CHADEMA Corona si muhimu tena mjitazame upya muda mchache

CHADEMA Corona si muhimu tena mjitazame upya muda mchache

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,439
Reaction score
38,118
Heshima kwenu wanajamvi,

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Mbowe amekuwa mstari wa mbele kupigania taifa liingie katika kile kinachoitwa LOCKDOWN lugha ya Malkia.Ni wazi Mh Mbowe amepigana kweli kweli lakini pia ni vyema akafahamu kwamba policy ya LOCKDOW si popular miongoni mwa wanachi wengi wa Tanzania kwa sasa wala hata kuwa na uwezo wa kubadili chochote.

Ningependa kuwashauri CHADEMA kwa sasa wajikite kuuelezea umma wa waTanzania fedha za ruzuku (Ingawa nafahamu ipo report ya CAG) na fedha za michango ya wabunge zilivyotumika.

Narudia tena lazima CHADEMA watoe maelezo ya kina namna fedha za michango ya wabunge zilivyotumia na zitakavyotumika kama bado zipo.Ni vizuri viongzi wa CHADEMA wakafahamu kwamba katika wabunge wote waliojiondoa chamani Mbunge Peter L kajiondoa kwa style tofauti kidogo tena kaondoka na hoja ambazo zisipojibiwa vizuri zitakwenda kukiumiza chama katika kiwango ambacho hakijawahi kutokea.

Mwisho tangu mwanzo tulishauri suala la kuhangaika na wabunge watukutu wakati huu ambao tumebakiza muda mchache kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu halikuwa na mashiko wala sababu za maana.

a. Mimi kama mwananchi wa kawaida nilijua hata mkiwafukuza speaker a gewakingia kifua.
b. Nilijua Wabunge waliofukuzwa walikuwa na nafasi ya kwenda mahakamani kupinga kufuzwa kwao,na wangeomba mahakama wasitishe kufukwa kwao hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.Kumbuka bado week chache bunge linavunjwa kupisha uchaguzi mkuu.
c. CHADEMA walipaswa kujua ikiwa CECIL karejeshwa na SPEAKER wakati alishajiondoa mwenyewe chamani,Ni wazi walikuwa wanapoteza muda,kuwachosha wanachama wao na migogoro isiyokuwa na sababu.
d. Mimi si mwanasheria lakini nafahamu huwezi kumwadhibu mtu bila kumpatia nafasi ya kumsikiliza.Hii kesi ingekwanda mahakamani kwa hakika wabunge watukutu wangeshinda kesi asubuhi na mapema.
e. CHADEMA imeshaumizwa sana nilitegemea hekima,maarifa na weledi ungepewa nafasi ya juu sana hasa tukizingatia majira na nyakati.Maamuzi ya kamati kuu yalikuwa ya hovyo hata kama kulikuwa na matatazo ya aina gani lakini CDM walipaswa kufahamu walitoa nafasi ya wazi ya kuendelea kuumizwa pasipo kuwa na sababu za msingi.

Nadhani KAMATI KUU ya CHADEMA imekosa watu aina ya Prof Safari.......Wapo watu wanaoongozwa na umimi hata kipindi hiki ambacho wanajua wanapaswa kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa yao.
 
Mbowe analilia lockdown Kwasababu wana lipwa na serikali Sisi Watanzania tuliowengi tunachapa kazi

Chadema inakufa kwa aibu sana
 
Mbowe analilia lockdown Kwasababu wana lipwa na serikali Sisi Watanzania tuliowengi tunachapa kazi

Chadema inakufa kwa aibu sana

Mkuu Bia yetu watu tunapuputika kweli kweli,vituo vya COVID 19 wataalam wa afya wanawaogopa wagonjwa nadhani vifaa vya kinga ni haba.

Nani atapenda kufa kwasababu ya kuwahudumia wagonjwa wa CORONA !.Wagonjwa siku hizi wanajitibia nyumbani ukifa unazikwa chap hakuna kutangaza.
 
Back
Top Bottom