soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Watanzania tu wabishi sana hata kisichotakiwa kupinga tutapinga tu, hata kama hatuna uelewa tutapinga almradi tuonekane tuna hoja.
Ni wazi kuwa wako watanzania wanaweza kumudu hiyo nafasi, swali la kujiuliza mna uhakika gani kama walishindanishwa na huyu dada akawapita wote? Jamani mwenye uwezo apewe haki yake, tusilazimishe mambo. Pia, hapa tunapigiwa kengele kuwa tumelala...tuamke wandugu wenzetu wametuzidi. Hivi ni wakenya wangapi wanaendesha makampuni makubwa huko Ulaya, Australia na America? Je, hawakuwepo wazungu wazawa wenye uwezo? Kumbukeni Vodacom iko kibiashara hivyo inataka faida, na inamhitaji mtu wanayeona anakidhi viwango vya malengo waliyojiwekea.
Tusomeshe vijana na watoto wetu, tuwahimize elimu sio kufaulu kwa alama nzuri bali ni kuwa na ujuzi na kuonesha uwezo wa kuutumia. Inauma sana kuzikosa nafasi kama hizi, isiwe sababu kumwaga mapovu bila kuangalia uhalisia.