Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Tundu Lissu ni kila kitu kwa CHADEMA ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuwepo kwake kunawafanya wabunge wengine wajiamini kwa vile ni yeye ndiye anayewaelekeza vifungu vya kusoma pindi wanapoomba Mwongozo wa Spika (Rejea Mwongozo wa Saed Kubenea juu ya wabunge kuvuliwa shanga). Kinyume chake, kutokuwepo kwake kunawafanya wabunge wa Upinzani wakose kabisa ujasiri si tu wa kuomba muongozo bali hata wa kuingia bungeni na kushiriki mijadala. Hivi uliwahi kuiona Real Madrid ya sasa ikicheza bila ya uwepo wa Christian Ronaldo? Jibu utakalopata lisogeze kwa CHADEMA bila ya Tundu Lissu.
Baada ya Tundu Lissu kuondolewa kutoshiriki vikao kadhaa vya bunge hadi Januari 2017, CHADEMA na kambi rasmi ya Upinzani watapata wakati mgumu sana bungeni. Hawatakuwa na ujasiri tena wa kuomba miongozo. Hawatakuwa na ujasiri tena wa kushinikiza jambo fulani bungeni. Hawatakuwa na ujasiri tena wa kuchangia hoja. Ujasiri watakaokuwa nao ni wa kutoka nje pindi mambo yanapowaendea mrama.
Natafakari sana hoja ya Mbowe kususia Bunge hasa baada ya akina Tundu Lissu kupewa adhabu hiyo. Ukiunganisha dots utagundua kuwa tatizo si Dr Tulia Akson bali tatizo ni akina Lissu kutokuwepo Bungeni. Najaribu kuwaza hivi ikitokea Dr Tulia akaongoza vikao vyote vya bunge nini hatma yake? Najaribu tu kuwaza na naamini pia na wewe msomaji unawaza kama mimi.
Hakika Lissu umeacha pengo kubwa sana ambalo hakuna wa kuliziba bungeni ndani ya Kambi ya Upinzani. Daima wana CHADEMA wanakulilia Tundu Lissu. Watakumiss sana kwa kipindi hiki hadi Januari 2017. Mwenyezi Mungu akujaalie ujasiri na utulivu huku akikujaza siha njema ili urejee tena Bungeni ifikapo Januari 2017