CHADEMA haiwezi kushindana na serikali kwa namna hii; Iitishe mgomo wa Kitaifa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Na. M. M. Mwanakijiji
Kilichotokea Arusha Jumamosi iliyopitajioni ni kitu cha kulaaniwa kwa kauli yote kali. Lakin pia ni kitu ambacho kinahitaji CHADEMA ioneshe kuwa ‘sasa imetosha’. Inawezekana vipi ndani ya miaka karibu mitatu tu vitendo vya kinyama vimekuwa vikifanyika dhidi ya Wanachadema mara kwa mara wanapojaribu kufanya mikutano ya amani? Ni nani amesahau yaliyotokea ile Januari 5 huko huko Arusha na matukio mengine yaliyofuatia kuanzia Mwanza, Iringa, Morogoro, Songea, Tukuyu, Mbeya, Igunga na sehemu nyingine?

Hivi ni kweli nchi yetu ina vyombo vyovyote vya usalama? Ni kitu gani kwa kweli wameweza kukilinda kikawa salama? Matukio haya yote yangelazimisha kufukuzwa kwa watendaji wakuu wa vyombo vya usalama – Polisi, TISS n.k. Nilishawahi kuuliza huko nyuma katika mojawapo ya makala zangu – MPAKA NANI AUAWE ndio tutajua kuwa tuna tatizo?

Tukio la Arusha ni ishara tu ya kile ambacho kiko vibaya – ubovu wa mfumo wetu wa intelligensia na usalama. Kama tunavyojua tukio hili limekuja miezi michache tu baada ya tukio kama hilo huko huko Arusha katika Ibada ya Wakfu ya Kanisa Katoliki. Nani atasahau mazingira yale ni kama yamejirudia tena? Na safari hii sijui watamkamata kijana gani maana hawa vijana wenye ujuzi na uthubutu wa hivi ni lazima wawe makini kweli – na inaonekana wako wengi! Yule mwingine bado yuko ndani halafu kuna mwingine/wengine?

CHADEMA ndio wamekuwa waathirika wakuu wa matukio haya nan i wanachama na viongozi wao ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya aina hii na inashangaza wakati mwingine mbele ya polisi. Ni nani amesahau jinsi wale wabunge wa CDM walivyopigwa kule Mwanza? Au nani kasahau watendaji wa CDM walivyopigwa kule Kiteto? Au nani kasahau mauaji ya kinyama ambayo Polisi hadi leo hawayajtolea maelezo ya kijana wa CDM kule Igunga? Au ni kumbushe tukio lile la Januari 5 huko huko Arusha?

Bahati mbaya sana CDM bado wameendelea kuamini kuwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu jeshi la polisi litabadilika sasa hivi na kuonesha weledi na kutoa ulinzi na kuhakikisha usalama wao. Wapo kabisa watu ndani ya CDM wanaoamini kuwa wakitoa kauli kali basi Polisi watetemeka au kina Mwema watabadilika? Ni ndoto za Alinacha. Bila kuwatumia ujumbe watawala kuwa mizani ya nguvu imebadilika na sasa upepo umebadilika. Maneno makali na nyuso za huzuni na hata machozi havijawatisha watawala na zaidi tumeona kuwa vinawafanya wawe na mioyo migumu zaidi! Inahitaji moyo sana kulaumu wahanga kwa madhara yanayowapata!

Maoni yangu yako wazi kabisa CDM waoneshe msimamo vinginevyo – na nilishawahi kuwaambia ndugu zangu hawa – wataendelea kuzika na kubeba majeneza ya wanachama wao na mashabiki wao. Msimamo wao uwe wazi kabisa kuwa sasa imetosha. Baadhi ya mambo ambayo naamini yanatakiwa yawepo kwenye msimamo huo:

a. Kutaka Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Operesheni pamoja na DCI kujiuzulu au kufukuzwa kazi. Matukio kama haya yanahitaji watu kuwajibishwa siyo kupandishwa vyeo kama ilivyotokea kwa Kamuhanda!

