Chadema hapatoshi Mwanza

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
VIONGOZI wa juu na wabunge wa Chadema jana walitawanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza na kufanya mikutano ya hadhara kuendelea kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.

Viongozi na wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Katibu wake mkuu Dk Willbrod Slaa aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31 mwaka 2010 walichagiza katika mikutano hiyo ya mtawanyiko.

Mikutano hiyo ya hadhara ilikusanya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mwanza, huku mwenyekiti Mbowe akifanya mkutano wa hadhara wilayani Geita akiwa ameongozana na wabunge wanne wa chama hicho na Katibu wake Dk Slaa akiwa Kisiwani Ukerewe ambako naye aliambatana na mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli na wabunge wa viti maalum, Rebecca Mngodo na Grace Kiwelu.
 
Freeman Mbowe
Mbowe alifuatana na Joseph Mbilinyi ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini, Halima Mdee (Kawe), Paulina Gekul na Anna Mallaki (viti maalum) pamoja na Profesa Kulikoyela Kahigi wa Bukombe.

Akihutubia katika mkutano huo Mbowe alisema wilaya ya Geita, ni masikini kupindukia kutokana na wananchi wake kuhujumiwa na viongozi wachache walioko serikali licha ya kuwa na mgodi mkubwa wa dhahabu.

Mbowe aliyasema hayo katika uwanja wa magereza nje kidogo na mji wa Geita, katika mkutano ambao ulitanguliwa na maandamano yaliyoaongozwa naye, huku wafuasi wa chama hicho wakibeba mabango mbalimbali, moja likilosomeka,''Dowans ikilipwa, mimi nitajiua. Mtanzania halali'.'

Huku akikatishwa na kelele za wananchi Mbowe alisema kuwa mgodi huo ilikuwa umejitolea kutoa umeme katika mji wa Geita kwa kuunganisha kwenye gridi ya taifa, lakini viongozi wa CCM waligoma kwa vile wao hawana uchungu na mgao wa umeme na kwa vile wana majenereta nyumbani kwao.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alirejea kauli yake kuwa kamwe Chadema hakitakubali ushirika na vyama vingine bungeni akidai kuwa vyama hivyo ni mawakala wa CCM, lakini akasema chama chake hakina ugomvi na wananchama wa vyama hivyo na kuwaomba radhi kuwa ugomvi uliopo ni kati ya chama hicho na viongozi wa vyama vingine vya upinzani hasa kile cha CUF.
 
Dk Wilbroad Slaa
Dk Slaa alifanya mkutano wake wilayani Ukerewe ambapo amemtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kwa kile alichokiita uzembe wa serikali yake, kuendelea kusababisha maafa kwa wananchi pamoja na kauli yake ya kutowafaamu wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans.

Alisema haiingi akilini kuwa Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lililoidhinisha mkataba wa kampuni tata ya Richmond ambao umerisishwa kwa Dowans kudai kuwa hafahamu wamiliki wake ambapo aliongeza kuwa ikiwa ni kweli Kikwete hawafahamu wamiliki wa kampuni hiyo, basi huo ni uzembe na anatakiwa kujiuzulu pamoja na serikali yake.

Dk Slaa alisema pia kwamba Chadema haitakubali Tanesco kuingia mkataba na Dowans kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba anavyoshauri, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kupinga hilo .

Akifafanua alisema kimsingi mitambo hiyo inastahili kutaifishwa na kuonya kuwa kitendo cha kutaka kuingia mkataba na kampuni ya kifisadi ni ya kushangaza, kwani Serikali ilitambua tatizo la umeme wa kutegemea mabwawa ya maji tangu mwaka 2001 na baadaye tatizo hilo likajitokeza mwaka 2003.

"Serikali makini, ingenunua mitambo yake yenye uwezo wa kuzalisha nishati hiyo na siyo kuingia mikataba ya kifisadi kama ya Richmond na baadaye Dowans," alisema Dk Slaa.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema kwamba ameshangazwa na mtu aliyejitokeza kuwa ndiye mmiliki wa Dowans (Suleiman Al- Adawi) kujitokeza sasa akitoa madai tofauti ikiwemo na kutaka kusamehe deni hilo, baada ya kubaini mpango wa Chadema wa kutaka kutumia umma kupinga utapeli huo.
 
title zingine zinatisha kweli,ila afadhali content haitishi!

