CHADEMA au CCM Siwaelewi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA au CCM Siwaelewi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizotaka, Mar 7, 2012.

 1. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Great Thinkers, niseme yanayonikera nchi hii. mimi naangalia matatizo ya nchi hii na jinsi nchi inavyokwenda naona hatuna dira wala mwelekeo uanaoeleweka. Kinachosikitisha ni kwamba vyama vya siasa havina mwelekeo wala mwonekano unaotakiwa kuwapambanua viongozi wake moja kwa moja mbele ya jamii yetu. Jina kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo au CCM, halitoshi kukielezea chama, je hawa ni wajamaa au mabepari? wanafuata siasa zipi? Hii itasaidia kujua watatekeleza vipi sera zao, kijamaa au kibepari? Tutaendelea kuwa watumwa wa IMF na WB? Kiitikadi hasa wanafuata siasa za mrengo upi? kwangu hili ni muhimu na silioni.

  Jingine ni kutenganisha chama na serikali, hili ni balaa lingine. Tutajaongozwa na wahuni hapa tusipoangalia. Uwepo mfumo unaotenganisha vitu hivi viwili. haiwezekani rais aogope kufanya mambo ya kitaifa kisa wanachama,eti nitawaudhi wanachama. upuuzi huu.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni kweli tunatakiwa kuliangalia hili na kuvifahamu hivi vyama kabla ya kuvipa ridhaa ya kushika dola. Lakini najaribu kuviangalia japo si kwa undani sana ninabaini kuwa vipo vyama vya siasa hapa nchini ambavyo hata hadhi tu ya kuitwa vyama vya siasa havina, pengine vinaitwa hivyo kwa sababu tu vilitimiza masharti ya usajili lakini angalia jinsi vinavyoongozwa na jinsi viongozi wake wa ngazi mbalimbali wanavyopatikana... unaweza kukubaliana na mimi kuwa vingi ni makampuni ya watu fulani na watu hao siku zote hawako tayari kuachia nafasi zao kwa watu wengine japokuwa wapo wanaoonekana kushindwa kuviongoza. Ubinafsi huo ndiyo unaosababisha fukuza fukuza ndani ya vyama na mwisho wa siku vinajikuta ni vya kuibuka na kuzama. Iko wapi NCCR Mageuzi ya miaka 90 chini ya Mrema? Iko wapi CUF ya mwanzoni mwa miaka ya 2000? Sasa hivi wapo CHADEMA lakini nao wape muda tu, nadhani baada ya miaka michache ijayo inaweza kufuata nyayo za NCCR Ya Mrema na CUF.
   
 3. R

  Romee Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tunakujua ndoto yako ni kuona chadema inaanguka kama cuf na nccr,pole sana utasubiri mpaka yesu atarudi.chadema ni chama mbadala kufa utakufa wewe na chadema iko na inaendelea kuwepo.
   
 4. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa great thinker hapo unaaribu, kwani cdm ni mabepari au wajamaa, maana hawa maandazi wa ccm hawaeleweki, katiba wanayoisimamia ni ya kijamaa japo ni kopi ya uingereza, mambo yanavyokwenda kwa uasilia wake nikibeparibepari hawaeleweki ni mauzauza matupu. Ndo maana nikauliza hili mkuu
   
Loading...