CHADEMA chatoa ushahidi kuhusiana na Green Guard

CHADEMA chatoa ushahidi kuhusiana na Green Guard

Green Guard sio sawa na Red Brigade. Kama CHADEMA wanataka iwe sawa, basi wafuate utaratibu kama wa UVCCM wa kuwakuza chipukizi, lakini CHADEMA wanabeba majambazi na wahuni mtaani ambao tabia zao zimeshindikana, eti ndio wanaunda kikosi cha kujilinda kwa utaratibu huu. Kikosi cha CHADEMA hakikubaliki.

995910_521683421218587_118609687_n.jpg


Hadi mtoto wa mkuu nae anakagua
 
IQ Ndogo shida kweli.

Mkuu nafikili hata shule za kata zinachangia katika hili!! Watanzania tunacho hitaji/taka ni amani na utulivu wa kudumu na sio propaganda za kuhadaa wananchi kwa ku-copy na ku-paste maelezo kutoka Wikipedia mkiwa na nia ya ku-exploit ignorance ya Watanzania walio wengi. Nani kawambieni Red Brigade ya Italy kilikuwa ni chama cha upinzani au itikadi yoyote ya kisiasa! Wale walikuwa ni vijana ambao hawakutaka nchi yao ijiunge na NATO, narudia - TAIFA lao lisijiunge na NATO ni hilo tu hawakuwa na itikadi zozote za kisiasa, sasa naona hapa kuna baadhi ya wana JF wanafanya makusudi kupotosha Watanzania wenzao!!

Jamani eh, kama ni kujifunza ukakamavu tumekwisha fufua JKT, hukuna haja ya vyama vya siasa kuendeleza/kuendekeza vikundi vya ulizi, mnavig'ag'ania ili vifanye kazi gani? Saa hizi tunajiona ni wajanja sana lakini kadiri siku zinavyo kwenda na matukio yasiyo ya kistaarabu yaendelea kushamiri, tukae tukijua tuna draw an International Community wawe na interest ya kujua kwa undani ni nani ma Engineer wa zahama zote hizi zisizo za kawaida katika ndani ya TAIFA letu, narudia - tusipo kuwa makini tunavyo ji-conduct kama Taifa, tutakuja kuhaibaka vibaya sana siku za usoni na heshima yote kuhusu TAIFA letu itakwenda na maji. Nawaobeni tusahau mambo ya itikadi za vyama kwanza, tukumbuke mshikamano wa Kitaifa ni paramount; who knows labda Mh.Kagame amekwisha nusa mifarakano hii ya kijinga ndani ya Taifa letu ndio maana anakuwa na guts za kusema/kutenda apendalo. Mambo tu ya kupenda madaraka kupindukia ndio usambaratishe TAIFA LETU??
 
Mkuu taffu69 ndani ya katiba ya CCM hakuna hata mstari mmoja unaohusu kuwepo green guards. Wameshikwa pabaya sasa wanaweweseka huku na kule hata yule DHAIFU anazungumza hadharani eti CHADEMA kutaka kuanzisha vikosi vyao vya kujilinda ni uvunjifu wa amani wakatu huo huo hajazungumzia lolote kuhusu CCM kumiliki green guards ambayo tayari imeshaanza kujihusisha na uvunjifu wa amani sehemu mbali mbali nchini dhidi ya CHADEMA. CHADEMA songa mbele katika kuanzisha vikosi vya kujilinda kila kona nchini dhidi ya uhuni, ujambazi, uonevu wa kila aina unaofanywa na polisi magamba, green guards na hata jeshi.

Ni vyema ccm ingeweka wazi green guard imeelezewa wapi kwenye katiba ya chama hicho. Kama kundi hilo halijaelezewa kwenye katiba yao, wauambie umma wa Watanzania green guard imeanzishwa kwa kuzingatia sharia ipi; imesajiliwa lini na maudhui ya kundi hilo ni yapi.

Kushindwa kwa ccm kutoa ufafanuzi huo kutadhihirisha wazi kuwa green guard wanayoitetea haina tofauti na magenge ya wahuni na wahalifu kama MUNGIKI la nchini Kenya ambalo limekuwa likijihusisha na uhalifu uliokidhiri kwenye maeneo ya jiji la Nairobi.

