Chadema Digital yazidi kuchanja mbuga, Yaingia Kasumulu Jimbo la Kyela

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,237
Ule mpango wa Kisasa wa Kusajili wanachama wa Chadema unaoitwa CHADEMA DIGITAL umeendelea kusonga mbele kwa mafanikio makubwa sana, Na sasa umeingia boda ya Malawi kwenye kijiji kinachoitwa Kasumulu.

Kwa Wasioelewa vizuri kuhusu Kyela ni hivi, Kasumulu ndio kijiji cha mwisho kabisa kabla hujavuka daraja na kuingia Nchi ya Malawi , hiki ndio kijiji cha kwanza kabisa Wilayani Kyela kuiteketeza ccm , kwa faida ya watu wa Mjini na wanajf wengine ni kwamba , unapovuka kutoka Malawi kuingia Tanzania Bendera 5 za mwanzo unazokutana nazo ni bendera za Chadema , Jambo lililosababisha Baadhi ya Raia wa Malawi kudhani Bendera ya Chadema ndio bendera ya Taifa la Tanzania.

Leo Naibu Katibu Mkuu Salum Mwalimu ameongoza Usajili wa kidigital Kijijini hapo, ambako umati mkubwa wa Wananchi umehudhuria bila kujali Msimu wa kilimo cha mpunga unaoendelea.

Naibu_Katibu_Mkuu_Zanzibar_Mhe._Salum_Mwalim_akiendelea_na_ziara_ya_uhamasishaji_wana-Chadema_...jpg
 
Welldone dunia ya sasa ni technology kwa sana!lini nchi hii yetu tutanza kufundisha coding kwenye mashule yetu!
 
CHADEMA ipo ndani ya mioyo ya watu. Ingekuwa CHADEMA ipo kwaajili ya maslahi, ingekuwa amekufa zamani.

CCM muda mwingi imekuwa inafanya iharamia ili kuwakatieha tamaa wapenzi wa CHADEMA ili wakate tamaa, likini ndiyo kwanza inawazidishia ari, mshikamano na maendeleo zaidi. Kadiri CCM inavyowafanyia uovu, ndivyo CHADEMA inavyozidi kuimari zaidi.
 
Hakika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom