CHADEMA hawakujiandaa kwa kampeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA hawakujiandaa kwa kampeni?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tuko, Sep 6, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli inasikitisha sana hasa kwa sisi wapenda mabadiliko na wafuasi wa CHADEMA kuona haya mapungufu ya wazi katika kampeni za CHADEMA.

  Ukizunguka maeneo mengi Tanzania, mijini na vijijini, hakuna mabango ya mgombea uraisi wa CHADEMA!!!!. Sijui sababu ni nini lakini nadhani CHADEMA kama chama makini walitakiwa wajiandae mapema angalau katika hili suala la mabango. Najua kampeni inahusisha mambo mengi lakini hili la mabango ni muhimu na lilitakiwa kupewa kipaumbele.

  CHADEMA wasibweteke kwa kudhani kuwa mgombea wao anajulikana na kila mtu... mbona KIKWETE anajulikana lakini kila unakopita mabango yake yamejaa! Na ukweli ni kwamba bado ni asilimia kubwa tu ya watanzania ukiwauliza mgombea uraisi mwingine zaidi ya Kikwete anashindwa kutaja au inamchukua muda fulani kufikiria (na hii ni mijini na zaidi vijijini). Kwa hiyo kama kuna watu wanahusika hili suala naomba wajitahidi, NI AIBU...
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kampeni inahitaji fedha na sio pesa!Chadema wana pesa lakini hawana fedha!
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Very sad... :lying:
   
 4. N

  Nataka Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu makini hawahitaji pesa kuwa makini na umakini haimanishi unapesa au hauna pesa, masikini makini ni bora kuliko tajili fisadi mwenye mabango
   
 5. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  TUKTunapotoa maoni yetu ni vyema tukafanya na utafiti kidogo. CCM licha ya kupata Bil 2 kama ruzuku kila mwezi. mabango yao yametengenezwa ka gharama za Serikali, sasa CHADEMA yenye kupata Mil 61 tu kwa mwezi inepata wapi hizo pesa?

  Tatizo la Tanzania ni moyo wa uzalendo miongoni mwa wananchi kuuawa kabisa kutokana na na matendo mabaya viongozi wa CCM wanayowatendea wananchi; hali hii imepelekea wananchi kukata tamaa ya kuchangia chochote, sijui wewe.

  Sijui mwanaJF TUKO umeshachangia CHADEMA shilingi ngapi mpaka sasa. Ni kutokana na kutambua athari za wananchi kuchangia vyama vya upinzani ndio maana Serikali ya CCM huwaandama watu wanaojitoikeza kuchagngia vyama vya upinzani kwa nia ya kuvidhoofisha.

  Hivyo katika mazingira haya ni lazima tupongeze hicho kidogo kilichopo na tukaze buti kuelimisha wapiga kura ushindi utapatikana tuu, kwani dhambi ya ufisadi haiwezi kusafishwa na picha na mabango.
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Naelewa hali halisi ya kifedha kwa chama kama CHADEMA. Hata hivyo najua kuwa wamekuwa wakifanya jitihada katika kufanya mambo ya muhimu kama mikutano ya kampeni na ya kawaida. Hoja yangu ilitokana na ukweli kuwa suala la mabango naliona kuwa la muhimu sana sawa na ilivyo kwa mikutano ya kampeni.

  Binafsi sijachangia CHADEMA taifa (hasa baada ya njia ya SMS kuhujumiwa), lakini nashukuru kuwa nafanya kazi kwa karibu na mgombea ubunge huku na michango yangu ya HALI na MALI nailekeza katika hili...
   
 7. Zungu la Unga

  Zungu la Unga Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini wao si wana helikopta ya kusombea kura vijijini? Kwi kwi kwi!

  Mnazungumzia chama ambacho mpaka miezi miwili iliyopita kilikuwa hakijui kama kitamsimamisha mtu kwenye nafasi ya Urais ama la, halafu kikakurupuka kuweka mgombea siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu. Hicho ndiyo mnaita CHAMA MAKINI?

  Jamani kura hazipigwi kwenye Internet forums. Na msidhani kila mkibandika habari za uongo na kupiga kelele nyingi ndiyo kura za Chadema zitaongezeka. Hilo mlisahau!

  Chama mbadala ni kimoja tu ila kwa sababu za udini wenu mlikipiga vita sana wakati ule mlipokuwa mmeshika upini ndani ya CCM. Na sasa mnaona aibu kujiunga nacho!
   
 8. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  [kusema ukweli hata mimi nakuunga mkono lakini ukweli ni kwamba ilitakiwa angalau hata picha za size ya A4 zingepelekwa vijijini, nadhani hii ingesaidia sana kwa wananchi wa huko kupata hamasa.
   
 9. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,477
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  mabango kama dar yanachanwa na vibaraka je huko vijijini itakuwaje?
   
Loading...