MUHIMU: Kwa kutambua jinsi ccm inavyoongozwa na kushauriwa na watu waliobeba vichwa vilivyojaa tope na wasioweza kujishughulisha japo kidogo, ni vyema wakatambua kuwa;

  1. Kwenye katiba ya chama hicho iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 hakuna sehemu yoyote inayozungumzia green guard
  2. Kwenye katiba hiyo maneno "green guard" hayamo kabisa;
  3. Neno "kijani" limetajwa mara moja tu likiwa linaelezea rangi ya bendera ya chama hicho na sio kundi tajwa

Kwa msingi huo, Green Guard haipo kihalali na ni muhimu kundi hilo likatambuliwa kama moja ya makundi ya kihalifu yaliyoanzishwa kwa siri ndani ya nchi yetu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu taffu69 ndani ya katiba ya CCM hakuna hata mstari mmoja unaohusu kuwepo green guards. Wameshikwa pabaya sasa wanaweweseka huku na kule hata yule DHAIFU anazungumza hadharani eti CHADEMA kutaka kuanzisha vikosi vyao vya kujilinda ni uvunjifu wa amani wakatu huo huo hajazungumzia lolote kuhusu CCM kumiliki green guards ambayo tayari imeshaanza kujihusisha na uvunjifu wa amani sehemu mbali mbali nchini dhidi ya CHADEMA. CHADEMA songa mbele katika kuanzisha vikosi vya kujilinda kila kona nchini dhidi ya uhuni, ujambazi, uonevu wa kila aina unaofanywa na polisi magamba, green guards na hata jeshi.

Nafikiri sasa ni muda sahihi kabisa kwa wanasheria makini (Prof. Safari, Mhe. Lissu, Mabere Marando) kulichukulia suala la GREEN GUARD ya CCM kisheria na kwa uzito unaostahili kwani ni wazi kuwa hili kundi limeundwa kinyemela pasipo kufuata taratibu, kanuni na sharia za nchi kwa minajili ya kupanga na kutekeleza mipango ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuteka, kutesa na kuua watu.

Ni dhahiri kabisa pasi na shaka kuwa kelele zinazopigwa sasa na watawala wa ccm kuhusu ugaidi ni njama za wazi za kuwapumbaza Watanzania kuwa kuna ugaidi unaendeshwa nchini ilhal ugaidi huo unafanywa na kundi walilolianzisha kinyemela kwa jina la green guard.

Nashauri wanasheria wachukue hatua za haraka kuhakikisha kuwa CCM na Green Guard yao inafunguliwa mashtaka ya kujihusisha kwa vitendo vyenye viashiria vya ugaidi ndani ya JMT kwa kuanzisha na kuendesha makundi yenye mlengo wa kigaidi kinyume na sheria za nchi yetu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kweli kabisa! CCM watauza hii nchi ili mataifa makubwa yawasaidie kubaki madarakani.Kupitia kulazimisha kwa CCM kubaki madarakani lazima tuchague moja, ama kulazimisha haki zetu bila kujali matokeo au tuwaachie nchi wafanye watakavyo wao!

it may be too late... keki imeshagawiwa, na yoyote mpya anonekana ni mharibifu... kauli ya mkapa ni tosha kuonyesha panya buku wamegawana cheese yote na hawataki kusikia cha nini wala nini

Mkapa, Rais mpuuzi aliyeregista kampuni kwa address ya IKULU hata yeye anapata courage ya kukosoa watu asiowajua.

ANASEMA WAPINZANI WACHANGA WAKATI YEYE ALIHITAJI MBELEKO YA NYERERE KUPATA UONGOZI HATA NDANI YA CCM, NA ALIONDOKA URAIS AKIWA BADO HAJA-MATURE, HUWEZI KUMATURE HALAFU UKAFUNGUA KAMPUNI KWA ANUANI YA IKULU

HIYO NDIO TANZANIA,
 
Green Guard sio sawa na Red Brigade. Kama CHADEMA wanataka iwe sawa, basi wafuate utaratibu kama wa UVCCM wa kuwakuza chipukizi, lakini CHADEMA wanabeba majambazi na wahuni mtaani ambao tabia zao zimeshindikana, eti ndio wanaunda kikosi cha kujilinda kwa utaratibu huu. Kikosi cha CHADEMA hakikubaliki.