b. Kutaka Mkuu wa Usalama wa Taifa awajibishwe. Taasisi hii imekuwa dhaifu kuliko wakati wowote wa historia yetu. Udhaifu wake unatokana kwa kiasi kikubwa na kuwa “compromised”. Inapofikia mtumishi wa Idara anakufa kwenye kisima cha maji Makao Makuu ya Idara pamoja na mauaji na vifo vya baadhi ya maafisa wa TISS ndani ya miaka miwili tu inatosha kuhoji weledi, uwezo, na utendaji wa Mkurugenzi wa Idara hiyo.

c. Kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani awajibike au awajibishwe. Ameshindwa kuonesha uongozi na maono ya kulibadilisha jeshi la polisi kulifanya liwe la kisasa na siyo la kisiasa kama lilivyo sasa.

e. Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa awajibike yeye mwenyewe kwa kuvumilia kauli za viongozi wa CCM ambao kwa kauli zao wao wenyewe wamejithibitisha kuwa wako katika mipango ya kukidhulumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Msajili anaposhindwa kukemea na kuwawajibisha watendaji hawa anaonekana kukibeba na tusije kushangaa na yeye akimaliza zamu yake atapozwa na ka-jiubalozi fulani ‘somewhere’.

Kilichotokea ni mwendelezo wa kuvurugika na kubomoka kwa mfumo wa Usalama na Intelligensia wa Tanzania; ni matokeo ya kuendekeza mifumo ya usalama ambayo imeshaonesha kuwa imeshindwa. Kama watu wanaweza kufanya hivi kwa uchaguzi wao – iwe kanisani au uwanjani- hivi tumefikiria uwezekano wa jambo kama hili kutokea mahali ambapo pana viongozi wa serikali, watoto, au mashuleni? Ni udhaifu gani huu wa mfumo?

Sasa yasiwe matakwa ya juu juu tu; ujio wa Rais Obama ni nafasi nzuri ya kusukumikiza ajenda ya haki za kiraia na binadamu nchini na mbele ya jamii ya Kimataifa. Njia mojawapo ni kutumia nafasi ya ujio huu kuitisha maandamano makubwa zaidi nchini yawe ya active (ya watu kuandamana) au ‘passive’ ya kusimamisha shughuli zote nchini dhidi ya Jeshi la Polisi na Serikali endapo watajwa hapo juu hawatakuwa wameondolewa.

Si lazima kufanya maandamano ya watu kutembea barabarani kwani kufanya hivyo ni kuwapa kisingizio watawala kutumia nguvu zaidi; lakini inawezekana pia kufanya maandamano ya kunyamaza; aina ya mgomo wa kuwakatalia watawala. Yaani, kukataa kufanya mambo fulani ambayo yatatuma ujumbe kwa watawala kuwa sasa “nguvu ya umma” imechoka na itatumika.

Watanzania na wapenda mabadiliko wanasubiri kuona CDM itafanya nini tena; je itaendelea kutoa maneno makali na kuendelea kucheza ‘zero distance’ na CCM huku wanachama wake wakiendelea kupopolewa na damu kumwagika? Je wataendelea kukubali kubebeshwa lawama kwa matukio ambayo yanawaangukia wao?

Kama CDM wanaona kuwa hawawezi kufanya passive resistance kama ambavyo kina Martin Luther Kinga walifanya na kusababisha mabadiliko basi wasitishe maandamano na mikutano yao. Haiwezekani waendelee kufanya mikutano na watu wao wanapigwa na kuumizwa halafu wanaishia kutoa matamko makali na sura zilizojaa ndita lakini wakija kwenye vitendo hakuna kinachofuatia! Siyo tu kusitisha maandamano bali watangaze kutokushiriki uchaguzi mwingine wowote kwani gharama ya kufanya chaguzi hizi ni kubwa zaidi kwa maisha ya watu kuliko watu wanavyofikiria.

