CHADEMA: Hatuchukui tena makapi toka CCM

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Dr. Slaa katibu mkuu wa CHADEMA Taifa amesema kuanzia ngazi ya Udiwani hawatachukua wanaoachwa na CCM kugombea ndani ya CHADEMA.
Source Mwananchi gazeti la leo.
=======================

slaa.jpg

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akizungumza waandishi wa gazeti la Mwananchi katika mahojiano maalumu ofisini kwake Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitasubiri wanachama watakaoachwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uteuzi wa wagombea katika uchaguzi mkuu ujao.

Kutokana na tamaa ya kuingiza watu wengi kwenye Bunge, vyama vya upinzani vimekuwa na tabia ya kuwapokea wanachama wa CCM wanaoshindwa kwenye kura za maoni na baadaye kuwapa nafasi ya kugombea ubunge, lakini Dk Slaa anasema safari hii hawatakuwa tayari kufanya hivyo.

"Tulishasema kwamba kwa ngazi zozote hata ngazi za udiwani au ubunge hatusubiri mabaki, makapi yatakayotokea CCM ndiyo yaje kwetu," alisema Dk Slaa katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

"Safari hii hatusubiri. Tulishasema kuwa wagombea wetu tunawaandaa mapema ili tusitegemee mtu anayekuja dakika za mwisho kuwa ndiyo atuokoe."

Kauli ya Dk Slaa inaweka msisitizo katika ile iliyowahi kutolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba hawatapokea wanasiasa watakaoihama CCM ili kupata nafasi za uongozi kwa tiketi ya Chadema.

Katika mahojiano hayo, Dk Slaa alisema: "Huwezi kuzuia kupokea mwanachama kokote alikotokea, lakini unapofika wakati wa kuweka watu katika nafasi, lazima ufikirie."

Mwaka 2010, Chadema ilipokea wagombea wawili walioshindwa kwenye kura za maoni za CCM, John Shibuda aliyeshindwa katika kura za maoni za Maswa Magharibi na Freddy Mpendazoe ambaye alienguliwa kwenye kura za maoni za CCM Jimbo la Segerea.

Shibuda alifanikiwa kurudi bungeni baada ya kushinda uchaguzi wakati Mpendazoe alishindwa katika hali ya kutatanisha na juhudi zake za kutengua matokeo hayo mahakamani ziligonga mwamba.

"Tatizo hilo lilitokana na ugeni wetu," alisema Dk Slaa akizungumzia kitendo cha Chadema kupokea wagombea walioshindwa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

"Lakini kwa wakati huu, Chadema ina wanachama wengi wenye sifa za kugombea hivyo hatuhitaji kusubiri mtu," aliongea katibu huyo mkuu ambaye aliwahi kutangaza kuwa nafasi za wagombea ubunge wa Chadema katika majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti na watakaojitokeza, watafanyiwa usaili.

Kuhusu uchaguzi mkuu wa chama hicho, Dk Slaa alisema utafanyika Desemba mwaka huu baada ya kuridhiwa na kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika Julai 18.

Alisema wanahakikisha uongozi unapatikana kuanzia ngazi za chini na watachukua hatua kwa maeneo ambayo watabaini viongozi wamepeana nyadhifa bila chaguzi madhubuti kufanyika
.

Chanzo; Mwananchi
 
Hatutaki mashibuda tena,Huku Mwanza tunaye Matata ambaye alihamia CDM tukamuani kumbe ni gamba mchumia tumbo tu! Awamu hii hatutaki makapi na hili lisimamiwe vizuri na kila mwana CDM!
 
Dr. Slaa katibu mkuu wa CHADEMA Taifa amesema kuanzia ngazi ya Udiwani hawatachukua wanaoachwa na CCM kugombea ndani ya CHADEMA.
Source Mwananchi gazeti la leo.

Kwa hiyo yeye slaa na rose camil watakua wa kwanza kuachia ngazi maana wao ndio makapi namba moja.
 
Hana lolote yeye mwenyewe alikuwa kapi la CCM na aliondoka CCM kwa sababu hizo hizo anazozikataa yeye
 
Mwaka 2010 chama kilikuwa hakijasimama sawa ndio maana hata maeneo kadhaa kilikosa watu wa kuwasimamisha hivyo ikabidi yeyote anayejitokeza apokelewe na kusimamishwa. Hapa hakuna wa kumlaumu kwa yaliyojitokeza kwa haya makapi ya CCM. Ila kwa sasa chama kiko sawa na hakina sababu ya kupokea kila mtu maana kwa sasa chama kina hazina kubwa ya watu makini sana. Hao watakaotemwa huko wajue wameumia hawana pa kukimbilia.

Kwanza huu mpango wa UKAWA wa kuachiana na kupeana support katika majimbo kulingana na kukubalika kwao inaweza kusababisha CCM ikaambulia wabunge wasiozidi 50 uchaguzi ujao. Angalieni kwa mfano mikoa kama Lindi na Mtwara ambako ilikuwa ngome kuu ya CCM jee leo hii inachakusema kule? Walivyotuma wanajeshi kuwapiga na kuwabaka dada zao na mama zao walitegemea nini? Kiburi chao ndio kaburi lao.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Dr. Slaa katibu mkuu wa CHADEMA Taifa amesema kuanzia ngazi ya Udiwani hawatachukua wanaoachwa na CCM kugombea ndani ya CHADEMA.
Source Mwananchi gazeti la leo.
=======================

Chanzo; Mwananchi

Huyu babu mbona na yeye ni kapi kutoka ccm?
 
HATUTACHUKUA WALIOKATWA NA CCM WAKITAKA WAJE MAPEMA-DKT SLAA

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitasubiri wanachama watakaoachwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uteuzi wa wagombea katika uchaguzi mkuu ujao. Kutokana na tamaa ya kuingiza watu wengi kwenye Bunge, vyama vya upinzani vimekuwa na tabia ya kuwapokea wanachama wa CCM wanaoshindwa kwenye kura za maoni na baadaye kuwapa nafasi ya kugombea ubunge, lakini Dk Slaa anasema safari hii hawatakuwa tayari kufanya hivyo.

"Tulishasema kwamba kwa ngazi zozote hata ngazi za udiwani au ubunge hatusubiri mabaki, makapi yatakayotokea CCM ndiyo yaje kwetu," alisema Dk Slaa katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
"Safari hii hatusubiri. Tulishasema kuwa wagombea wetu tunawaandaa mapema ili tusitegemee mtu anayekuja dakika za mwisho kuwa ndiyo atuokoe."

Kauli ya Dk Slaa inaweka msisitizo katika ile iliyowahi kutolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba hawatapokea wanasiasa watakaoihama CCM ili kupata nafasi za uongozi kwa tiketi ya Chadema.

Katika mahojiano hayo, Dk Slaa alisema: "Huwezi kuzuia kupokea mwanachama kokote alikotokea, lakini unapofika wakati wa kuweka watu katika nafasi, lazima ufikirie."

Mwaka 2010, Chadema ilipokea wagombea wawili walioshindwa kwenye kura za maoni za CCM, John Shibuda aliyeshindwa katika kura za maoni za Maswa Magharibi na Freddy Mpendazoe ambaye alienguliwa kwenye kura za maoni za CCM Jimbo la Segerea.

Shibuda alifanikiwa kurudi bungeni baada ya kushinda uchaguzi wakati Mpendazoe alishindwa katika hali ya kutatanisha na juhudi zake za kutengua matokeo hayo mahakamani ziligonga mwamba.

"Tatizo hilo lilitokana na ugeni wetu," alisema Dk Slaa akizungumzia kitendo cha Chadema kupokea wagombea walioshindwa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

"Lakini kwa wakati huu, Chadema ina wanachama wengi wenye sifa za kugombea hivyo hatuhitaji kusubiri mtu," aliongea katibu huyo mkuu ambaye aliwahi kutangaza kuwa nafasi za wagombea ubunge wa Chadema katika majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti na watakaojitokeza, watafanyiwa usaili.

Kuhusu uchaguzi mkuu wa chama hicho, Dk Slaa alisema utafanyika Desemba mwaka huu baada ya kuridhiwa na kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika Julai 18. Alisema wanahakikisha uongozi unapatikana kuanzia ngazi za chini na watachukua hatua kwa maeneo ambayo watabaini viongozi wamepeana nyadhifa bila chaguzi madhubuti kufanyika.

Chanzo: Mwanachi
 
Alisema Zitto,usiamini maneno ya WANASIASA,haya huyooooooooooooo Lowassa atua CDM na kupewa UGOMBEA URAIS ,ila kama panaukweli NI AIBU,kuchukua UCHAFU toka nyumba ya jirani eti PAMBO kwenye sebule yako.Hapa ndipo sitawaelewa viongozi wa CDM,na Dr.Slaa mwenyewe,sitamuelewa kamwe,unachukuaje mtu anayenunua uongozi?