Kwanza The Hague inawasubili.

Pili kama unadhani Chadema inaweza ikatumia watoto wadogo kwenye ulunzi Wa chama basi umenoa. Chadema inaheshimu haki za binadamu Na haki za watoto.

Tatu Kama unadhani wanachama Na wapenzi Wa Chadema ni wahuni basi subiri siku utapata Jibu.
 
Terrorist Organization Profile:


Red Brigades
Mothertongue Name: Brigate Rosse (BR)
Aliases: Armed Communist Combatants, Italian Red Brigade, Red Regiments
Bases of Operation: n/a
Date Formed: 1969
Strength: Group is inactive
Classifications: Communist/Socialist
Financial Sources: Unknown
Founding Philosophy: The Red Brigades were founded on rigidly Marxist-Leninist principles. This radical leftist group advocated violence in the pursuit of class warfare. Concentrated in Italy, the Red Brigades targeted businessmen and politicians and were a notable terrorist threat in Italy during the 1970s and early 1980s. Due to developments during its existence, the Red Brigades took on some qualities of anarchist groups while still propagating its especially virulent and violent Communist philosophy. In the end, the Red Brigades' increasingly brutal attacks eroded the support of those sympathetic with the group's Communist ideals.
Current Goals: In April 1984, four of the Red Brigades' key leaders wrote a communique from their jail cells. In the open letter, the leaders proclaimed further armed combat as futile. The Red Brigades essentially ceased to exist with this letter. In their words, "The international conditions that made this struggle possible no longer exist." (Xavier Raufer, "The Red Brigades: Farewell to Arms," Studies in Conflict and Terrorism, 1993, Vol.16)
However, the legacy of the Red Brigades continues to this day. Following the release of this letter, two splinter groups broke off from the Red Brigades: the New Red Brigades/Communist Combatant Party (BR/PCC) and the Red Brigades/Union of Combatant Communists (BR/UCC). The BR/PCC specifically has chosen to continue in the ideological and violent path of the Red Brigades.

Akili ndogo kama ya chura...! Ukiitwa David maanake wewe ni mfalme wa zamani wa Israel...? Ukiitwa Julius maanake wewe ni Julius Caesar...?
 
CHADEMA ni chama cha wavuta bangi tu. Ukianzia na Wabunge wake mpaka Red Brigade yao wanayotaka kuanzisha.
Umevuka mstari kwa mbali. Ulikutana wapi na wabunge wake wakiwa wanavuta bangi?


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nimepata picha kwa nini kila siku Mwigulu anadai Chadema ni cha Wakatoliki na kwa nini mapadre na kulipuliwa mabomu aliyotoka nacho china kanisa anaamini ni wafuasi wa chadema. Ikumbukwe anaamini pia kuwa yeyote mwenye mafungamano na Italia ni Mfuasi wa RED BRIGADE na ndio maana yule mlipuaji pamoja na kukamatwa na wananchi na kukabidhiwa polisi mpaka leo polisi wanakanusha kumfahamu, kama vile walivyomtorosha yule aliyerusha bomu la kufanana na toka kiwanda kimoja lililorushwa kwenye mkutano wa Chadema. Naamini kuwa warushaji wa mabomu haya mawili wote walipewa na mtu mmoja na maelekezo yalitoka kwa mtu huyohuyo ndio maana style zinafananana.
 


