meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,394
- 4,748
Wasalaam...
Kwa furaha kabisa napenda kusema kuwa mimi nilikuwa PRO CDM au PRO Slaa kabla ya gia za angani kupanguliwa.
Nasikitika sana kuona Gia za Angani zilivyopelekea maafa makubwa ya kisiasa ya Chama cha upinzani kilichovumilia mikikimikiki mikubwa kutoka kwa CCM kwa miaka takribani 20 lakini kikaufyata mkia ndani ya kipindi cha chini ya mwezi mmoja kwa mwanaCCM aliyekatwa na CCM.
Hayo ni masikitiko ya wengi hasa hasa kwa wale wanaoitwa Chadema Asilia.
Uteuzi wa katibu mkuu wa 'MAJARIBIO' wa Chadema ni kituko kingine cha kisiasa nchini baada ya kile cha kupokea yule aliyeimbwa kama fisadi na kumfanya kuwa mgombea wao,Namuita katibu mkuu wa majaribio kwa kuwa ni wazi ndani ya kipindi cha muda mfupi tu mwenyekiti Itabidi arejee tena akiwa na jina la katibu mkuu haswa mwenye haiba,weledi,uzoefu,ushawishi na msimamo unaoendana na ukatibu mkuu sio tu wa chama cha siasa bali wa Chama cha siasa kinachoendesha siasa za kiharakati.
Ni katibu mkuu wa majaribio kwa kuwa kasi iliyofikiwa na Chadema kipindi Dr Slaa akiwa katibu mkuu ilikuwa ni kasi yakipekee...ilikuwa ni kasi iliyowaamsha CCM na kuja na operesheni vua gamba....ilikuwa ni kasi ya kufa mtu iliyofanya CCM ibadili safu za uongozi....
ilikuwa ni kasi ya ajabu iliyomfanya Kinana na Nape waanze utalii wa ndani!!
Kiufupi naweza kusema Dr Slaa ali-set standards ndani ya Chadema kiasi cha kuanza kuona makatibu wakuu wa Chadema wakiongea ama wakitenda mithili ya Dr Slaa.
Inawezekana Mbowe amemuweka katibu mkuu kwa jicho la ukanda yaani akijaribu kuiteka kanda ya ziwa....ingawa aliyemuweka hana ushawishi wowote katika kanda hiyo.
Inawezekana Mbowe amemuweka Msomi ili avute wasomo lakino pia ni ukweli usiopingika kuwa jamaa hana ushawishi kwa wasomi wa kada yake,hana ushawishi wa kitaasisi ya usomi mithili ya alivyo Baregu au Kitila Mkumbo.
yaani CV yake inataka kulazimishia usomi wakati sio msomi kihivyo!...Nimepenyezewa kuwa hata huo udaktari bingwa alioundika kwenye CV yake hakufanikiwa kuumaliza(MMED ANAESTHESIOLOGY)
Chadema imepiga gia nyingine ya anga na itaangukia pua kama ilivyoangukia pua oktoba 2015.
Kwa bahati mbaya sana wakati Chadema inafanya majaribio ya SG ,CCM inazidi kubebwa na jeshi la mtu mmoja ambaye ni mwenyekiti mtarajiwa JPJM.
Yaani ungeniuliza ni kipindi gani chadema walitakiwa kufanya majaribio basi ningesema ni vipindi vyote ila isiwe kipindi hiki cha Magufuli.
VIATU VYA DR SLAA HAVIVALIKI!!!!