CHADEMA badilikeni

CHADEMA badilikeni

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,512
Reaction score
40,197
Siyo siri kwamba asilimia kubwa ya Watanzania hasa vijana ni wapenzi na wanaikubali sana CHADEMA. Kwa hali ilivyo sasa hata chama Tawala wameacha kutekeleza Ilani yao na sasa wanajibidiisha kutekeleza Ilani ya CHADEMA kwa vitendo huku wakiilaanai kwa maneno.

Ushauri wangu kwa viongozi wa CHADEMA ni huu, Pamoja na kufanya mikutano mingi ya M4C nchi nzima pamoja na mikutano ya NDANI, inapaswa sasa kwenda hatua za mbele zaidi. Kuna wapenzi wa dhati wa CHADEMA ambao wengi ni wapiga kura ambao kutokana na ufinyu ama sababu zisizozuilika hawawezi kufika ama kuhudhuria mikutano ya CHADEMA.

Ni vyema Kamati ya Utendaji ikaona vyema kuandaa vitini na machapisho ya manifesto ya Chama ili kuweza kuwafikia wengi zaidi. Simple folding handout inaweza kubeba ujumbe mkubwa na kuwafikia wengi zaidi. Hii itazidi kusimika chama kwenye nyoyo za Watanzania wengi. Matamko na press releases ni cheche tu lakini badilikeni sasa kwa kutuletea machapisho sambamba na harakati zilizopo za vuguvugu la Mabadiliko.

Kumbukeni kuwa CCM ilipendwa sana lakini sasa inachukiwa sana. Inafutika kwenye akili za wengi na walio hai wanailaani itokomee. CHADEMA jifunzeni kupitia anguko la CCM maana walipoacha kuishi ktk walichokiamini ndipo walipoanza kuporomoka...
 
Back
Top Bottom