Binafsi nitalaani vikali kama CDM itashiriki uchaguzi wa marudio hapo Arusha kama watu wale wale – Polisi, Usalama wa Taifa, RPC na Msajili wa vyama wataendelea kuwepo. NItalaani kwa sababu CDM itakuwa inakubali kuwa chini ya huruma ya watu wale wale waliothibitika kushindwa na walioonesha udhaifu uliopitiliza. Vinginevyo, watakuwa wanakejeli damu ya MASHAHIDI WA TANZANIA MPYA ambayo tayari imemwaga nchini!

Ni kwa hili tu nitaendelea kuwaunga mkono CDM badala ya kusubiri kauli za kisiasa na kunyemeleana. Wanachama na Mashabiki wenu wanataka kuona mnaongoza siyo mnavaa magwanda lakini hamuoneshi uthubutu wa kusimamia mnachoamini. Magwanda na kauli kali wakati wa mazishi mengine hazitoshi tena. Ni wakati wa vitendo. Na hapa simaanishi vitendo vya kulipiza kisasi; bali vitendo vitakavyomulika udhaifu wa vyombo vya usalama lakini zaidi vitendo vitakavyomulika jinsi haki za raia na haki za binadamu zinavunjwa nchini.

Na hili linaweza kufanywa kwa kuitisha mgomo wa kitaifa kama aina ya passive resistance ya utawala wa kiimla wa chama kimoja. Siku hii siyo tu ya watu kugoma kwenda kazini lakini pia kufunga, na kufanya mambo yaende pole pole (go slow movement). Mfano mzuri wa hii go slow ni kama kilichotokea hapa Detroit miezi michache nyuma ambapo wananchi wanaotumia magari waliamua kupunguza mwendo kwenye barabara kuu kupinga kitendo cha Serikali ya Jimbo kumteua Mwangalizi Maalum wa Jiji na kuwaweka pembeni viongozi wa kuchaguliwa wa Jiji hili lenye matatizo. Japo Mwangalizi huyo aliweza kuja lakini hakuweza kufanya mengi bila kuwahusisha viongozi kwani wananchi walishaonesha namna ya kugoma. Unapotumia ‘passive resistance’ polisi na usalama wa taifa hawana cha kufanya! Hawawezi kuwalazimisha watu kutembea haraka au kwenda kazini!

Hili lisiwe kwa watu wengine tu bali wabunge wote wa CDM nao wagome kuingia Bungeni kwa muda wote wa siku za mgomo (na hivyo kunyimwa posho za siku hizo). Ujumbe ni lazima utumwe kuwa nguvu ya umma ni kweli ina nguvu. Nguvu ya umma isiwe katika kuhesabu umati wakati wa kuhutubia au maandamano; bali iwe katika kulazimisha serikali kufanya mabadiliko.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Facebook:"Mzee Mwanakijiji"
 
Kazi kweli kweli! Ikifanyika hivi utawala huu kwishnei! Ila damu itaendelea kumwagikaaa, anyway labda itakuwa ni matambiko ya chama chetu pia kabla ya kuchukua nchi.
 
well said ingawa kwa kufanya uliyoyasema kwa wengine wataonekana CHADEMA kama wasaliti
 
Kazi kweli kweli! Ikifanyika hivi utawala huu kwishnei! Ila damu itaendelea kumwagikaaa, anyway labda itakuwa ni matambiko ya chama chetu pia kabla ya kuchukua nchi.

Hakuna damu itakayomwagika; itamwagika vipi wakati watu wako majumbani kwao; hawaandamani wala kufanya mikutano mikubwa?
 
upo sahihi kimtazamo lakini suala la mgomo baridi kwa Tanzania bado si muda muhafaka kwa sasa, bado kuna wananchi wengi sana bado hawaelewi nyuma ya pazia ya serikali yao, bado kuna watu wanaamini mabadiliko ya kimfumo kuwezekana. Umetoa mfano wa Martin Luther King, ulijaribu kusoma hali ya kisiasa ya wakati wake hadi kutumia passive resistance ilitumiwa baada ya mambo yapi kutokea? Mimi bado naamini viongozi wa CDM wapo sahihi na wanajua wanachokifanya.
 
