Dar kumepambazuka. Walio madarakani waliahidi kuwapatia wananchi maji lakini hadi leo kero ya maji iko palepale. Ni haki ya wananchi kuwaambia kuwa wameshindwa kazi! Chama tawala fanyeni kazi wananchi wapate nafuu ya maisha hali ni ngumu sana huku mitaani.
Wana Jf,
Katika mikutano na semina za chadema vurugu ni sehemu yake! Tukumbuke kule Arusha Mwigamba na Lema,
Dar Zitto na Slaa! Mikutano ya cdm pia huwa na vurugu za kutosha mpaka mabomu.
Lakini hiki walichokifanya kwa Naibu Waziri wa Maji Mh.Makalla hakifai hata kidogo na inabidi kikemewe kwa
nguvu zote na Watanzania wenye mapenzi mema. Ikumbukwe Mh Waziri yuko katika ziara ya kukagua
shughuli za Maji ambapo maji ni kero kubwa kwa wakazi wa Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba, mwakani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.