[TD="bgcolor: #FFFFFF"] MALEZO yaliyotolewa na viongozi wa CHADEMA kwamba kitaandaa mafunzo ya ukakamavu kwa vijana wake kwa minajili ya kujilinda yamechokonoa mengi. Polisi haraka haraka wakasema ni jambo lisilokubalika. Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, akakema upesi upesi. Na mjadala ukaanza katika jamii yetu kuhusu kauli hiyo. Binafsi kimsingi sipendelei dhana ya vyama vya siasa kuwa na vikundi vya kujilinda ambavyo vinakuwa na sura kama ya mgambo. Lakini si wakati wote unafanya yale unayopendelea. Kuna wakati unalazimika kufanya mambo usiyopenda ikiwa busara na hekima inataka ufanye hivyo. Mathalani, wengi wetu hatupendi kuchomwa sindano, lakini unapokuwa mgonjwa na wataalamu wakakuambia tiba yako ni sindano, unatakiwa ukubali kuchomwa sindano japo inauma. Usiwaone watu wanaofanya kazi za suluba ukadhani wanafurahia na kupenda, la hasha, ni kwa sababu kusudi maisha yaendelee lazima wateseke na kuvuja jasho jingi. Kwa hiyo ingawa sipendelei vyama vya siasa kuwa na vikundi hivi vya ulinzi, kwenye hili la CHADEMA nalazimika kutafakari zaidi kwa sababu kadhaa.
Sababu ya kwanza na ya msingi ni kwamba chama hiki kimekumbana na kadhia nyingi katika mikutano yake. Vifo vimetokea katika shughuli zake na hakuna maelezo yanayoeleweka hadi sasa.
Bomu lilipolipuka kanisani huko Arusha, polisi waliwataka viongozi wa dini kuwa macho na kufikiria namna ya kulinda usalama katika sehemu za ibada. Hili ni jambo le hekima. Utakuwa -------- kama unashambuliwa nyumbani lakini hufanyi marekebisho yoyote ya ulinzi wako. Huko huko Arusha bomu likalipuka katika mkutano wa CHADEMA. Na hadi sasa hatuna taarifa za msingi kuhusu mlipuko huo aaidi ya kuambiwa na Waziri Lukuvi eti polisi walipotaka kumkamata mtuhumiwa, watu waliokuwepo kwenye mkutano waliwazuia kumtia mbaroni mhalifu. Ukiidadavua kauli hii maana yake ni kwamba polisi wenye silaha walizidiwa nguvu na raia kumkamata mhalifu. Au kwa maneno mengine serikali inasema kwamba polisi walishindwa kukabiliana na tukio la uhalifu (hapa hatuangalii sababu iliyowazuia kumkamata mhalifu).
Lakini pia huko nyuma katika mkutano mwingine wa CHADEMA tulioambiwa ulikuwa wa kuzindua matawi, aliuawa mwandishi wa habari akiwa katikati ya kundi la polisi. Maana yake nini? Polisi waliokuwepo katika harakati hizo hawakuweza kulinda watu hadi amani ikavurugika na uhai ukapotea. Orodha ya matukio ambapo fujo au damu imemwagika katika harakati za siasa za CHADEMA zipo nyingi. Swali linakuja, ni hadi kitokee nini au afe nani ndipo tutasema kwamba imetosha? Kama sasa mikutano hii imefikia kurushiwa mabomu na bado hakuna hata rambirambi kutoka kwa rais wa nchi kwa chama kilichokuwa mhanga wa tukio hilo, tutarajie watu hawa wajikunje wakisubiri ulinzi kutoka wapi? Nadhani thamani ya uhai ni kubwa kuliko kitu chochote. Kama kuna sheria yoyote ambayo utekelezaji wake unaondoa uhai, basi sheria hiyo ungeweza kuiita ya kigaidi. Licha ya kutokuwa muumini wa vyama vya siasa kujilinda vyenyewe kwa makundi yake, lakini kwa hali iliyofika ambapo hadi bomu linarushwa kwenye mkutano halali, basi nadhani ni hekima kwa chama husika kufikiria upya namna ya kujilinda. Lakini pia nina sababu nyingine ya kutowashangaa CHADEMA kwa uamuzi wao huo wa kujipanga kujilinda. Hii ni sababu ambayo hata polisi wenyewe wanakiri. Kwamba suala la ulinzi na usalama si suala la polisi peke yake. Ni suala la kila raia.
Wanachama wa CHADEMA nao ni raia wa nchi hii. Wana haki lakini pia wajibu wa kujilinda na kuwalinda wengine ili wawe salama. Na haki hiyo inaongezeka zaidi tunapoangalia historia ya matukio waliyokuwa nayo.