Mkuu ni wazo zuri lakini aina hii ya sisi Watanzania bado hatuna jeuri hiyo.
 
Umeonyesha njia, me naanzia hapa nilipo. Ni upuuzi kuvumilia dhuluma hii ambayo ipo chini yetu.
 
Tatizo ni kwa CHADEMA, Wazungu wanasema the odds against them, wamelikoroga tangu Mwanzo, wameshindwa kuisoma Jamii yetu ikoje, hata wewe pia unafanya makosa yale yale kulinganisha Jamii mbili tofauti zisizolingana, Marekani na Tanzania, unaongelea Martin Luther sijui alivyofanya, hapa Tanzania hilo HALIWEZEKANI, kwanza Marekani ina mfumo tofauti na wetu, hapa kwetu Raisi ndio mkuu wa kila kitu, hapingwi wala haingiliwi na mtu yoyote, sasa unawezaje kuanzisha vita dhidi ya mtu kama huyo? Marekani Raisi anaweza kushitakiwa, kwetu je? Uelewa wa Watu wa Marekani ukoje ikilinganishwa na TZ?
Raisi akiamua kuifuta CHADEMA kesho, chadema watafanya nini, zaidi ya kwenda kuomba msaada kwa Wazungu, ambao tayari kwao CCM ni mfano wa kuigwa barani Afrika?
Eti unaongelea wamwambie Obama, hivi unafikiri Obama hajui yanayotokea TZ mbona yuko kimya? JWTZ Kongo wanafanya nini? wanalinda maslahi ya nani? British Gas wamepewa kibali kuchimba gesei, unafikiri Serikali yao itawasikiliza CHADEMA? Statoil ni kama TPDC ya Norway unafikiri watawasikiliza CHADEMA? Amnesty international hawajawahi kuilaumu Serikali ya TZ kwa lolote lile, nani ata wasilikiza CHADEMA?

Mfano mdogo tu Marekani ukiwaambia watu kesho watoke kuandama kupinga vita ya Syria watajaa watu mpaka utashangaa, hapa kwetu kuna watu tena ndio wengi hata maana maandamano hawajui, halafu usisahau kwamba CCM pia ina washabiki tena wengi tu, CHADEMA wakilianzisha pia CCM nao wanaweza kulianzisha, counter demo kama alivyofanya Erdogan wa Uturuki na ukichukulia CCM wana Serikali.

Hapa njia pekee ni kwa CHADEMA kujirudi kuwa wapole, na kujaribu kwenda pole pole, wajitahidi kuongeza viti Bungeni Uchaguzi kila baada ya Uchaguzi, ili mwishowe waweze kuwa na Wabunge wengi kama CCM, hapo sasa ndio wanaweza wakaleta mabadiliko ya kweli, lkn kwa sasa hv unaongelea Chama chenye Wabunge 40 dhidi ya CCM sijui 150 wapi na wapi? Na usisahau Propaganda ya Serikali ambayo inaweza hata kuwageuza baadhi ya Wanachama wa Chadema dhidi yao!

CHADEMA IS FIGHTING GOLLIATH!
 
Tatizo lilopo hapa nyumbani siyo tu ni la kiuongozi bali zaidi la kimfumo kwahiyo hata uliowataja wakiuzulu watakaokuja watafanya kama wale wanaotoka na pengine mbaya kuliko wale waliotoka. tutoke ktk mfumo ambao vyombo vya umma vinatumikia watawala badala ya wananchi. moja kati ya idea ninayoiona ni kutengeneza mfumo ambao utaviondoa vyombo vyote vinavyoshugulikia haki za wananchi wakiwemo polisi toka mikononi mwa wanasiasa ili kuvifanya vifanye kazi kwa mujibu wa taaluma zao.
 
Good idea Mzee Mwanakijiji, but remember you can't compare Tanzania with US poitically! The system here is devide destrory (kill) and rule them.

