CHADEMA (Dr Slaa) afuate nyayo za CUF (Maalim Seif) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA (Dr Slaa) afuate nyayo za CUF (Maalim Seif)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HM Hafif, Mar 4, 2011.

 1. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika kabisa kuwa CUF ni chama kikongwe cha siasa kilichopitia misukosuko mingi sana ikiwa pamoja na viongozi wake waandamizi kuwekwa ndani kwa takriban zaidi ya miaka miwili kwa kusa la kutaka kupindua nchi.

  Vile vile ni chama kilichotia tashtiti nyingi sana na hata pamoja na uchakachuaji wa kura walieza kufikisha zaidi ya asilimia 48 ya kura za urais Zanzibar.

  Katibu wake mkuu Maalif Seif Sharif hamad ni mtu aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali mpaka kuwa waziri kiongozi na amepata misukosuko mingi sana na mtu mwenye kauli kubwa.

  Kwa hakika napenda kumsifu kwani Kwa yeyote anayeijua na kumjua maalim Seif especially wakati wa uchaguzi utajua kauli yake ni muhimu sana katika mustakabali wa Taifa la zanzibar. mara zote aliweka maslahi ya taifa mbele japo walikuwa wanaporwa ushindi wao.

  Ushauri wangu kwa Chadema ingekuwa Busara zaidi Dr Slaa akapata au kufuata nyayo za maalim Seif hususan anapoingia kwenye maslahi ya Taifa.

  Inaeleweka wazi kuwa hajawa maarufu kama maalim Seif lakini ni vizuri kupata Uzoefu kutoka kwa maalim ambaye amepitia misukosuko mingi au Chadema nzima kama ingekuwa wasikivu wangefuata nyayo za CUF katika kutaka kuleta muafaka halisi wa nchi hii ya tanzania na sio kuleta mifarakano na uchochezi jambo linaloweza kuleta machafuko na umwagaji damu.

  Chadema fuateni nyayo za CUF katika kuleta yale mema mnayoyataka wananchi wa tanganyika wayapate.

  Nawasilisha.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  vipi ghahawa inastimu????
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hivi maalim seif kumbe ni maarufu! Mimi nilijua ni mpemba tu kama mimi nilivyo mbara!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  asubuhi umepata uji?
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Katika katiba ya Tanzania Maalim Seif ni nani!!??
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Kwanini waige chama cha mkoa kata (zanzibar)?
  Kwani chadema imeanzishwa mwaka gani?
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ni mke kiongozi wa Rais Shein ,anasimamia 1.Mazingira 2.The need group 3.Vita dhidi ya ukimwi 4.Mihadarati
  Akisafiri rais nchi inakuwa chini ya Makamu wa pili.
  Hatambuliki kwa waelewa ila wanywa ghahawa na wacheza bao ambako hawajui umuhimu wa kustick kwenye katiba.
   
 8. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  .....sikubaliani na wewe asilimia mia moja!
  labda ungeorodhesha mambo ambayo unadhani huyu Dr. Slaa(Phd) anayafanya ambayo unadhani yanaenda kinyume na sheria na sio kuanza kufananisha tembo na sisimizi!!!!
   
 9. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  heri ungenyamaza kimya coz huna ulijualo wala huju ulio otherwise uniambie wewe ni kibaraka wa mafisadi
   
 10. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we wa wapi wewe kumfananisha Dr slaa na maalim Seif ni sawa na Kumfananisha Mrisho Ngasa na Messi sasa wapi na wapi wewe jiheshimu na acha chuki binafsi wewe
  "Kama wewe sio Mdini basi ni Fisadi"
   
 11. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtasema mengi sana lakini sikio haliwezi hata kidogo kuzidi kichwa.

  CUF ni wakongwe na wakomavu katika siasa za nchi hii sio Chadema. Kwani ili kuweza kujikita na japo kufikia hata nusu ya CUF katika kura za uchaguzi wa rais na Wabunge katika Tanganyika, Chadema lazima wapate uzoefu wa CUF kinyume chake ni propaganda tu na kuleta machafuko.
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Angalia watu wa kuiga bana sio Chama cha Ufinyanzi na Fumigation (CUF)

  _51515556_011433892-2.jpg
   
 13. M

  Marytina JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Yahe hiyo ghahawa kapika akiwa uchi mbona kama imekupa stimu??
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Maalim Seif ni Zaidi na hilo nimeliweka bayana. Kwani ukiondoa PhD ya sheria za kikatoliki na Kuongoza kigango na jimbo la katoliki na ubunge ni wadhifa gani aliowahi kushika Dr Padre Slaa.

  Sasa mfananishe na maalim Seif. Sasa ni lazima akajifunze kwake ajue kuwa katika harakati hizi kuna kuwekwa ndani, kufungwa na mengi mengine ambayo Seif ameyapitia mpaka kuleta muafaka wa kweli Zanzibar. Au wewe unafikiri Rome watakutetea ukiekwa ndani. wao watakupa pesa lakini ndini ni wewe tu wao hawamo.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Aliyefuata nyayo za Maalim Seif na "akafanikiwa" kama yeye ni Dr Mohamed Ghalib Bilal, makamu wa JK.
   
 16. M

  Marytina JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata kikwete alikuwa na mivyei kibao kabla ya 2005 sasa ametufanyia nini?
  Nyerere alikuwa na hayo mavyeo ya Maalim 1961?
  Huyo lipumba ni cheo gani cha siasa zaidi ya ugombea urais wa maisha alichowahi kushika.
  Mivyeo haina maana kama hamna uzalendo.

  Mwambie JK aende pale IMAN ya kiislam redio aongee kiarabu kwa waislam nini cha kufanya.
   
 17. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ''Any man who reads too much and uses his own brain too little falls into lazy habits of thinking''. Albert Eistein
  Inaonekana unatumia nguvu nyingi sana kurejea kwenye historia ya Cuf unguja bila ya kujaribu kui-relate na hali ya sasa kwa CDM na wananchi wa bara na kwingineko duniani pamoja na hali zao!
   
 18. kyemo

  kyemo Senior Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nawasihi msichangie hii thread wanajf coz watu wengine wanatafuta umaarufu kupitia migongo ya watu au hawana cha kupost,ni heri utumie muda huo kuangalia tom&jerry unaweza ukaongeza maisha kwa kufurahisha moyo wako
   
 19. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ebu tudokeze Dr Slaa ana PhD ya nini vile.
   
 20. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hebu tupe hali ya sasa kisiasa ya chadema ambayo tuione tofauti na ile ya CUF kule Zanzibar? kama wewe sio mzandiki.
   
Loading...