Nice to hear,wasichoke mchaka mchaka hadi 2015
 
Mkutano wa Misungwi
Katika Wilaya ya Misungwi mkoani humo mkutano wa hadhara wa Chadema uliongozwa na mbunge wake wa Ilemela, Highness Kiwia huku ikielezwa kuwa mkutano huo ulisababisha kuvunjika kwa mkutano wa hadhara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, George Mkuchika uliokuwa ufanyike wilayani humo.

Katika mkutano huo Kiwia alifuatana na wabunge wa viti maalum wa Chadema Raya Ibrahim (Pemba) na Chiku Abwao (Iringa) ambapo alisema aliyekuwa mpinzani wake katika kuwania kiti cha ubunge Anthon Diallo amemfungulia kesi mahakamani akimtuhumu kwa kuiba kura katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010.

Kiwia alisema pamoja na kumshitaki akidai aliiba kura kura zilizompa ushindi ametuhumiwa pia kufanya kampeni za vitisho na kusababisha wananchi kuogopa kujitokeza kwenda kupiga kura, lakini akasema ana uhakika kuwa waliomuweka madarakani ni wananchi kwa ridhaa yao na kudai kuwa atawapigania katika kuleta maendeleo.

Kuhusu Katiba Kiwia alisema Chadema haitapumzika hadi Serikali ifanye mabadiliko ya katiba ambayo itamuwezesha mtanzania kufanya uchaguzi wa haki na kweli bila ya kupigwa mabomu.
Katika mkutano huo wananchi waliohudhuria walipaza sauti wakisema kuwa Rais Kikwete hana budi kujiuzulu wakidai ameshindwa kuindesha nchi hii.
 
Mkutano wa Kwimba
Ezekia Wenje alifanya mkutano wake wa hadhara katika wilaya ya Kwimba huku akitoboa siri ya yaliyomsibu wakati wa kampeni za kuwania ubunge wa jimbo hilo.

Katika mkutano wake Wenje alifuatana na wabunge wenzake wa chama hicho ambao ni Rachel Mashishanga, Philip Maturano, Joyce Mukya pamoja na mkurugenzi wa fedha wa chama hicho Antony Komu.

Wenje alidai kuwa katika uchaguzi uliopita alihongwa Sh300 milioni ili ampishe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo Lawrence Masha ambapo pia alidai moja ya chama siyo Chadema kilitenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuwagawia wapiga kura ili wachague chama hicho, lakini wananchi wa jimbo hilo waligoma na kulinda kura zao.

Viongozi hao wa Chadema na wabunge wao watafanya maandamo ya amani na baadaye mkutano wa hadhara leo katika mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa taarifa hizo maandamano hayo yataanza saa 5 asubuhi yakianzia eneo la Makutano na kuelekea katikati ya mji wa Musoma kwenye uwanja wa michezo wa Mkindo.

Habari zinaeleza kuwa ujumbe wa maandamano na mkutano wao wa hadhara ni sawa na ule walioutoa mkoani Mwanza, kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.
Habari hii imeandaliwa na Sheila Sezzy, Misungwi, Frederick Katulanda, Kwimba na Jovita Kaijage, Ukerewe.
 
Habari zinaeleza kuwa ujumbe wa maandamano na mkutano wao wa hadhara ni sawa na ule walioutoa mkoani Mwanza, kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.
Habari hii imeandaliwa na Sheila Sezzy, Misungwi, Frederick Katulanda, Kwimba na Jovita Kaijage, Ukerewe.

Nitafurahi nikisikia kuwa watapinga na malipo ya makampuni yaliyoingia mikataba kifisadi na ambayo ni mzigo mkubwa kuliko Dowans, nitafurahi nikisikia wanaichokonoa na IPTL yenye mkataba wa kinyonyaji wa miaka 20 otherwise nitaendelea kutowaamini wanasiasa na nitajiridhisha kuwa wanasiasa hufanya yale yenye manufaa na wao tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom