CHADEMA "achaneni" na Dr.Slaa (Ushauri)

Kweli CHADEMA ni cha Watanzania na Kila Mtu anaruhusiwa kutoa Maoni yake.Tatizo ni Kwamba Maoni yako ni Dhaifu Mno.

Kama ni dhaifu mbona unatokwa na mapovu.Ukiona halikuhusu/halina maana piga chini.Watanzania mbona mnapenda sana "ndio mzee"?Halafu huu ni ushauri,na wala sio lazima.
 

OK, CHADEMA tumekataa Maoni yako.
 

Hivi ushauri unaotoa lazima ukubaliwe? Basi si ushauri ni amri.

Somo la bure.

Jifunze kutumia njia ambayo itahakikisha ulichokikusudia kinafanikiwa. Kama hakitafanikiwa achana nacho. Ndiyo maana nimekushauri upitie kwenye ofisi za Chadema karibu na ulipo ndio utaratibu wa kusikilizwa maoni yako.
 

Katoe ushauri katika vikao halali vya chama.
 
ok. naomba nione ushauri wako kwa CCM na jinsi inavyofanya siasa zake hapa nchini. Put a particular emphasis on Mwigulu Nchemba (kama jinsi ulivyomtaja dr. slaa). Come up with a balanced opinion wewe mwenye uchungu na nchi!

Siku zote unamshauri unayempenda.Inawezekana hamkubaliani na ushauri wangu.Sawa haina tatizo.Nia yangu ni njema tu.Ila siwezi kuwashauri CCM.Hapa walipofikia,hawashauriki.Kwa mfano,umjadili Mwigulu Nchemba kwa lipi?Kwangu kumjadili Mwigulu Nchemba ni kupoteza muda.Zaidi wapenda busara wakishika dola,Mwigulu ashikiliwe.
 

Asante kwa somo lako.
 
Mlihangaika sana na ZZK chama makini kikatulia mmeanza tena ee??

"To know the enemy is half the victory"
 

Sijui kwa nia yako njema uliyojipambanua kuwa nayo unaweza kuitumia kumsauri baba yako mambo ya kifamilia sokoni?
 
Chadema wanawekeza kwa wananchi, tatizo lenu wanaCCM mbamuogopa Dr. Slaa mno!

hivi umemwelewa mleta hoja au? mtoa mada usipoteze muda wako kushauri hiki chama tunakipenda sawa ila jf inawadanganya viongoz hawajui hawa wa key-board hata kura hawapigi vijijin ndo kuna kura
 
Dr. Slaa anakunyima usingizi eeh!! Pole sana!! Nakumbuka JK baada ya kutangazwa mshindi 2010 alisema " tulibidi turudi mara mbili tatu katika sehemu nyingine kufanya kampeni upya".

"Cowards die many times before their death" Shakespeare
 
Unaweza kutafsiriwa vibaya kutokana na namna ilivyotumia lugha tatanishi kwenye uandishi, vinginevyo yale mazuri yatazingatiwa na pumba zitaachwa!
 
Sijajua Plan B ya CHADEMA.Lakini hali hii kiendelea hivi,na kama hakutakuwa na makubaliano (Pinda anasema wapigwe tu),ili kuepusha maafa zaidi kwa wanachama wao,watanzania wenzetu,hebu wajaribu kubadilisha mbinu.Mikutano ya hadhara ambayo haina ulazima wa kuwepo Viongozi wakuu wa chama waachane nayo.

Sasa waanze kampeni ya na na viongozi wa vijiji,kata,wilaya n.k.Kitu cha msingi wawawezeshe.Mikutano mikubwa ifanyike pale panapokuwa na ulazima.[/QUOTE]

Ushauri mzuri ila unajichanganya hasa point ya kwanza ambayo imeshindwa kutofautisha charistimatic cum born leader na self-imposed leader. Labda kosa si lako maana vyama vingine na hasa CCM hawana viongozi wenye sifa kama za Slaa. Slaa ni koo chaa uongozi na anaongea lugha ambayo watu wanaelewa na anayaishi yale anayoyasema kwa vitendo. Ndio maana na wewe unakiri amekuwa tishio kwa watawala ambao wanatembea chini ya busati si kwa sababu ya physical power bali intellectual power. Kila muungano wa kiitikadi ungependa kuwa na mtu wa aina kama kiongozi lakini cha kushangaza unashauri kinyume chake.Pili ukishauri basi jitofautishe walau kidogo wasiiona mbali na pua zao. Mshahara halali tena ambao wabunge wanapata na sio marupurupu kama ya wabunge umekuwa ni silaha wanayoitumia CCM kumsema Dr.Slaa ambaye amejitoa kukisaidia chama. Yeye si wakala wa meli wala mfanyabiashara wa meno ya tembo. Muda mwingi ni yeye na chama. Kwanini mshahara umekuwa nong'wa. Ukipungua polisi wataacha kuipiga wana Cdm? Ukipungua mabomu ya machozi na maji ya kuwasha na kesi za kubambika zitaisha? Waziri Mkuu na Wassira watakuwa na hofu ya Mungu. Hivi ndio adui wa demokrasia na sio Dr.Slaa
 
Sijui kwa nia yako njema uliyojipambanua kuwa nayo unaweza kuitumia kumsauri baba yako mambo ya kifamilia sokoni?

