CCM inajipambanua kuwa chama kisichopenda rushwa, wakati ni tofauti kabisa na matendo yake. Kinanunua, kina warubuni na mara nyingine kuwatisha kuwafilisi mali zao wapinzanu wasipohama upinzani. Ahadi za kupewa madaraka nje ya upinzani ndo ngao yao kubwa (nafikiri hii ina baraka ya mkubwa wao).
Anayerudi CCM kwa kisingizio cha kwamba hicho chama sasa kinafanya makubwa ni zezeta, ni makubwa yapi? Mfano wa haraka ni kile kitendo cha rais kuzuia private contarctors kujenga hostel za UDSM na badala yake wakajenga TBA - ni nini kimetokea? Ni ujenzi usiokidhi engineering specifications ambao umeleteleza crack kubwa kabla hata mwaka kwisha. Sasa kitachofuata ni gharama mara dufu, either tubomoe ukuta ujengwe upya au tuwe wa kuziba mara kwa mara.
Mifano ni mingi. Ugua au uguliwa ukazwe Muhimbili, kama unapaswa kupelekwa chumba cha upasuaji uatkuta hata machela hayapo na kama yapo hakuna nesi wa kuyasukuma hadi huko - upuuzi mtupu. MOI hukomndo usiseme.
Nenda mahakamani uone jinsi haki inavyonunuliwa kwa pesa......
Tukija maisha ya kawaida leo ni afadhai ya jana. Wanaokula mara tatu kwa siku namba yao inapungua kila siku na hii ni hatari sana.