa pesa zao zote kwa wakati mmoja na wanaotumika muda mrefu kwa mishahara midogo wanapewa 25%.
Eti mabeberu wa Magharibi ndio wanyonyaji; kwani wao ndio waliotoa mishahara midogo kwa watumishi wa umma na kuwalipa mishahara mikubwa wanasiasa na wateule wasiozalisha chochote zaidi ya kupotezea watu muda na mikutano ya kuuza sura tu.?

Utawadanga watu wasiofuatilia bunge lakini bado Wapinzani wanaibua hoja zenye mashiko kuliko wale wanaosifia binadamu wenzao muda wote mpaka wengine wanawaona kama miungu wakati wanafanya makosa.

Rushwa ipo mana tunaona jinsi pesa za umma zinavyotumika vibaya kwa Sababu tu ya kusifia. Tunaona misafara ya mawaziri,wakuu wa mikoa ,wakuu wa wilaya ikiwa mikubwa sana kuliko wakati wowote tangu kuumbea kwa dunia.

Hakuna binafamu asiyepigania tumbo lake. Ufisadi mkubwa unaofanywa na watawala kwenye nchi za kijamaa zinalenga kuimarisha vyama vilivyoko madarakani ili kizidi kuwapa kura na kula milele.

Siku watakapokuja kutawala wengine mdipo mawe yote yatafukukuliwa na kuonekana ufisadi wote unaojificha nyuma ya miradi ya kichina.

Watawala wanakazi yao basi wafanye majukumu yao bila kuathiri majukumi ya wapinzani ya kukosoa. Vinginevyo tutaamini kuwa kuna kinachofichwa nyuma ya pazia.
 
Wazee Wa Kusifia Sifia Wanapojiona Wao Ndio Wazalendo Kuliko Wengine.

Ngoja Niwaambie Kitu;
Uzalendo Wa Kweli Ni Pamoja Na Kuikosoa Serikali Inapofanya Makosa. Ni Kusimama Na Nchi Na Sio Serikali Au Rais Na Chama Chake!

"Loyalty To The Country ALWAYS, Loyalty To The Government When It Deserves It" - Mark Twain
Hakuna cha uzalendo hapo Bali ni kila mtu kutetea maslahi yake.

Mzalendo ni yupi kati ya mtu anayelipwa mshahara laki 4 huku akiwa anakatwa kodi au yule anayelipwa mil 7 bila kukatwa kodi ya maendeleo??
Wanahubiri maendeleo gani wakati hawayachangii??
 
H
Siasa za Tanzania zimetawaliwa na hila,vituko na tamaa binafsi zaidi ya siasa halisi. (Hususan kipindi hiki cha awamu ya tano).

Mfano halisi;

Ikumbukwe kuwa kabla ya awamu ya tano ya uongozi wa JPM, kelele na gumzo kubwa nchi hii ilikuwa ni mambo yafuatayo.

*Ufisadi na ubadhirifuwa raslimali na fedha za nchi hii.
*Elimu duni na miundombinu yake.
*Ukosefu wa uwajibikaji na rushwa katika sekta ya umma.
*Ubinafsishaji holela na usiozingatia vigezo, wa viwanda na taasisi mbalimbali za nchi hii.

Hoja yangu:
Haya mambo yaliwakera wananchi kwa kiwango cha juu na hii kuwapa fursa wanasiasa wa upinzani wakionozwa na chadema na cuf kujizolea wingi wa wafuasi nchini kwa hoja na kashfa mbalimbali walizokuwa wakiziibuwa ndani na nje ya bunge.

Walituaminisha watanzania kwamba wao wana nia safi ya kulikwamua taifa katika shimo lililokuwa mbele yetu kama nilivyoainisha hapo awali.kwanba wao walikuwa na nia madhubuti kukomesha Ufisadi, rushwa na mengineyo maovu yote ikiwemo escrow na iptl ,saga ambazo ziliibeba chadema hadi ilipo sasa.

Kabla na baada ya uchaguzi.

Mambo yalianza siku kadhaa kabla ya uchaguzi,
Wale walioyumbisha nchi hii, kwa kuunda mitandao ya kusaka uongozi(baada ya kukosa nafasi kule ccm).kwa mbinu zilezile zilizowanyima nafasi huko, wakitumia ukwasi wao walipora nafasi za uongozi asubuhi sana huku chadema na kuwatupilia mbali waasisi wa harakati halisi za kupinga ufisadi na huku wakimuaminisha mwenyekiti mbowe kuwa na mafuriko ya wapiga kura,almaarufu gia ya angani.

Baada ya CCM kushinda na JPM kuchaguliwa Rais wa awamu ya tano. Akaanza kazi siku ya pili, hadi leo sitaki kurefusha stori maana yote yako wazi.
*MAKINIKIA.×
*MISHAHARA HEWA.×
*IPTL.×
*MADAWATI.
*MAABARA.
*UFISADI.×
*BANDARI.
*VYETI BANDIA.×
*SAFARI ZISIZO TIJA NJE. ×
*MIKUTANO YA BODI ZA MASHIRIKA NJE YA NCHI.×
*ATCL MPYA.
*RELI MPYA.
*NDEGE MPYA.
*UWAJIBIKAJI SEKTA YA UMMA.
nk,nk,nk.....

Mshangao na ajabu kwa watanzania.

Sasa tunaona siasa za ajabu sana katika huu unaoitwa upinzani.
Sasa sera sio ufisadi tena wala ubadhirifu wa mali za umma,la khasha! ni dhahiri kwamba ujio wa wale mapapa ndani ya CDM umelazimisha chama kubadilika toka upigaji vita hadi utetezi wa wabadhilifu,mafisadi na mabeberu wa nchi za nje kwa mgongo wa uwekezaji wa kinyonyaji kama acacia nk.
Huku sasa sera ikiwa ni uminywaji wa demokrasia nchini.(na hii gaikuwahi kuwa kero ya wapiga kura wa nchi hii.)

Sasa magufuli hakika anapambana na sura halisi iliyokuwa imejificha ya mtandao wa kifisadi toka makundi mbalimbali yaliyokuwa yakiishi kinafiki huku wakitunyonya watanzania.

*Mh Magufuli anapambana wafanyabiashara mangimeza .

*Mh Magufuli anapambana na wanasiasa mamluki waliokuwa kwenye siasa kwa maslahi binafsi.

*Mh Magufuli anapambana na kundi kubwa la wadanyakazi waliokuwa wamezowea kuishi kwa kukumbatia rushwa na ubadhirifu katika nchi hii.

*Mh Magufuli anapambana na mafisadi halisi waliolazimika aidha kukimbia nje ya nchi kutokana na mianya takriban yote kuzibwa,lakini wakitafuta namna ya kurudi na ikiwezekana kuendelea kutunyonya kama awali.

*Lakini pia mh Magufuli anapambana na kundi kubwa la watumbuliwa majipu toka nyanja mbalimbali nchini wenye nia ovu ya ulipizaji kisasi.

Matokeo yake!
Sasa tunaona watu woote toka makundi haya wakiungana na kusahau tofauti na aina ya dhambi zao na kuweka nia moja tu ya kumkwamisha Mh rais wetu JPM, lakini kila kundi likiwa na malengo yake ila nia moja.

Provocative politics.

Baada ya kuona muelekeo sahihi wa Mh magufuli kwenda 2020, huku wananchi wakimuunga mkono,sasa wamejiunga na kuweka mikakati ya uchokozi na propaganda chafu wakisaidiwa na mabeberu huko nje na majarida yao, pamoja na taasisi zao za kinyonyaji wakijaribu kututishia misaada yao nk.
Hapa nchini wanasiasa hawa wamejitwisha uwakili wa ufisadi huku ntakutumia mbinu kadhaa za kutoa matamko, matusi,kejeli, vijembe na hata kutotii amri halali za kisheria na kimahakama ili kutafuta kutiwa nguvuni au lugha nyepesi kukamatwa na vyombo vya dola ili kupata pa kuanzia ili kumvuruga Mh rais atoke kwenye mstari wa kutekeleza ilani yake ya ahadi ya kuwaletea wananchi na taifa kwa ujumla maendeleo .

wana mikakati mingi,Na huenda pia wako hata ndani ya chama na serikali,maana maisha waliyozowea kuishi wao na familia na vimada wao hayapo tena.

Ni vema serikali iwe makini nao mapema na si wakati wa mzaha.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Naomba kuwakilsha.
Hizi siasa za namna hii waachie kina Kibajaji na Zitto. Tumeshazichoka kabisa mkuu. Hakuna mabadiliko yeyote kwa maisha ya kawaida ya Mtanzania miaka mitatu tangu aingie madarakani. Tuanzie na hapo kwanza usituletee mambo ya safari za nje kupungua wala kuongezeka. Watu bado wanalia njaa
 
Jibu au hoja yako ni hoja za kichadema zaidi yaani chonganishi na wewe ni mmoja wa niliowataja kwenye topic yangu.
Nyinyi ndio aina ya wapiga deal makazini niliowataja pia.

Unaweza kunitajia taasisi tano ambazo zilikua zinapigiwa kelele kwa rushwa kutokana na uwazi lakini sasa kuna uwazi lakini Rushwa haipo na wananchi wao huru kuzitaja taasisi zenye rushwa?
 
Hakuna cha uzalendo hapo Bali ni kila mtu kutetea maslahi yake.

Mzalendo ni yupi kati ya mtu anayelipwa mshahara laki 4 huku akiwa anakatwa kodi au yule anayelipwa mil 7 bila kukatwa kodi ya maendeleo??
Wanahubiri maendeleo gani wakati hawayachangii??
Chukua bia moja hapo ndugu yamgu kwa Gharama yako lakini si unajua hali ilivyo.

Umesema kweli kabisa nimechoka na hawa Nyumbu wa kijani kila kukicha wanaleta masifa yasiyo na mshiko. Sijaona tofauti ya Nyumbu UKAWA na Nyumbu CCM. Watanzania tunatakiwa kubadilika tusichague mizigo ya ndiyo mzee kama kina Kibajaji hata na huko UKAWA. Tuchague watu watakaotupigania maslahi yetu. Kuna watu wazuri huko UKAWA na CCM wakirudi 2020 tuwaulize kama wanakwenda kule DODOMA kutetea vyama ama kututetea sisi. Tusipeleke watu kwasababu tu ya Itikadi tupeleke watu wanaomuogopa Mungu kwa maana wataenda kututetea na siyo kwenda kuwa mizigo.
 
Back
Top Bottom