Kamanda Ben, mleta uzi msamehe bure may be his is reflecting a problem that we have and is there to stay if we do not remove CCM through ballot box. The problem is fragile education system that has been architected by CCM in a number of ways that need not repeat. Matokeo ni kuwa na watu ambao wanashindwa kujieleza and keep themselves busy beating about a bush. Huwezi kusoma shule za kata tena zisiwe na walimu au zinao wachache lakini wa fasta fasta na ukategemea atajenga hoja ieleweke. Huyu ni wa kusamehe na kwenda naye taratibu maana elimu haina mwisho lakini kwanza ajitambue na kuwa tunaye bado online atajaribu kujiona ni wapi alipokosea. Ukiacha pale ambapo ni controversial kama ambavyo wengine wameanisha elimu vijijini na pembezoni mwa miji ni muhimu katika kukijenga chama. Elimu ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ni muhimu lakini isitoe umuhimu wa public rally. Hii ya nyumba kwa nyumba inaweza kukuoyesha nguvy yako maana utajua unao wanachama wangapi na je wanazo sifa za kupiga kura. Ukishakuwa na list hiyo ni rahis kufanya tathmnini dakika za mwisho kujua wangapi watakuwa tayari kupiga kura maana watakuwa na shahada ambazo ni valid na hazijanunuliwa kwa hila
 
Mtoa mada nadhani nimemuelewa, hata kama alidhani atakuwa ataoa kwa kudhani anaiharibu CHADEMA lakini ukweli ikiwa plan B yaani kuelimisha umma kwa njia ya nyumba kwa nyumba itakuwa ni zaidi ya kufanya mikutano ya hadhara, maana wananchi hawatakubali kutishwa kwa lolote kwan watakuwa wameelea vizuri namna ya kujitafutia ukombozi wao wenyewe kuanzia katika familia, mashina na kata zao. Nadhani atakuwa anamaanisha kuwa BIG RESULTS ni muunganiko wa matokeo chanya kwenye mirija mingi....
Mkuu, suala la ruzuku na matumizi yake, milioni 200+, sijui unazionaje, lakini kwa kazi tu za kila siku achana na mshahara wa Dr. Slaa si kitu kabisa. Ni ndogo mno, angalia kazi zinazofanywa ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa magari yaliyoko mitaani kwa shughuli za kichama. Mimi na wewe wenye mapenzi mema tushirikiane kwenye hili, tusaidie kadiri ya uwezo wetu halafu tuhoji pia namna ya matumizi bora ya fedha hizo.
Awe chama chochote kwa huo ushauri mi nadhani anastahili pongezi...Si lazima aupeleke ofisini, popote pale hasa anapodhani utafanikiwa kuufisha ushauri wake kwa haraka zaidi na kupata uchambuzi wa kina inafaa. Hii hoja ya kila kitu kukipeleka kwenye ofisi za chama nadhani ni mifumo isiyo na tija sana hasa katika kipindi hiki chenye muingiliano wa mambo mengi...
 
.

Nakushukuru kwa maelezo yako.Inawezekana kweli tatizo ni elimu yangu.Inawezekana!Hoja ya Dr.Slaa naona haijaeleweka kwa sababu sijaipambanua vilivyo.Nakiri kosa.Lakini sijaona sababu ya wewe "msomi wa enzi za mwalimu" kunishambua,mara nimesoma shule za kata,mara vile.Elimu bila hekima na busara,ni ujinga.Sitaki kufanya kosa la kukushambulia,kama ulivyofanya wewe.Na wala hakuna sababu ya kushindana.
 

Nashukuru kwa ushauri wako.Mimi sina chama,ila nawaona Chadema wako kwenye mwelekeo mzuri ukiachana na kasoro ndogondogo ambazo huwa hazikosekani katika maisha ya binadamu.Nimeandika haya kwa moyo mkunjufu,na wala lengo halikuwa kuwabomoa Chadema.Nakiri kwamba Hoja yangu ya kwanza,sikuieleza kwa kina.Tuepuka dhana ya kwamba kila anayeisema Chadema ni adui,mwisho wa siku,adui ataachwa,kwa kuparamia wasio maadui.Pia tukubali kuyasikia hata yale tusiyoyapenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…