I strongly suggest that your idea is good and it came at the right time but at the wrong place!!
 
Last edited by a moderator:
Good idea Mzee Mwanakijiji, but remember you can't compare Tanzania with US poitically! The system here is devide destrory (kill) and rule them.

I strongly suggest that your idea is good and it came at the right time but at the wrong place!!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni kwa CHADEMA, Wazungu wanasema the odds against them, wamelikoroga tangu Mwanzo, wameshindwa kuisoma Jamii yetu ikoje, hata wewe pia unafanya makosa yale yale kulinganisha Jamii mbili tofauti zisizolingana, Marekani na Tanzania, unaongelea Martin Luther sijui alivyofanya, hapa Tanzania hilo HALIWEZEKANI, kwanza Marekani ina mfumo tofauti na wetu, hapa kwetu Raisi ndio mkuu wa kila kitu, hapingwi wala haingiliwi na mtu yoyote, sasa unawezaje kuanzisha vita dhidi ya mtu kama huyo? Marekani Raisi anaweza kushitakiwa, kwetu je? Uelewa wa Watu wa Marekani ukoje ikilinganishwa na TZ?
Raisi akiamua kuifuta CHADEMA kesho, chadema watafanya nini, zaidi ya kwenda kuomba msaada kwa Wazungu, ambao tayari kwao CCM ni mfano wa kuigwa barani Afrika?
Eti unaongelea wamwambie Obama, hivi unafikiri Obama hajui yanayotokea TZ mbona yuko kimya? JWTZ Kongo wanafanya nini? wanalinda maslahi ya nani? British Gas wamepewa kibali kuchimba gesei, unafikiri Serikali yao itawasikiliza CHADEMA? Statoil ni kama TPDC ya Norway unafikiri watawasikiliza CHADEMA? Amnesty international hawajawahi kuilaumu Serikali ya TZ kwa lolote lile, nani ata wasilikiza CHADEMA?

Mfano mdogo tu Marekani ukiwaambia watu kesho watoke kuandama kupinga vita ya Syria watajaa watu mpaka utashangaa, hapa kwetu kuna watu tena ndio wengi hata maana maandamano hawajui, halafu usisahau kwamba CCM pia ina washabiki tena wengi tu, CHADEMA wakilianzisha pia CCM nao wanaweza kulianzisha, counter demo kama alivyofanya Erdogan wa Uturuki na ukichukulia CCM wana Serikali.

Hapa njia pekee ni kwa CHADEMA kujirudi kuwa wapole, na kujaribu kwenda pole pole, wajitahidi kuongeza viti Bungeni Uchaguzi kila baada ya Uchaguzi, ili mwishowe waweze kuwa na Wabunge wengi kama CCM, hapo sasa ndio wanaweza wakaleta mabadiliko ya kweli, lkn kwa sasa hv unaongelea Chama chenye Wabunge 40 dhidi ya CCM sijui 150 wapi na wapi? Na usisahau Propaganda ya Serikali ambayo inaweza hata kuwageuza baadhi ya Wanachama wa Chadema dhidi yao!

CHADEMA IS FIGHTING GOLLIATH!

maneno ya kushindwa hayo mkuu.
Watu wa tanzania wanapenda haki na uhuru kama watu wa marekani hakuna tofauti hakuna binadamu yeyote duniani asiyependa kuishi huru na haki zake kulindwa on both sides. watanzania wanweza wasiwe na elimu kama wamarekani lakini when it comes to those important pillars mentioned above wote tunakuwa kitu kimoja.

chini ya uongozi wa chadema tumeweza kupata nafasi kujadili katiba yetu na mawazo yetu kusikiliza

chini ya chadema tumeweza kujua na kuona jinsi watawala wanavyoitafuna nchi yetu kwa chadema ku expose wizi bungeni

chini ya chadema wananchi tumeweza kutufumbua macho kujua haki zetu na namna ya kuzisimamia kwa wananchi kusimama

mashambani na mijini kuoji matendo ya viongozi wao.
 