Tulishaambiwa kwa uhakika kabisa kwamba hatuna polisi wa kutosha kufanya ulinzi wa mtu na mtu. Sasa kwa nini CHADEMA wakiamua kujilinda inakuwa nongwa? Wakianzisha jeshi tutawaambia hapana na watashtakiwa. Wakisema wanaanzisha vikundi vya kufanya fujo tutawakemea na kuwazuia. Lakini wakisema wanajilinda tutawashangaa wanaowashangaa kwa nini wanajilinda.
Pia nina sababu nyingine ya ziada inayonifanya nisisite japo sipendi kukubaliana na mantiki ya CHADEMA ya kuanzisha mikakati ya kujilinda. Sababu hii ni kwamba hata wenzao wana vikundi kama hivi. Chama tawala kinafahamika sana na kikundi chake maarufu cha Green Guard ambayo tafsiri yake ni Walinzi wa Kijani. Ikiwa chama hiki ambacho mwenyekiti wake ni rais wa Jamhuri ya Muungano na ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu bado kinaona ulazima wa kuwa na ulinzi wa kichama wa ziada, kwa nini wanadhani wapinzani ambao ndani yao hawana mtu mwenye uwezo wa kutoa amri hata kwa mgambo wa jiji wasiwe na mikakati yao pia ya kujilinda? Mwenyekiti wa CCM ni rais wa Muungano. Ukweli umedhihirika kwamba huwezi kumtofautisha mtu huyu anapokuwa rais au mwenyekiti. Anakuwa mtu huyo huyo mwenye mamlaka hayo hayo kwa wakati mmoja. Huyu analindwa muda wote na vyombo vya dola. Je, mwenyekiti wa chama cha upinzani analindwa na nani? Baada ya tuliyoshuhudia mnataka atafute ulinzi gani? Akafanye tambiko? Lakini kubwa zaidi ni ujasiri unaopatikana wa kuwazuia CHADEMA wasianzishe mikakati hiyo ya ulinzi lakini macho yakifumbwa kwenye kundi la chama tawala. Je, sheria zetu sasa zinabagua? Wapo walio juu na walio chini ya sheria? Kama kweli uanzishwaji wa vikundi hivi ni kinyume cha sheria za nchi, basi vipigwe marufuku katika vyama vyote. Tusidanganyane kwamba wahusika hawajui kwamba CCM ina kikundi hiki cha ulinzi na wala hakikuanza leo wala jana. Tusitake watu wafuate tunayohubiri bila kufuata matendo yetu. Mahubiri ya vitendo yana nguvu kuliko maneno. Mwenyekiti wa CCM anaposhtushwa na hatua ya CHADEMA aanze kuvunja kundi hilo la Green Guard. Jambo jingine lililonifanya nitafakari upya uhalali wa wale wanaopinga CHADEMA kuandaa mikakati ya ulinzi ni ukweli kwamba sasa hivi hata ulinzi rasmi katika maeneo mengi umebinafsishwa kwa maana kwamba kuna makampuni binafsi mengi ya ulinzi tena yanayolinda na kutumia silaha za moto. Je, ikiwa CHADEMA watasema hawataanzisha kundi lao la kujilinda na badala yake wakakodisha kampuni ya ulinzi kuwalinda popote wanapotaka, polisi na wengine waliokasirika watafurahi? Kama mtu binafsi na taasisi nyingine zinaruhusiwa kujipangia mipango yao ya ulinzi na kutumia walinzi wenye silaha za moto ambao si askari wa majeshi yetu, iweje CHADEMA wakifikria pia mikakati yao binafsi ya ulinzi ionekane wanafanya jinai? Na hapa niongeze kwamba bila shaka serikali inatambua sana umuhimu wa ulinzi binafsi ndiyo maana hata imeruhusu silaha kuwa zinauzwa. Hizi si silaha za kuwindia swala au nyumbu. Ni zile silaha za kujilinda. Tukitazama mwenendo mzima wa maudhui ya ulinzi katika kipindi hiki cha uhuria wa soko sioni namna ambavyo unaweza kuwashangaa CHADEMA kuanzisha mikakati yao ya kujilinda. Kikubwa ambacho nadhani tunapaswa kushangaa kwa pamoja na kujiuliza ‘kulikoni?' ni imekuwaje tukafika hapa. Imekuwaje vyama vya siasa kikiwamo chama tawala wanadhani hawako salama bila vikundi binafsi vya ulinzi? Tukiweza kupata hilo jibu tujisahihishe. Tusilazimishe watu wasitumie dawa wakati ni wagonjwa!

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Juvenalis Ngowi
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]
[/TD]
 
Back
Top Bottom