CHADEMA hakiipeleki CCM mahakamani kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA hakiipeleki CCM mahakamani kwanini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kingadvisor, Dec 28, 2011.

 1. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na matamshi mengi kutoka CHADEMA kuwa CCM ni chama cha mafisadi.Hivi kama wana ushahidi kwa nini hawakipeleki mahakamani? Wanabaki kusema kwenye bunge ,mikutano ya hadhara na vyombo vya habari wakati mahakama zipo.Ni kwa nini kama kweli wamepania kusaidia nchi hawakipeleki CCM mahakamani? ukweli ukathibitike huko? Siamini kwa chama kinachoamini utawala wa sheria kinaweza kuishia kusema mafisadi kwenye press conference,mikutano ya hadhara na bungeni kikaacha kwenda mahakamani kama kinao ushahidi wa kutosha.Vinginevyo kama hakina kitabaki kinabwabwaja maeneo ambayo hakuna hatua ya maana inayoweza chukuliwa na kuiacha nchi ikiendelea kuumia.

  Nadhani ni wakati muafaka wananchi tushinikize vyama na viongozi wa upinnzani,wa Dini na wale wa ndani ya CCM wanaoimba wimbo wa kuweko mafisadi tuwaambie kuwa kama wako serious wanaona CCM ni mafisadi na kuna mafisadi wanaowajua na wanaowataja majukwaani bila aibu wala kumeza maneno wakawafungulie mashtaka mahakamani vinginevyo binafsi nawaomba wananchi tuwaone kama wanasiasa wasioheshimu utawala wa sheria na waendesha siasa za maji taka wawe CCM au nje ya CCM maana mwizi haongelewi barabarani hukimbizwa hupelekwa polisi na baadaye mahakamani.Kila chama na kila mtu ana haki ya kisheria. Si haki hata kidogo kupiga yowe kwenye mabarabara kuwa fulani fisadi au chama fulani fisadi bila ushahidi wa kutiwa hatiani wa kimahakama hata kama una vipande vya magazeti ulivyokata millioni vilivyoandika tuhuma za ufisadi wao.

  Kuanzia leo sisikilizi tena mtu au chama kiwe Chadema au CCM au chama chochotete kitakochosema kuna mafisadi popote kama hakiwapeleki mahakamani nitakiona au kumwona mtu huyo anayesema hivyo tapeli wa kisiasa na mwendesha siasa za maji taka ambazo haziwezi kuikomboa nchi hii.Nimechoka siasa za maji taka.

  kingadvisor@yahoo.com
   
 2. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa wewe kumbe jibu la kwa nini CDM haiendi mahakamani unalo alafu unaanza kuleta porojo humu jamvini. Ok ni hivi CDM hakiamini katika Utawala wa Sheria uliopo nchini hivi sasa ndio maana hakiendi mahakamani.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mods: ebu kuweni makini na matumizi ya neno "Masaburi" ili tukomeshe wahuni humu Jamvini.
   
 4. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  kumbe umeshaona CHADEMA ndo mtetezi wako, sasa kwanini hukisupport?.
  Mkuu chadema inaamin katika nguvu ya umma. so mahakama ya chadema ipo kwa wananchi. ndo maana chadema ikisema inaenda kwa wananchi ccm inatetemeka sana. CHADEMA wanajua Tanzania hakuna utawala wa sheria ndo maana hawaendi mahakamani. Mia
   
 5. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hakiamini utawala wa sheria uliopo kwa nini kimesajiliwa kwa sheria zilizopo,kinapokea ruzuku kwa sheria zilizopo,kinaenda bungeni na kupata posho za vikao kwa sheria zilizopo? Kingekuwa hakitambui kingekuwa cha wapigania uhuru wa msituni kisingetafuta usajili.
   
 6. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CHADEMA ni chama makini ndugu yangu. Hakuna mahakama iliyoimara na yenye haki kama wananchi. Kitendo cha CHADEMA kusema kwa wanachi wenye nguvu ishara tosha kwamba kipo kwa ajiri wa wananchi. Wananchi ndio siku ya siku itakapofika watatoa hukumu kwa wale wote wanaosemwa semwa.