Sio kweli uelewa ni kitu kikubwa sana, huwezi kulinganisha Jamii ya Marekani na Tanzania hata kidogo, huko ni kujidanganya na linalowezekana Marekani kamwe halitowezekana TZ kila nchi/jamii iko tofauti, na ndio maana wazungu kwa kuwa wana akili waliweza kututawala, huwa hawakurupuki kwanza wanaisoma jamii ikoje na ndio maana Ulaya kote na Marekani kuna watu wanasomea mambo ya Afrika na ni maprofesa, wanakuja kwetu wanakwenda kuishi vijijini, unafikiri ni kwa nini? wanatusoma halafu wanatuma ripoti kwao na kuishauri Serikali yao jinsi tulivyo, wanawambia Viongozi jinsi ya kudili na sisi, kwamba ukiwa Afrika kama Mzungu wewe ni kama Mungu na chochote unachosema kinaaminiwa, na Viongozi wao wanafanya hivyo hivyo!

Ndio maana unaona sisi kila kitu tunataka Mzungu kwanza ajue, Mleta mada anashauri tumwambie Obama, sasa wazungu wanalijua hilo, wengine wantaka Viongozi wa Chadema waende ubalozi wa Marekani au Uingereza kujisalimisha, sasa kwa nini?

Good idea Mzee Mwanakijiji, but remember you can't compare Tanzania with US poitically! The system here is devide destrory (kill) and rule them.

I strongly suggest that your idea is good and it came at the right time but at the wrong place!!

Mbona mnatutisha jamani; yaani CCM imetawala fikra za watu kiasi kwamba mtu akiamua kujikalia nyumbani kwake anahisi korokoroni ataenda kumchomoa na kumpeleka shambani? Hawa hawa watu ambao wanajiona wako wakati tofauti na wakati wa Nyerere? Hivi leo hii kuna watu hata wanaweza kuthubutu kuwafungia mabbosi wao wao wasiingie ofisini na wakabakia salama? si tuliyaona haya wakati wa Nyerere?

Au watu wanasahau kuwa watu wamewahi kuandaana hadi Ikulu ya Nyerere na hawakupigwa risasi Nyerere mwenyewe (na Kawawa) walikuja na kuzungumza nao? Au ni nini kimeingia kwenye vichwa vya watu wetu ambao wanalaani wakati wa Nyerere wakati inaonekana wanaishi kwenye wakati mbaya zaidi kuliko hata wakati unaodhaniwa mbaya wa Nyerere?
 
Mzee nakubaliana na wewe.
lakini tukio la Arusha na CDM mimi naona lina mafindofindo sana. Kwa nini vifo vyote ni vya kushambliwa na vyombo vya usalama na mara nyingi wanaokufa ni waliopo (kwenye mikutano) na wasiokuwapo (wapita njia)? Kwa nini wakati wa umaarufu wa NCCR -MAGEUZI na TLP hatukuwahi kushuhudia ukali huu wa polisi kutwanga wananchi risasi? Kuna uhusiano gani kati ya Nyerere kufa na ukali wa risasi kwa wananchi kuzidi? Mfano dhahiri ni juzi jumamosi - Hivi kuna kichaa gani (maana hatuhitaji mtu timamu) anayeweza kutuelewesha KUNA UHUSIANO GANI KATI YA BOMU KULIPUKA NA WANANCHI KUTWANGWA RISASI? (Maana majeruhi wengi pia walitokana na risasi za polisi). Hii inanipa kuamini kwamba kwenye mkutano wa juzi aliyekoswa na bomu risasi ya polisi ilikuwa ni halali yake!
Mimi naamini kuna kitu nyuma!
Kuna mtu atafaidika kwa Tanzania kuingia katika vurugu.huyu mtu ndiye anayetawala ama kuongoza mambo haya machafu! huyu mtu ama kikundi wamejaribu kila njia ili watanzania tuvurugane lakini kwa umoja wetu tumekataa. Ukiangalia shambulio la Kanisani lililenga kuleta vurugu kwa njia za dini lakini ikashindikana. Kwa mtindo uleule akaamini akishambulia mkutano wa CDM kwa sababu ya jazba za wana CDM vurugu zingeanza na yeye ama hicho kikundi kingefanikiwa. Kwa mara nyingine watanzania wakakataa. Hakika kuna bomu la tatu linakuja! Mimi naamini na naziamini hizi hisia zangu kwamba tuendelee kuwa wapole kwa mda kidogo sana na tutajua mwisho wa haya yote. Amini usiamini mimi naamini kwamba nyuma ya mpango huu NAPE NNAUYE na LUKUVI wanajua. Ndio maana walikuwa wa kwanza kuongea upuuzi. Lakini pia naamini hata ndani ya CDM kuna watu wanahusika!Mpaka polisi wanashambulia raia ni mpango tu wa watu kujitafutia madaraka! Hivi kweli ilikuwa ni bahati mbaya MBOWE kushuka jukwaani na bomu kulipuka? hisia zangu zinaniambia Hata Mbowe anaweza kuwa anajua. Lipumba? tusubiri tuone lakini more are yet to come! kuna consipiracy kubwa sana hapa!