Itabidi niwauliza CDM mmepewa shilingi ngapi viongozi wangu?Nausemea moyo wangu.Hata nia mshwe USIKU VOTE NO FOR LOWASSA period.

BILA LOWASSA CHADEMA INAWEZA
 
Sasa babu anakataa nini na kukubali nini, mzee anachekesha kweli huyu, mbona kutwa wanaomba fisadi papa aje.
 
Alisema Zitto,usiamini maneno ya WANASIASA,haya huyooooooooooooo Lowassa atua CDM na kupewa UGOMBEA URAIS ,ila kama panaukweli NI AIBU,kuchukua UCHAFU toka nyumba ya jirani eti PAMBO kwenye sebule yako.Hapa ndipo sitawaelewa viongozi wa CDM,na Dr.Slaa mwenyewe,sitamuelewa kamwe,unachukuaje mtu anayenunua uongozi?

Itabidi niwauliza CDM mmepewa shilingi ngapi viongozi wangu?Nausemea moyo wangu.Hata nia mshwe USIKU VOTE NO FOR LOWASSA period.

BILA LOWASSA CHADEMA INAWEZA
Mbona huu uchangiaji wako hauendani kabisa na habari husika, ama hii ni muendelezo wa habari hiyo hapo juu. Maana haijamtaja kumpokea Mh. Lowasa. Otherwise inapingana kabisa na kumpokea mwanachama kutoka chama kingine kwaajili ya kutaka madaraka.
 
Mwaka 2010 chama kilikuwa hakijasimama sawa ndio maana hata maeneo kadhaa kilikosa watu wa kuwasimamisha hivyo ikabidi yeyote anayejitokeza apokelewe na kusimamishwa. Hapa hakuna wa kumlaumu kwa yaliyojitokeza kwa haya makapi ya CCM. Ila kwa sasa chama kiko sawa na hakina sababu ya kupokea kila mtu maana kwa sasa chama kina hazina kubwa ya watu makini sana. Hao watakaotemwa huko wajue wameumia hawana pa kukimbilia.

Kwanza huu mpango wa UKAWA wa kuachiana na kupeana support katika majimbo kulingana na kukubalika kwao inaweza kusababisha CCM ikaambulia wabunge wasiozidi 50 uchaguzi ujao. Angalieni kwa mfano mikoa kama Lindi na Mtwara ambako ilikuwa ngome kuu ya CCM jee leo hii inachakusema kule? Walivyotuma wanajeshi kuwapiga na kuwabaka dada zao na mama zao walitegemea nini? Kiburi chao ndio kaburi lao.

Sent from my iPad using JamiiForums

Hii taarifa ni ya muda mrefu ivyo mbona? Week ni ndefu sana kwenye siasa, lolote linaweza tokea
 
Mbona huu uchangiaji wako hauendani kabisa na habari husika, ama hii ni muendelezo wa habari hiyo hapo juu. Maana haijamtaja kumpokea Mh. Lowasa. Otherwise inapingana kabisa na kumpokea mwanachama kutoka chama kingine kwaajili ya kutaka madaraka.

Haujasikia MAGAZETI ya Leo? Inaendana sana, maana anachoongea Dr. Slaa ni tofauti na tusikiacho, unless atoke akisemee kwamba hiki cha kwenye magazeti si sahihi.

Je Lowassa hajakatwa? Au sababu ana pesa?

Au alikuwa anaongelea nini, sikumuelewa aliyeleta mada????
 
Katibu Bora Kabisa Kuwahi Kutokea Katika Siasa Za Tanzania,
 
Asee mzee huyu atakufa kwa kihoro na majuto. . . .Kama kweli yasemwayo yapo basi Mungu ampe mja wake roho ya uvumilivu sana. . . . !!!!!
 
Hana lolote yeye mwenyewe alikuwa kapi la CCM na aliondoka CCM kwa sababu hizo hizo anazozikataa yeye

Aaaah mimi hili nililisemea mapema kabisa Dr Slaa hana huo uwezo wa kishindana na Makapi maana yeye mwenyewe ni zao la makapi hata akileta ubishi wenye chama watamuuliza mbona hata wewe ulikuwa kapi na tukakupokea na uongozi tukakupa?
 
Back
Top Bottom