CHADEMA, Azisheni Mashamba Makubwa ya Mfano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Azisheni Mashamba Makubwa ya Mfano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Mar 26, 2011.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pamoja na kufanya shughuli za kila siku na za kimkakati katika kukijenga chama chenu, nashauri muanzishe kampuni kubwa ya uwekezaji na kuanzisha mashamba makubwa ya mfano katika sehemu mbalimbali hapa nchini kwa kushirikiana na wanachama wenu na Watanzania wengine. Mazao yanayopendekezwa muyape umuhimu wa juu ni Mpunga, Kahawa, Korosho, Alizeti, Chai, Mahindi, Maharage, Matunda ya aina mbalimbali. na miti ya mbao. Kwa upande wa miti ya mbao wekeni lengo la kupanda angalau ekari 25,000 kia mwaka kwa angalau miaka 25 mfululizo Pia angalieni uwezekano wa kujenga viwanda vya ukubwa wa kati kwa ajili ya kusindika mazao ya wakulima wetu na kuyaongezea thamani kwa ajili ya soko la ndani na nje.

  Kwa upande wa mtaji, tumieni sehemu ya ruzuku mnayopata kila mwezi toka Serikalini na pia uzeni hisa za kampuni mtakazoanzisha kwa wanachama wenu na Watanzania.
   
Loading...