CHADEMA, do the talk | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, do the talk

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Speaker, Apr 29, 2012.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Toka mwaka 2005 tumekua tukimsikia Mbowe akiongelea swala la
  "uongozi wa majimbo".

  Juzi hapa bungeni pia ali penyeza wazo la chadema kwamba
  ili matatizo mengi yaliyopo kwenye serikali leo hii yaweze
  kuisha inabidi serikali i-adopt mfumo wa majimbo katika uongozi
  wake.

  Wapo walio chambua hapa juu majimbo hayo yagawanywe vipi,
  umuhimu wake,na nchi gani zinafanya hivyo pia na vipi ume saidia.

  Tatizo langu mimi liko kwa chadema hawa hawa wanao hubiri
  mfumo wa majimbo wakati hata HAWA UFANYII MAZOEZI.

  Leo nimesoma mada Allen Kilewella akielezea uchaguzi wa "mwenyekiti"
  wa mkoa wa Iringa.

  Katika topic hiyo akachangia pia Josephine akidai mgogoro wa Iringa
  hautadumu sana maana Mkoa wa Iringa utagawanywa hivi karibuni yaani kutakua
  na Iringa na Njombe,....kwa maana nyingine Chiku Abwao na Thomas Nyimbo wata
  gawana "ulaji" baada ya JK kuleta "wazo takatifu".

  Sasa chadema mnacho fanya ni nini?
  Mnacheza ngoma gani tofauti na CCM?
  mbona kwanzia upikaji hadi ukombaji wa mboga ni sawa kabisa na CCM?
  Kwamba CCM wakigawanya mikoa,basi na chadema ina gawanya "mikoa" kiuongozi?

  kwanini msinge tumia mfumo wenu wa "majimbo" hapa, ili awepo mwenyekiti wa
  chadema jimbo A,...au Balozi wa chadema jimbo B etc?

  Sasa kwa style hii kuna chochote kipya kitakacho patikana pale chadema itakapo
  chukua uongozi wa nchi?

  Maana msingi wa uongozi kichama ndio reflection ya jinsi mtakavo ongoza
  taifa,mfumo wenu ni sawa kabisa na wa CCM,....na sina shaka umebeba ufisadi
  kibao ndani yake.

  Hapa tuna danganyana tu,ni sawa na JK kubadili baraza la mawaziri katika mfumo ule
  ule na watanzania waka shangilia kubalika uongozi.

  Chadema onesheni kwamba sera ya majimbo mnayo ihubiri ni practical,...

  DO THE TALK,DON'T TALK THE DO.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwanza kabisa ni muhimu kutambua msemaji wa chadema mkoa wa Iringa katika issue uliyotaja ni Allen, huyo Josephine ni nani katika Chadema hadi umtumie kujenga hoja yako? Umeisoma katiba ya chadema au umesoma ya ccm na kudhani ndiyo ya chadema!?

  Unafahamu mfumo wa kuendesha chama cha siasa katika nchi zinazotumia mfumo wa kuwa na serikali za majimbo? Unapaswa kufahamu kwamba kuwepo kwa majimbo hakuondoi mikoa na wilaya, huo ni mfumo mzuri zaidi wa kushusha madaraka ya kuendesha serikali kwa wananchi wenyewe na kuweza kuisimamia kwa ukaribu zaidi.

  Kwahiyo mkuu usijichanganye ama kuchanganywa na mfumo wa serikali ya majimbo vs mfumo wa uongozi wa chama cha siasa.
   
 3. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mura Amang'ana! Mbuuya waraye!

  Hapo pekundu Chadema wasipoangalia ipo siku historia itajirudia. Delila na Samsoni, Ever na Adam, mimi na Mke wangu, nk. mwenye ufahamu ataelewa nini namaanisha hapa.
  TELO.
   
 4. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama hujisomi hv..
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  magamba at work...
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  Hapana mkulu mtoa mada ana pointi
   
 7. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna hoja,,,,ni vyema kutafakari,./majimbo ni muhimu,,,,onyesha inawezekana//haileti ukabila wala ubaguzi///anza na chama,,watu waone...thankx:yo:
   
 8. B

  Benaire JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Naomba uelewe kuwa kuna tofauti kati ya serikali na chama cha siasa.....kwanza mapendekezo ya serikali za majimbo ni kwa lengo la kutoa mamlaka kwa majimbo kujiongoza kiuchumi na kiushindani kwa kuzingatia theory ya comparative advantage...pia hii ita-influence inter provice trade na kusaidia ku-control na kuregulate mapato ya jimbo.
  Pili chama cha siasa kinaongozwa kwa kufuata sheria ya vyama vingi chini ya msajili wa vyama vya siasa....chama kinatakiwa kuwa na wanachama kutoka kila mkoa...howcomes mkoa huo usiwe na kiongozi?
  Mwisho chama cha siasa sio serikali....Mbowe alipendekeza serikali za majimbo na sio uongozi wa chama kwa mfumo wa majimbo...hope you will not misunderstand.
   
 9. k

  kindafu JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana na wewe mkuu kuwa kuna haja ya kujadili hii hoja ya Majimbo! Nilianzisha uzi hapa nikawaomba viongozi wa Chadema watuwezeshe kutembea pamoja kwa kutuainishia taswira waliyo nayo ya kuigawa Tz i.e Majimbo yatakuwa mangapi na mipaka yake ki-Jiografia itakavyokuwa nk nk. Kwa bahati mbaya hamna kiongozi yeyote aliyejitokeza kutufafanulia hilo!! Ni vema uongozi ukaweka mambo bayana mezani yakafanyiwa "panel beating" ya kutosha mapema kabla hatujaingiza watu Ikulu na wakishaingia huko wakatugeuka na kutuletea mambo ya kuwawezesha kudumu huko Ikulu!!!
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hizi ni comment za watu wenye Upungufu wa Akili Kichwani (UAK)
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Red: Leo amegeuka kuitwa "ni nani katika chama" eh?

  Blue: Ni kazi sana kutetea udhaifu maana bado utaonekana.
  Hoja yangu ni kwamba kwanini hawa fanyii mazoezi hoja yao ya majimbo?
  Kama kuwa na majimbo hakuondoi wakuu wa mikoa (wenyekiti wa mikoa kwa sasa kichama) hakuna
  maana ya kuwa na majimbo maana ni kuongeza gharama,.....na hata kama ni muhimu,...
  kwanini chadema hawaoneshi kuwa na viongozi wa kimajimbo sasa? hili ndio swali la msingi hapa.
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante sana,sina uhakika kama siku itaisha haujapewa ban lakini.
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asanteni,hapa unachoweza kuona ni kwamba sera ya majimbo haiwezekani
  ndio maana haitekelezwi hata katika msingi wa kichama.

  Badala ya chadema kuonesha watatoa tofauti gani kama chama katika kuongoza
  serikali,wao wanafuata msingi ule ule wa ccm ambao umesha zoeleka na
  hauwezi kuleta tofauti yoyote ile kiutendaji.

  Huwezi kusema unaweza kuendesha gari kwa kujifunzia kuendesha kwenye
  play station.
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sikatai wasiwepo viongozi wa mikoa,lakini nachotaka kujua ni
  nini kina zuia wasiwepo viongozi wa chama kijimbo?
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hapa ndipo kwenye hoja ya msingi:clap2:
   
 16. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  This is a "loud speaker" and not a "speaker"; as it amplifiers what the "speaker" says. Ask yourself, who might be a "speaker"?
   
Loading...