Chadema acheni kupiga mayowe jengeni chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema acheni kupiga mayowe jengeni chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Sep 17, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Chama kinachojinasibu kwamba ni cha demokrasia na maendeleo hapa nchini huku kikishindwa kutekeleza nadharia yao ya demokrasia kwa vitendo kwa kujaribu kuzuia wanachama wake kwa hila mbalimbali kugombea nafasi za juu chamani kimekua kikijinasibu na kupiga mayowe mengi kuulaghai umma na hasa wafuasi wake ambao wengi ni wenye upeo wa wastani juu ya masuala ya kisiasa kwamba kinao uwezo wa kuiangusha CCM madarakani na kwamba eti CCM inakihofia jambo ambalo kama wafuasi wake wangekua na upeo wa kutosha wangebaini kwamba si jambo rahisi na halitekelezeki kirahisi kama viongozi wao(baadhi) wanavyojaribu kuliweka.

  Ukweli ni kwamba chama iko bado kina safari ndefu sana na wafuasi wake wana upeo wa kutosha wangeweza kuwahoji kwanza viongozi wao ilikuaje chama chao ambacho wamekua wakiwaaminisha kinao uwezo wa kuchukua dola na kina mtandao mpana kikapata viti 23 tu vya ubunge kati ya viti 239 vilivyokua wazi tanzania nzima tukiacha suala la urais ambalo linaeleweka na lilieleweka kuwa ni ndoto kwa chadema kushinda kama alivyopata kutabiri na kuandika mhariri mmoja kwenye gazeti lake kabla ya uchaguzi mkuu uliopita lakini akashsmbuliwa vikali na mashabiki wa chadema wenye upeo wa wastani ambao walijazwa na kukaririshwa wimbo wa ushindi bila maadalizi ya kutosha???

  Naomba kuwasilisha huku nikiwaomba wapenzi wa chadema mtoke usingizi mfunguke na kutafakari matokeo mabovu ya ubunge kwanza kabla ya kufikiria urais.

  Nawasilisha rasmi
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu nakuunga mkono ila hapo kwenye upeo wa wastani fafanua zaidi ili watanzania waweze kukuelewa
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Subiri matusi sasa.
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Usijali mwezi ujao kuna uchaguzi mdogo kata kama 28 hivi. Utaona kama kinachosemwa na CHADEMA ni maneno matupu au wewe ndio una upeo mdogo na upofu.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenifurahisha sana pale uliposema, wafuasi wa CDM ni wa upeo wa wastani kwenye masuala ya siasa. Maneno yako yananifanya nami kujiuliza swali hili:
  Hivi kuna ususiano wowote kati ya elimu za viongozi wa CHADEMA na siasa zao za shari?
  Hivi mbona, HALIMA MDEE, ZITTO KABWE, JOHN MNYIKA na wengine wenye angalau elimu ya wastani ndani ya CDM hawako kwenye M4C? Sasa napata jibu kwamba, hawa jamaa wangekuwa kwenye M4C hata mauaji yasiyo ya lazima yasingetokea. Nina wasiwasi na elimu ya Mbowe, SLAA ni wazi kuwa elimu yake ni ya kuongoza watu kiroho na siyo kisiasa na kwa maana hiyo sishangai kuona akiongoza vurugu kwa vile tayari alishaasi wito wa kueneza amani, pale alipoamua kulivua joho la Upadre.
   
 6. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nashangaa hawa jamaa wako busy kudai slaa ndio alistahili ama wengine wanaenda mbali zaidi kwa kudai ndie rais wao wakati walishindwa kutumia ushawishi na ushabiki wao kumpa wabunge wa kutosha rais wao huyo,sijui hiyo serikali yenyewe angeiundaje au ataiundaje bila wabunge,ni kichekesho ndio mana nasema wana chadema wengi ni misukule wanapelekwa pelekwa na kuburuzwa na viongozi wao hasa slaa,anawaburuza sana huku akijua wazi kwamba anazichosha akili zao kwa kuwatamanisha urais ambao hana uwezo wa kuupata bali anaona raha tu kuitwa mgombea urais wa kudumu kwa tiketi ya chadema
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280
  Sasa Chadema wanapiga mayowe gani? Malalamiko mtaani ni ya wananchi mkuu Chadema wanafanya siasa tu kama sehemu ya majukumu yao yaliyofanya kisajiliwe kama chama cha siasa.

  Tunajadili matatizo yetu kama Watanzania kama wewe ni sehemu ya mfumo wa kinyonyaji na unafaidika kwa namna yeyote jiandae na dhoruba.unafikiri leo Chadema ikifa nchi itatulia? Wale waislamu walioandamana malalamiko yao yameletwa na Chadema?

  Endeleeni kudanganyana vijiweni lakini mtaani kuna vijana wenye elimu wengi tu wenye kiu ya mabadiliko na sasa hawana mbadala zaidi ya Chadema na mnavyoiandama Chadema mnazidi kuwatia hasira Wananchi tu!
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Magamba mmeamka lakini hamjajipanga......naona ile ofisi yenu ya UPANGA sasa iko kazini
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Unaliangusha hilo jina mkubwa,mwenyewe Julius malema ni kamanda wa ukweli.
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tumeujua nawewe UPEO wako! viti 23 kati ya 239 safi sana 1+1=3 karibu rasmi
   
 11. d

  dotto JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakienda kufungua matawi ili wapate wanachama ambapo ni kujenga chama WANAUWAWA na CCM. refer: Mwangosi R.I.P.
   
 12. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hivi mnyika si ndo mlisema hana adabu leo anaonekana ana akili,kama cdm ni chama cha mayowe acheni basi kuwaua wananchi kwenye mikutano yao.ni usahaulifu wa kitanzania tu na upuuzi wa baadhi ya watu kujisahaulisha sijui kwa makusudi au bahati mbaya.polisi na ccm hawakuanza leo kuvishambulia vyama vya siasa na mikutano toka kwa lyatonga tukayaona kwa cuf.na mpaka sasa mauaji ya wana cuf bado yana rekodi nyingi ya vifo kulinganisha na cdm.lakini leo mmejisahaulisha na mnataka na wengine mtusahaulishe.slaa angependa shari angeshaivuruga hii nchi siku nyingi hata hivyo cdm gari kubwa na safari hii mtawaua hata baba na mama zenu maana wapo mbioni kuisapoti cdm.hata hivyo mtake msitake shida za watz hazihitaji tena kuelezwa na cdm au nani,kama sio woga na ustaarabu wa watanzania hii nchi kwa hali hii ingeshalipuka siku nyingi sana na hata cdm ikifa leo tz italipuka tu.
   
 13. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Slaa na Mbowe ndiyo wamekiletea chama umaarufu, sasa mnaomba nafasi zao zichukuliwe na wengine hili kidhoofike mfurahi
   
 14. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we tazama cuf wamezindua mchakamchakawatafanya raha mustarehe lakini wakianza chama kubwa utasikia mara risasi mara fulani kafa tuweke uwanja sawa wa kidemokrasia halafu kila mtu ajigambe kihaki.elimu haiongezi busara.
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hao vijana kama kweli mnataka tuamini wapo mbona waliwawezesha kupata viti 23 tu vya ubunge kati ya viti 239,mna uhakika wote wanawaunga mkono kweli?hapa panahitaji tafakuri ya kina
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kweli wamejitahidi lakini kufikisha viti 29 bungeni si lelemama!sasa yanahitajika mawazo mapya ili viti viongezeke
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Anazungumzia vya majimbo sio special seats mzee,ni kweli mmeshinda mara 23 tu majimboni,vingi mmepata vya kina mama ndio vinawatia kiburi lakini majimboni mmekataliwa vibaya licha ya operesheni sangara ambayo sasa mnaiit m4c,wizi mtupu wa kichagga
   
 18. status quo

  status quo Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Those are mere figures you moron they require analysis . from 5 seats to 29 seats is a growth rate of 480% so it means that interms of growth CDM outperformed all the political parties in tanzanian political arena and if CDM maintain this growth rate, And offcourse they are ( arumeru case study) the will win over 140 seats majority in 2015.
   
 19. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Chadema ni genge lisilokuwa na uongozi madhubuti, chama kinachoongozwa na JAZBA pasipo uelekeo maalum
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuwa na wabunge 23 halafu ukasema umeshinda urais, halafu hapo hapo unasema una nguvu ya umma.
   
Loading...