  Chama makini kama CHADEMA si rahisi kusema bila ushahidi kwasababu kinajua pindi itakapodhibitika kuwa si sahihi kitakuwa kimejijengea taswira mbaya kwa wananchi. Mbona wanaotajwa kuwa ni mafisadi hawaendi mahakamani kutafuta haki? :yawn:
   
 7. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hii yako ni pumba kabisa. Wewe uliona wapi kesi ya jinai ya wizi wa mali ya uma ikapelekwa mahakamani na chama? Hii ni kazi ya jamhuri. Nilitegemea ujiulize swali hili "Kwa nini vyombo vya dola havifanyi utafiti kubaini hizi tuhuma zinazotolewa na CDM ili wawafungulie mashataka wahusika?" Dr Slaa amezungumza kwa nguvu zote kwenye bunge la tisa kuhusu wizi wa Meremeta, Tangold, Deep green finance,Mwananchi Gold, Kagoda nk. Sasa unajua wanaotakiwa kuchunguza na kuwapeleka watuhumiwa mahakamani? Sasa solution ni moja tu. 2015 pigia CDM iingie madarakani, halafu baada ya miezi mitatu toka wachukue madaraka hawatawafikisha wote waliowasema ni mafisadi, itabidi nao tuwatilie mashaka. Nchi hii inahitaji overhaul ya mfumo ili haki itendeke na mali asili zetu zilindwe.

  Mimi nina hakika asubuhi inakaribia na ukombozi wa Mtanganyika uko just around the corner.

  MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Kama vipi lichukue ukalifungie kabatini kwako,kama hutaki watu walitumie.
   
 9. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini alienda kusema bungeni kwa nguvu zote kwa nini hakwenda kwenye vyombo vya dola ili wachukue hatua? sehemu ambayo yangethibitishwa hayo na kuchukuliwa hatua ni mahakamani sio bungeni.Kama mtu mwenye uchungu na nchi angepeleka huko na ushahidi wake.
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona na wewe umelitumia hilo neno? Au na wewe ni Muhuni humu Jamvini?!

   
 11. k

  kuzou JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  NENO UFISADI NI KARATA YA CDM YA KISIASA na wao wanajua ukweli.
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika mambo uliyoyataja hapo juu kinaamini katika sheria zinazotumika lakini katika swala la kupeleka Mafisadi Mahakamani hakiamini Mfumo wa Sheria unaotumika kuhukumu Mafisadi!

   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Inaonekana wazi kabisa kuna mtu ana ku Cameron!
   
 14. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndgu yangu ni kweli kwamba unapenda sana cdm iwe inaact utakavyo wewe,na ni kuthibitishie tu kwamba hicho unachokitaka ndio na cdm wangependa iwe hivyo.Tatizo liko kwenye mfumo wa kupeleka kesi za ufisadi mahakamani.Kuna mmoja humu kajaribu kukueleza naona kama umeamua tu kumignore lkn ukweli ni kwamba cdm haiwezi kufungua kesi za ufisadi nchi hii.Nakushauri jaribu kuulizia au kufuatilia kazi ya DPP (Director of Public Prosecution)na TAKUKURU.njia waliyonayo cdm kwenye hili la ufisadi ni kuwaeleza tu wananchi na ndo hicho wanachozidi kufanya mpaka sasa.
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  huelewi maana ya falsafa ya NGUVU YA UMA
   
 16. d

  dotto JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mahakam kuu ya TAnzania ni Nguvu ya Umma.
   
 17. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mtoa hoja inaelekea hujui kabisa mfumoi wa sheria unavyofanya kazi.................... chama chochote cha siasa hakiwezi kufungua kesi ya jinai mahakamani, hata ccm hawawezi...................... kafanye tena homework yako kuhusu taratibu za kuendesha kesi za jinai.............. hususani kazi za mkurugenzi wa mashitakla, polisi, takukuru nk..................... kisha urudi hapa na mawazo ama maswali mazuri zaidi......................
   
 18. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna aliye juu ya sheria awe mtu mmoja mmoja au umma.Au ulitaka umma uwe juu ya sheria ndio hicho kinachoitwa nguvu ya umma.
   
 19. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...naunga mkono hoja 100%...
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  masaburi at work
   
Loading...