Cha mwanaume cha kwetu chake ni chake

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,787
Reaction score
37,992
Wanaume wengi wamekuwa hawaamini mali zao ni za familia
mali za mwanamke ni zakwao...ndugu wanaume naomba mjitahidi
kuwaridhisha wake zenu ........mmepata mishara weka mezani...mwambie mkewangu mwezi nimepata hiki...unasemaje...usiogope wala kumlazimisha mwanamke aonyeshe mshahara wake..unapofanya hivyo ndipo utakapomwonyesha kwamba mapenzi si hela...hivyo na yeye ataamua kuja siku moja mmewangu nimepata hiki tunafanyaje???chenu kiwe vyenu.....mtaishi kwa amani
 
wanawake wa kihindi tu ndo wanaelewa hilo..
waswahili kazi ni kufuja pesa tu....
 
Hili kuna ukweli, pesa ya mwanamume ni ya familia.
 
Kwa maoni ya wanwake wengi wanaamini hivyo...iala pesaa ya kwetu ni yafamilia
 
wanawake wa kihindi tu ndo wanaelewa hilo..
Waswahili kazi ni kufuja pesa tu....

yaani we acha tu kuna wanawake wengine kweli ukiwawekea hivyo....loh kwa wakwe unakutana na ghorofa...siku unaenda kwa wakwe unashukia kwenye gorofa unaambiwa hii ya shemeji yangu
 
yaani we acha tu kuna wanawake wengine kweli ukiwawekea hivyo....loh kwa wakwe unakutana na ghorofa...siku unaenda kwa wakwe unashukia kwenye gorofa unaambiwa hii ya shemeji yangu

Kwa wale wanawake wenye wanaume wabishi na wasiopenda maendeleo hii ndio dawa yao, unabana kamshahara kako na kujijenga kwenu.
 
mhhhh...
Na wewe pia?????

Mimi nimeongelea kwa wale wanawake wanaoonewa na waume zao, utakuta mwanamke anafanya kazi lakini akipata pesa yote ya mshahara anampelekea mwanaume wake ambaye hapendi maendeleo.
Mbaya zaidi mwanaume mwenyewe awe bahili haonyeshi hata mshahara kwa mkewe, kazi kutaka mshahara wa mke.
 

Hakuna formula ktk ku-manage income za familia isipo kuwa ushirikiano unatakiwa. Mimi bibafsi akaunti yangu ya mshahara ni akaunti ya familia na ATM card anayo mama watoto sasa akifuja pesa atajijua yeye na watoto wake.

Mimi nakuwa na akaunti nyingine ambayo vihela kama vya consultancies ndo natumia lakini nikikwama ndo ntachukua kidogo kwenye akaunti ya familia. Mama anafanya shughuli zake na simuulizi wala anashilingi ngapi, na sita muuliza kwa sababu kama yeye hapendi kuniambia why nimuulize??

Ni kweli kwamba akina mama wengi wa kiswahili/waafrika wana matatizo na kwa mwenye ndoa analijua hilo. Ushauri tu kwa wanaume ni kwamba jitahidi uwe na pesa zako lakini kama unafanya kazi basi mshahara uwe ni mali ya watoto na mama kwani akina mama hawana imani kabisa kwamba ukimwambia kiasi cha mshahara unachopata ataamini kuwa ndicho, mara nyingi wanaamini unawadanganya, sasa dawa ya hilo ni kumpa ATM card iliawe na uhuru na ajue kuwa kweli mshahara ni kiduchu.
 


kaka sina chakusema zaidi ya MUNGU akubariki katika ndoa yako hakika tungepata wanaume kumi kama wewe tanzania basi hata UFISADI tusingekuwa nao
 
wengi katika ndoa za siku hizi japo wanaoana hawazijui HAKI ZA MUME KWA MKE NA HAKI ZA MKE KWA MUMEWE. Wengi wetu tunajua kuwa haki ni kulala kitanda kimoja na .... tu.

Sasa kwa mtuyezifahamu haki hizo kuwa muwazi katika sio tu mapato yako ya mwezi bali pia hata shughuli zako za kila siku na shughuli zako nyingine za maendeleo ya kijamii na uchumi.


Tunaamini kuwa NDOA YA KWELI ni lile inayoongozwa na mapenzi na kuhurumiana na linaloangaziwa na UWAZI
 
Hii inategemea taswira mliyojijengea mwanzo,kama mwanaume aliachiwa gharama zote basi itakuwa hivo mpka kwenye familia! Mwanamke anataka haki sawa, lakini inapokuja kwenye mambo ya gharama na mengine mazito Anasema BABA hayupo! Wakati niko katika uchumba na mke wangu niimgundua kuwa ana tabia ya kuona kuwa mwanaume ndiyo kila kitu! Lakini wakati huohuo akawa hapendelei kunisaidia kazi zangu za ndani kama kuosha vyombo! Alinipa muda wa kumsoma na kumuelewa, na baada ya kuamua kuwa serious na mahusiano nilimpa conditions: 1. Aache kazi awe mama wa nyumbani nimpe kila kitu 2. Aache kazi nimpe mradi awe meneja lakini hesabu zikaguliwe na muhasibu wangu 3. Aendelee na kazi lakini mwisho wa mwezi kila mtu aoneshe hesabu zake za mwezi na faida iingie kwenye maingizo!. Sikwambii alichagua nini, lakini amini nakwambia TUNAISHI VIZURI SANA. Lazima mpange ni aina gani ya mahusiano na mkubaliane kuyafuata kwa misingi mliyojiwekea kwa sababu mkija kutengana sheria haiangalii nani alichangia nini katika nini, MALI INAGAWANYWA IVENLI!!!
 

ni kweli kabisa mkulu mi nakumbuka kuna jamaa yangu alikuwa na gfriend wake yeye alikuwa nyumbani ana mpa kila kitu..akifika nyumbani mwanamke
anamsalimia halo baby za kazi anajibu nzuri..anaingia ndani siku mwanamke akaanza kazi akaanza kurudi hoi mwanaume akawa anauliza polesana siku imeendaje jibu;ooooh darling yaani nilivyoytoka hapa nikapanda bajaji nikafika job piga mzigo nikaenda lunch na sakina tukarudi ndio mpaka mida hii ila nimepata shida kwenye basi......nafurahi sana kukuona tena ma baby.....,hiii iliendelea sasa mwanaume akusoma nyakati mapema...na majibu yake ya shotrcurt ,wakafunga ndoa mwezi tu mwanamke akiulizwa za job mkewangu anajibu na yeye safi huyo kitandani ama jikoni...mwanaume akaanza kuhisi anasaidiwa...,kumbe sio yale aliokuwa akijenga kama gfriend ndio yanamkuta ndoani...so wanaume/wanawake onyesheni maisha yenu live kabla ya ndoa acheni kuact.....haya maisha sio ya kutesana.....,lazima ifike wakatii WANANDOA TUwe WA WAZI.....inasaidia sana....,
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…