Chadema, CCM, CUF zakabana koo Z'bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema, CCM, CUF zakabana koo Z'bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 7, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]:A S 465:[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
  VYAMA vya siasa vitatu, Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinachuana vilivyo uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini, visiwani hapa.

  Uchunguzi uliofanywa wiki moja tangu kipenga cha uchaguzi huo kipulizwe, vyama hivyo vitatu vimeonyesha kung'aa kutokana na kusambaza mabango na bendera karibu kila kona ya jimbo hilo, huku vikiwa ni gumzo kwenye maskani mbalimbali.

  Hii inaashiria Chadema safari hii wamejidhatiti katika siasa za Zanzibar ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikitawaliwa na vyama viwili, CCM na CUF.

  Chadema kwenye uchaguzi kimemsimamisha Maalim Ali Mbarouk Mshimba, kuwania kiti hicho, CCM, Mohamed Raza na CUF Salma Hussein Zarali.

  Mambo yanayoashiria Chadema kwa mara ya kwanza kuingia na nguvu kubwa kwenye uchaguzi wa Zanzibar ni kusikika kwenye magumzo ya vijiwe sawia na CCM na CUF.

  Tayari Chadema kimeaanza kulia kufanyiwa rafu baada ya watu wasiojulikana kusambaza waraka unaodai kuwa Maaskofu Tanzania Bara wanakibeba chama hicho.

  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Hamad Yusuf Musa amkiri kupata taarifa za kusambazwa kwa waraka huo lakini akauelezea kuwa ni propaganda chafu dhidi ya chama hicho baada ya kuonekana kuwa na nguvu jimboni humo.
  CUF kwa upande wake, kimeanza kampeni hizo kwa kishindo huku kikitumia uzoefu wake wa siasa za Zanzibar kutaka kuibuka mshindi.


  Kwa upande wa CCM, chama hicho kimeendelea kujidhatiti kwa kampeni za wazi na vikao vya ndani katika kuhakikisha mgombea wao, wananyakua kiti hicho ambacho kilikuwa kikishikiliwa na Mbunge Mussa Khamis Silima aliyefariki dunia Agosti mwaka huu.

  Mgombea wao, Raza ambaye ni mwanasiasa na kada wa muda mrefu wa chama hicho, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini mojawapo ikiwa ni ya mshauri waa Rais Mstaafu, Salmin Amour, kuhusu mambo ya michezo.
  Vyama vingine ambavyo navyo vinajiwinda katika kuwania kiti hicho ni TADEA ambao wamemteua, Khamis Vuai Haji kuwa mgombea wao na AFP, Rashid Yusuf Mchenga.
  :A S 465:
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kama CDM ikipata japo ushindi wa pili, itakuwa umejipanga vizuri
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mwaka kazi ipo peoples' power hadi Zanzibar
   
 4. M

  Mbonafingi Senior Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akikusiki! Atakurupuka kama swala aliyefurusgwa na mbweha. Maana brain yake ikisikia CHADEMA anapata degedege. Mungu tubariki wanao tuepushe na akina Faiza Foxy
   
 5. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tanzania ni moja, CHADEMA lazima waweke nguvu kwenye siasa za Zanzibar tena nguvu kweli kweli hadi tupata wawakilishi na wabunge kutoka Zanzibar; Hii ndo njia nyingine ya kuthibitisha kuwa CHADEMA inauwezo wa kukabiliana na hali tofauti tofauti na kufanikiwa
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Fuatilia ujue uchaguzi uliopita walikuwa namba ngapi.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kama zanzibar ni muhimu mbona tundu lisu aliwatukana wazanzibar bungeni? ile ilikuwa technical mistake kubwa sana.
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,818
  Likes Received: 2,300
  Trophy Points: 280
  hakuwatukana wazanzibar, alikuwa anawajibu CUF na siasa zao za kujikomba komba kwa CCM as if wao ni small hse.
   
 9. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Chadema,CCM,CUF.....RESPECTIVELY.
   
Loading...