kila kitu kinawezekana hakuna cha kuogopa kitu.

Umesema sahihi.
Watu hawajui hata hizi dini zetu zilivyoasisiwa, Mitume walipambana na kila ubabe wa dola zilizowabana, mfano ni jinsi Mtume Muhamad(S.A.W) alivyopambana na Koreish waabudu vinyago pale Makka, mpaka akawang'oa... Hali kadhalika Yesu Kristo anakuta watu wamenogewa na TORATI, lakini alipambana, hata alipoteswa ndo kwanza watu wakaendelea kumfuata. CCM itang'oka tu ikiwa sote tutaungana kuitoa. Ikumbukeni Tunisia, ambayo haikutarajia kumng'oa Ben Ally lakin kama upepo akasepa. Misri na Tunisia vivyo hivyo
 
Sio kweli uelewa ni kitu kikubwa sana, huwezi kulinganisha Jamii ya Marekani na Tanzania hata kidogo, huko ni kujidanganya na linalowezekana Marekani kamwe halitowezekana TZ kila nchi/jamii iko tofauti, na ndio maana wazungu kwa kuwa wana akili waliweza kututawala, huwa hawakurupuki kwanza wanaisoma jamii ikoje na ndio maana Ulaya kote na Marekani kuna watu wanasomea mambo ya Afrika na ni maprofesa, wanakuja kwetu wanakwenda kuishi vijijini, unafikiri ni kwa nini? wanatusoma halafu wanatuma ripoti kwao na kuishauri Serikali yao jinsi tulivyo, wanawambia Viongozi jinsi ya kudili na sisi, kwamba ukiwa Afrika kama Mzungu wewe ni kama Mungu na chochote unachosema kinaaminiwa, na Viongozi wao wanafanya hivyo hivyo!

Ndio maana unaona sisi kila kitu tunataka Mzungu kwanza ajue, Mleta mada anashauri tumwambie Obama, sasa wazungu wanalijua hilo, wengine wantaka Viongozi wa Chadema waende ubalozi wa Marekani au Uingereza kujisalimisha, sasa kwa nini?

unaelekea unaitaji crash course ya civics
katika mada yangu nimezungumzia issue mbili haki na huru ambazo kila binadamu hapa duniani anazitaka kuishi ndani yake. hakuna binadamu anayetaka asitendewe haki iwe anaishi marekani au pangoni na vile vile kila binadamu angependa kuwa huru kwa kujiamulia mambo yake mwenyewe hata binadamu huyo anaishi mitaa ya san francisco au manzese kwa mfuga mbwa. kila linalowezekana marekani pia linawezekana Tanzania labda ungetoa mifano ya vitu unavyomaanisha kwamba vitu hivi vinawezekana marekani ambavyo Tanzania hata kama mna dhamira hamuwezi kuwa navyo
 
Back
Top Bottom